Kosa analofanya mama mzazi pale anapoachika na kuwaacha watoto kwa baba yao.

lup

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
2,514
2,737
Za jioni wakuu..niende kwenye mada..
Katika mazingira ambayo mda mwingine hayazuiliki kwa namna yoyote ile, inabidi kuachana kwa wazazi. Na kwa sababu za aina yoyote ya maisha mda mwingine inabidi mama kuwaacha kwa baba yao hata kama unawapenda.Au labda ulibeba ujauzito bila kutarajia na wewe sio mke wake,na ikakulazimu kumpa mtoto wake ili wewe uwe na maisha huru.
Sasa unakuta mama tayari watoto wako mikononi mwa baba na labda baba ameamua kuoa tena, wewe mama unaanza kuwaambia watoto maneno ambayo kimsingi ni kama kuweka chuki kwa baba yao...mfano,baba yenu alitaka kuniua huyo,tena ana roho mbaya sana,au baba yenu hawajari na amekalia umalaya tu na huyo hawara yake. Au tena na huyo mke wake msimheshimu kabisa yaani mfanye visa vya kutosha...nyie sio wafakazi wake hapo na hata vyombo msioshe... Na maneno mengi kama hayo ili tu kuwaonyesha watoto kuwa wamchukie mzee halafu wakuone wewe ni wa maana zaidi.
Kosa lingine,ni pale mama unapowaambia watoto mambo yenu ya chumbani kabisa ambayo yalifanya mkosane,
Ni kweli kwa mtazamamo wa hapo ni kama unaweka mazingira ili wakikuwa wasikusahau kuwa ni mama yao na wakujali ikibidi zaidi ya baba yao.lakini kitu unachotegeneza ni kibaya zaidi, kwani watoto kwa mda huo watakusikiliza sana na kuanza visa kwa baba yao...kitu ambacho baba hufanya ni kupunguza mapezi kwa wanaye na kuona kuwa kumbe wanamuheshimu mama yao zaidi yake.lakini watoto wanaweza kukosa hata huduma za msingi kwa sababu yako. Na jibu ambalo wanaume hupenda kuwaambia watoto..."wanangu mnakuwa na nyie na siku mkiingia kwenye ndoa mtajuwa kwa nini niliachana na mama yenu.."
Wamama, mjiamini kwani ni ngumu sana mtoto kumsahau mama yake akisha fanikiwa...ni lazima atakutafuta tu popote ulipo na kukuheshimu.
Pogezi kwa wanaume ..sijawahi kusikia mwanaume anamponda mme wa mzazi mwenzie ambaye anaishi na watoto wake na mzazi mwenzie.zaidi atawaambia watoto MSIMDHARAU HUYO BABA YENU.huwa napenda sana hii kauli ya wanaume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…