Ila Nchi yangu TZ ijitathimini upya. kwani sioni kama tuna rafiki wa kutumainia. hata Zimbabwe Rafiki yetu kipenzi, siku hizi hatuko naye tena. Mugabe alishachukia jinsi siasa zinavyoendeshwa humu nchini na kiukweli, hatuna Rafiki...Wanaogopa al- shababae..
Mkuu,Wanaogopa al- shababae..
swali zuri sana...! RespectMkuu,
Kwa hiyo viongozi/Maraisi waliohudhuria wao hawaogopi Al-Shabab ...?
Mkuu, sisi hatuendi kwa ajili ya uadui bali kuonyesha mshikamano na urafiki kama ilivyokuwa zamani enzi za Mwalimu na Mzee Mwinyi. Wasomali siyo adui zetu na hakuna ugomvi wowote kati ya Mtanzania na msomali. na Hata tunapokutana nje ya nchi, tunashirikiana vizuri tu na hata wao wakiwa tz wanajisikia amani sana. Somalia kuna biashara na ndo maana unaona Kenya yuko karibu nae kwa kila jambo.Lakini sisi watz hatutaki matatizo na hao jamaa ache wakae wenyewe huko mpaka watakapo kuwa na amani njaa inatusumbua halafu tuje tujichanganye nao tuwe na vita na Alshabaab itakuwaje.!?
mkuu, hata mimi nilikuwa nawaza hivyo. ikitokea mtanzania mmoja akahudhuria sherehe nchi jirani, itakuwa awakening call kwa hawa slave master wetu wa Bongo...Tuwe tunaenda wenyewe mambo mengine ni aibu
Uhusiano wa Kenya-Somalia ni mkubwa sana. Kenya imepeleka jeshi huko. Kenya ina wakimbizi wengi sana kutoka Somalia. Kabila la Wasomali ni mojawapo ya makabila makubwa Kenya na huu ni mwaka wa uchaguzi, lazima aonyeshe anasupport Somalia. Eastleigh, Nairobi nikama economic capital ya Somalia.J
Kenya ku-overtake kwenye siasa za kimataifa: tumeona Rais Uhuru Kenyatta akichanja mbuga kwenye medani za kisiasa za kimataifa. popote penye tukio whether in Africa na hata nje ya bara la Africa, Jamaa yupo. Siyo kwamba hajui anachokifanya, Wakenya ndo watafaidika baadae na jitihada hizi...
Logic/Lesson: wahenga walisema, riziki ya mbwa iko miguuni mwake. kuna faida kubwa sana ya kuwa na bilateral relationship kati ya Tanzania na Somalia. tunaweza kufanya biashara nao. Somalia ni jangwa na bila shaka hawana chakula cha kutosha. tunaweza peleka chakula huko na wafanya biashara wetu wakapata neema/Fursa...
Uhusiano wa Kenya-Somalia ni mkubwa sana. Kenya imepeleka jeshi huko. Kenya ina wakimbizi wengi sana kutoka Somalia. Kabila la Wasomali ni mojawapo ya makabila makubwa Kenya na huu ni mwaka wa uchaguzi, lazima aonyeshe anasupport Somalia. Eastleigh, Nairobi nikama economic capital ya Somalia.
hilo linawezekana pia mkuu...Huenda hatukupewa mwaliko mkuu