Kubenea uko wapi, rais anakutafuta kwenye Uzinduzi wa Hostel Chuo Kikuu

hegel

Member
Nov 18, 2016
15
31
KUBENEA UPO WAPI RAISI ANAKUTAFUTA

Leo Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwepo jimbo la Ubungo katika uzinduzi wa hostel mpya za chuo hicho.

Kabla ya kuhutubua alimtaka mbunge wa eneo husika kupanda Jukwaani kusalimia. Cha kushangaza mbunge huyo hakuwepo eneo hilo.

Najua kiprotokali alipewa mwaliko wa ujumbe huu wa Rais kuwepo Ubungo. Kubenea si kiongozi katika ngazi yoyote ya bunge useme majukumu yamembana kushindwa kufika labda kama ni mgonjwa. Na kama ni mgonjwa lazma raisi angelikuwa ana taarifa asingemtafuta pale.

Kubenea kapoteza bahati ya kukutana moja kwa moja na Raisi wa nchi. Hapa ndipo mahali pekee ambapo angeliweza kusema chochotebele ya Raisi hasa kwa kuwasemea shida zao.

Na Raisi mbele ya hadhara ile kasema kama mbunge wenu angelikuwa hapa angeniomba chochote ningempa. Amewataka wananchi wa ubungo kumpelekea shida zao ili aziwasilishe Serikalini.

Kwa siasa za sasa ni kutafuta uhalali wa wananchi tu bila kujali itikadi ya chama. Sintoshangaa asiporudi bungeni 2020 kwa kuwa sijui kama ana chochote anachoweza kukifanya ubungo hata kuchimba mtaro. Anapopata fursa kama hizi na kuzipoteza ni tatizo kubwa sana.

Ubungo ni mojawapo ya majimbo yenye shida lukuki hasa shida ya maji. Dumu la maji ubungo linafika hadi 500.....

Toka kubenea amechaguliwa ameweza kutetea shanga za kiunoni za wabunge wa Chadema zisikatwe na askari wa bunge. Hauna kingine alichofanikiwa kukifanya.........kubenea amka acha itikadi na kutetea Shanga za kina mama zisikatike huko bungeni.

Hii Ni Mara ya pili baada ya Uzinduzi wa ujenzi wa flyovers Ubungo pia Hakuwepo, Hata hapa Magomen Kota Hayupo! Huyu ndo Kubenea mwenyewe
 
Unaweza kuwa na hoja ila umeiwakilisha hovyo hovyo hovyo kabisa labda watakusapoti wenzako tu.
 
Hata ningekuwa mimi nisingeenda maana Rais ana tabia ya kuita mbunge ili kumdhalilisha.
Rejea alivyomtenda yule wa CUF huko kusini kwa kumlazimisha kuchangia kinyume na bajeti ya mfuko wa jimbo!!
##Hata hivyo,Kubenea amekuwa useless kwa sasa.Habari ni Bonifasi Jacob.Kubenea atumie akili ya "hapa na pale" kutuonesha alipo Ben Saanane kama ilivyoripotiwa na gazeti lake MwanaHalisi!!
 
Ubunge wa sasa kila mtu hautaki..watu waliingia wakidhani posho za semina Nje ya nchi, vikao vya kila mara, mafunzo na safari Nje ya nchi zitaendelea..mambo yamekuwa si mambo..wabunge wanakimbia wananchi..nape mwenyewe wananchi walikuwa wanamuona kwenye TV tu..wamshukuru magufuli kamtumbua akaenda kuwaona na kumwaga pesa..hata ahadi ya kuchangia kituo cha afya aliyoitoa baada ya kulazimishwa na magufuli alivyoenda kusini ametoa hela juzi..alishapotezea.
 
Magufuli anatumia mikutano hii kwadhalilisha wabunge wa upinzani akijua hawatapata nafasi ya kumjibi,Tunakumbuka alivyo fanya Bukoba Lindi na Pwani,na Kubenea sio mjinga wa kuingizwa mkenge na mtego mbuzi
Atafute mpinzani kama yule kibaraka wa ProPesa Lipumbavu wa Mtwara afuatane nae kwenye mikutano yake.Wapo watatu CUF Lipumbav
 
kumbe
kwani ubungo pawe sehemu muhimu ya Kubenea kukutana na Rais, hapo pana ikulu ndogo ya rais? ikiwa mbunge jimbo lake lina tatizo flani, malalamiko anapeleka bungeni waziri husika anaye iwakilisha serikali au anenda kumwambia rais? mwisho uliokuwa unataka kulisema ndio hilo la Kubenea kutetea shanga, ila ulishidwa kutumia njia fupi
 
Jamani watumikieni wananchi nasio kitafuta kiki.kwani wapinzani ni mara ngapi wameomba kukutana nae na asiwape nafasi?mie naona mwache aendee kuwa mfalme jozi.kwamba ni wa gharama sana.binadamu tu mavumbi na mavumbini tutarudi. Hakuna aliyebora zaidi ya mwingine machoni pa mungu. Madaraka,Jeshi vyote vitabaki hapa kila mtu atatoa hesabu yake iliyo sahihi bila kutengemea kupata kiki za wanadamu.tunapaswa kukumbuka hilo na kuendelea kuiombea nchi yetu na nafsi zetu na tukumbuke kutenda haki.
 
Makario katika ubora wako,mlishawah kumuita boniface jacob na mkaishia kumdhalilisha,uamuzi wetu ni huo popote atakapoenda huyo faru joni sisi hatutoshiriki,hatuwezi kuwa pamoja na akina dariki moko(bashite)
 

Kwani Lazima kwenda??Kubenea alikwenda Kusaga wale Polisi waliouawa.

Kwa mila na desturi zetu tunathamini msiba na si sherehe.

Kwa kawaida msiba huanza kwanza sherehe baadaye.Wabunge wetu wanathamini to na si kiki za fent font
 
Mbunge wa Magomeni, kamshukuru Rais kea pesa alizopokea za maendeleo ya majimbo ya wabunge. Na amesema amezitumiaje kutatua matatizo mengine...huyu akipewa cheo na mkulu sitamshangaa na yule Mbunge anayemaliza muda EALA wote CUF wamemvutia.
 
Naonà wameogopa kidhalilishwa pengine maana mh. Wetu naye wakati fulani mh! Ingawa naona kuna mabadiliko kaasi kwa wik mbili hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…