Kosa la kwanza kwa Gwajima na Manji ni kwenda polisi kabla ya wakati

Gari imepaki pale pale inasubiri boss atoke....Serikali haiendeshwi kwa kupigwa mikwala....hata kama ni serikali duni kiasi gani. Mwisho wa siku hata biashara zao zitayumba. Kama unategemea kusupply bandari, Tanesco na kwingine unatunishiana misuli na serikali ili iweje?
 
Watanzania bwaaaana! Serikali ikijiheshimu itaheshimika pia. Hv unamwandaa mhalifu af imkamate.? Ndo maana wajanja wanaona huu ni ukurupukaji. Fanya uchunguz af kamata mtu akiwa na kidhibiti af peleka mahakani fungaa!! Kinachotokea saiz watanzania tushashindwa
 
Jana ipi labda ss hatujaifikia
 
Wewe jamaa bana...... Manji anapiga biashara za kimataifa... Na infact wewe mwenyewe kwa kuccoment tu hapa tayari ushamwingizia cent kadhaa... Achana na ile kichwa Kaka...

Nenda Brazil ndio utajua busness za Manji...
 
Washauri wao hawakufanya kazi yao sawasawa,
Kulikuwa na haja gani kuwahi Polisi kabla ya muda uliopangwa?
Hilo ndio kosa LA kwanza so far nimeanza kuona kitu kinaitwa panic,
Sijui kama intelligence inaona hivyo !
Kupambana siku mbili za weekdayz ni uwanja mpana kuliko 1 day.... Badae watatoka na ndio utajua ile jamaa akili ipo kichwani
 
Kipanya Masoud juzi alichora katuni ikiwa na maneno kuwa "hivi viongozi wa siasa wote wakiwa polisi itakuwaje?" kapanya kamjibu kuwa "wananchi wote tutakuwa watuhumiwa". Huenda kuna waliomuelewa!
 
Sio Brazil tu wanakampuni kubwa sana ya kuunda mabasi ya Bodi za marcopolo wanauza hadi Ulaya ulizia basi za SCANIA marcopolo bei gani,hii familia wamejiwekeza sana uturuki,Canada,Brazil na Ulaya hapa bongo ni sababu ya asili ya babu yao
 
'Kumtuhumu' mtu ni mfanyabiashara wa madawa au moja kata ya watu wanaoweza kukupa taarifa juu ya biashara hiyo ni jambo la hatari sana kwa mtuhumiwa. Hivyo basi si vibaya akiwahi mapema ili kuondoa u hatari wa aina yoyote ile.

Mfano: Osama angeambiwa na marekani awasili USA ijumaa kwaajili ya mahojiano n.k alafu Osama akafika siku mbili kabla unadhani angekua amefanya kosa?
 
Wewe jamaa bana...... Manji anapiga biashara za kimataifa... Na infact wewe mwenyewe kwa kuccoment tu hapa tayari ushamwingizia cent kadhaa... Achana na ile kichwa Kaka...

Nenda Brazil ndio utajua busness za Manji...
Hebu acheni ujinga. Sisis wa mwalimu Nyerere tulifundishwa kuwa mtu hatakudharau simply because of vibiashasra vyake uchwara! Mnatakiwa kuwa bold vijana wa siku hizi. Njaa isikufanye mtu akudharau. Eti oohh anafanya biashara za kimataifa so what???? anatakiwa kufuata taratibu na sheria za nchi!
 
Huyo Makonda hiyo operation yake kakurupuka na haitaleta impact yoyote.Kama alikuwa na nia thabiti angeifanya kwa siri sanaaa ila kwa mwendo huu kama mtu kweli anahusika anaficha madawa yake then anaenda kuhojiwa anakanusha maana hakuna uthibitisho at the end biashara inaendelea kama kawaida
 
Tulia wewe.
Mwenye fedha ndio Mjanja wako.


Kama ulikuwa hujui wapo Wanaume 'Sio kama wewe na mimi' ukiwakorofisha na wakazila KaNchi kanapepesuka.

Sina maana sheria zisifuatwe lakini na mwenye mafwedha aheshimiwe.
Mf. Huyo bwana kaajiri watu wangapi unajua?
Akiamua kuhamisha biashara zake nje wangapi wataathirika?
Kodi itakayopotea je?
 
Sio Brazil tu wanakampuni kubwa sana ya kuunda mabasi ya Bodi za marcopolo wanauza hadi Ulaya ulizia basi za SCANIA marcopolo bei gani,hii familia wamejiwekeza sana uturuki,Canada,Brazil na Ulaya hapa bongo ni sababu ya asili ya babu yao
Fanya research yako tena mkuu marcopolo siyo kampuni ya manji labda yeye ni wakala.
marcopolo ni kampuni ya brazil hata kiwanda cha hizo body sio cha manj
 
Washauri wao hawakufanya kazi yao sawasawa,
Kulikuwa na haja gani kuwahi Polisi kabla ya muda uliopangwa?
Hilo ndio kosa LA kwanza so far nimeanza kuona kitu kinaitwa panic,
Sijui kama intelligence inaona hivyo !


Ukiwa shule ukichelewa ni adhabu na Kwenda polisi ukiwahi ni adhabu kweli?? Huku ni kukomoana wenye uwezo na wasio na uwezo AKA Kijicho.
 
Msidhani makonda kakurupuka, anachokifanya hakijawahi kufanywa na mtu before japo viongozi tunao na wengine wamekuwa wabunge na viongozi wa serikali kwa muda mrefu. Ukiangalia kwa fikra ya haraka utaona kuwa makonda kakurupuka lakin hajakurupuka kabisa na hana lengo la kuwakamata bali lengo lake la awali ni kuwaonya ili waache kabisa. Na anawaweka hadharani ili wajulikane ili kesho wakijichanganya iwe rahisi kuwakamata wakiwa na ushahidi. Kama angekuwa na nia ya kuwakamata angefuatilia kimya kimya na kuwakamata,lakin angeweza kukamata wachache sana ambao wangewa alert wengine wakawa makin au kusitisha kwanza biashara zao hizo. Mtandao wa madawa ni mkubwa sana, ndio maana kaamua kufanya hivo ili awe na coverage yao kubwa ili sasa aje kuanza kuwafuatilia taratibu kwa undani na umakini zaid hapo baadae. Tusilaumu kisa viongoz fulani au watu fulan maarufu tunaotukuza wanatajwa, vita ya madawa ni kubwa na inahitaji awam ya muda mrefu.
 
Huoni kwa kufanya hivyo atakosa ushahidi then wamfungulie kesi ya madai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…