Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,658
- 239,132
Mh , Mara tu ulipotangazwa mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo la Ubungo , uliahidi mambo mawili ya kuyashughulikia kwa haraka sana.
1. Uliahidi kuhakikisha UDA na mali zake zote zinarejeshwa kwa wenyewe wananchi wa Dar es salaam maana mkataba wa kuuzwa kwake una utata mkubwa.
2. Uliahidi kuhakikisha kwamba Mahakama ya jiji inafutiliwa mbali maana imewekwa kwa lengo la kukomoa masikini , mahakama hii kwa miaka yote imekuwa kero kubwa kwa Mama lishe , Machinga na Wajasiria mali wengine wadogowadogo
Kwa mfano , pamoja na askari wa jiji kudaiwa kupora mali za wafanyabiashara ili kuweka ushahidi mahakamani lakini wenyewe wanapozifuatilia baada ya muda mfupi hawazikuti !
kibaya zaidi hata Wali na maharage wa mamalishe unachukuliwa kama ushahidi lakini baada ya masaa machache yanakutwa masufuria matupu , je wali umepelekwa wapi ?
Nimeona nikukumbushe hili mkuu maana ndiyo mambo uliyoahidi kuyashughulikia kwa Haraka sana.
hiyo kesi haina nguvu yoyote kisheria kiasi cha kuzuia mbunge kutekeleza majukumu yake .Anasubiri hukumu ya kesi yake tarehe 13/04/2016, ya kumtukana Makonda.
Na kuna wanyetishaji wametonya kwamba hiyo tar 14 kuna uwezekano wa kuanza kula ugali wa Bure huko KEKO.Anasubiri hukumu ya kesi yake tarehe 13/04/2016, ya kumtukana Makonda.
asante mkuu , nimeweka uzi huu makusudi .Jiji liko chini ya UKAWA tuliza presha yote hayo yatatimizwa, uchaguzi uluoisha watu wa Dar wamefanya maamuzi ya karne ambayo siku chache zijazo hatutojutia kura zetu kuwapa UKAWA.
Hakuna mahakama itayotumika kujidhalilisha kwa kiwango hicho .Na kuna wanyetishaji wametonya kwamba hiyo tar 14 kuna uwezekano wa kuanza kula ugali wa Bure huko KEKO.
Kwa miezi 12. Unaona hiyo?
kubenea ni mbunge wa nchi nzima , anaanza na kurudisha mali za wana dsm , then wote waliodhulumiwa nchi nzima watafaidika na huduma yake .Hehehe
Mnategemea ZERO
Awafanyie miujiza
Team Masaburi bado tu hujakata tamaa ?Duh una moyo aisee bado unaiman na kubenea apo tulishakula loss wana ubungo uyo ni mbunge wa ovyoovyo
tumeweka makusudi ili wale wanaojiandaa kukimbia nchi ni bora wakawa na tiketi zao mkononi , maana hii issue msururu wake ni mrefu sana , na ninavyomfahamu kubenea atataja kila mhusika kwa majina yake yote matatu .Kukumbushana ni vizuri na atimize kweli ili ccm wasipate la kusema.