Kosa afanye jambazi kupigwa apigwe raia, sio sawa

Nadhani wananchi wa pale wapate kwanza kichapo maana wanachukuaje mkaa katikati ya damu za watu huku wauaji wakiwa hapo na wao wako comfortable
 
Tambua wanaotenda uhalifu ni miongoni mwa raia hao hao.
Mhalifu wa kosa la jinai ajionyeshe?

Haiingii akilini ,lazima wafanye mambo kwa siri kubwa ,

Hao wahalifu ni anoynomous ,wana plan kiakili ,

Ulaya ulaya tu ,..

Toka lini uhalifu ukitokea USA FBI wanasambaza dozi kwa RAIA ,lakini ndani ya 24hrs wanawapata wahalifu

Bara la Giza hili hakika ,
Nguvu bila akili ni tatizo
Mzigo kwa kichwa

Police uchwara
 
Wao wameuawa na sokwe? Hiyo ni njia mojawapo ya interrogation.tuache mihemuko raia wema wanajua ubaya wa uhalifu.
We umeona video watu wanavyopigwa road km vile anaua panya.? Sasa kuchukua pikipiki ya mtu na kutafuta majambazi wapi n wapi
 
Hiki ndicho kilichonifanya nianze uzi bila salaam kutokana na vitendo visivyo vya kizalendo vya askari polisi kupiga na kuumiza raia ambao sisi tunasema kuwa hawana hatia.

Baada ya kutokea shambulizi la kijambazi lililoua askari kadha mkoani pwani sasa imekuwa ni chuki na kulipiza kisasi kwa jeshi la polisi dhidi ya raia yeyote yule atakaeonekana anakatiza katiza barabarani kwa hari yeyote ile, ikiwemo kupigwa virungu na mashuti na ngumi mfano wa mtu anayecheza boxer, hawaishii hapo tu! bali hadi kupora mali za watu katika vioksi.

Kibaya zaidi ni pale mtaji uliozuka kwa wana usalama barabarani kuzidisha kasi ya kukamata magari na kupora pikipiki za watu na kuzifungia.

Sasa hii si njia nzuri ya kuzuia matukio kama haya kuendelea sababu yanaongeza chuki baina ya serikali na raia kwa kupitia polisi.

Angalizo

Njia ya pwani kwa sasa si salama tena kuanzia Mkuranga hadi kibiti hivyo mnaetembea ambao ni wafanyakazi wa ummah basi mnatakiwa muwe na set of ID.
Aiseeee
 
Nilitegemea wawafanye raia wawe Marafiki zao ili wawezw kupata info za watu wabaya wanaoua Wenzao,then the vice versa. Duh!!!!mbona kazi ipo Hapa jamani....!!
Au wangeitisha kura za siri waamrishwe wote waka pige kura halafu tuone kama wasingewapata
 
ndomana wakiuwawa kwetu sherehe,wajifunze basi hata kwenye movie hawa jamaa jeshi la polisi bado lipo katika mfumo wakikoloni wanadhani uonevu,mabavu na kuogopwa ndio ukakamavu
 
Polisi, mnazingua, mnaharibu mahusiano na RAIA, Je watawapaje taarifa za uhalifu?
Nilimsikia IGP anasema watatafuta taarifa kwa wananchi lakini wananchi wasipotoa taarifa watatafuta namna ya kulazimisha kuzipata hizo taarifa,, nafikri hili ndo linalofanyika sasa hivi!! Wakumbuke hii inaongeza chuki kati ya polisi na raia wa kawaida!!
 
Huku Pwani kuanzia Mkuranga mpaka Kibiti imekuwa Syria.Yaani hatuna uhuru wa kutembea,pikipiki mwisho saa 11 jioni baada ya hapo kitakachokukuta utatamani usingejifunza kuendesha pikipiki.Zinatobolewa tenki za mafuta,zinavunjwa taa na kipigo juu.
 
Polisi ni raia pia,tatizo midomo yetu!!! Kwani hao polisi ni kaka/dada/shemeji/baba zetu.Hatupaswi kushangilia wakifa hakuna makaburi ya polisi. Lakini tunavyojitenga nao!like hawana mwenyewe.
 
Nilimsikia IGP anasema watatafuta taarifa kwa wananchi lakini wananchi wasipotoa taarifa watatafuta namna ya kulazimisha kuzipata hizo taarifa,, nafikri hili ndo linalofanyika sasa hivi!! Wakumbuke hii inaongeza chuki kati ya polisi na raia wa kawaida!!
Ni heri ikawa hivyo.Uhalifu unatendwa na raia na wanaodhurika sana ni raia.Kama unaona uendelee kuhifadhi taarifa za wahalifu utakuwa unajiandalia moto ww mwenyewe na raia wenzako.Nalo hilo kuna uhitaji wa polisi kukubembeleleza umpatie taarifa wakati nyoka unamfuga ili akudhuru wewe mwenyewe?Basi ushenzi huo wa kuficha wahalifu uishie huko kwenu wapenda wahalifu na uhalifu.Mnapofuga uhalifu kiasi cha kuleta madhara kwa wanaolinda usalama wenu kuna haja gani ya kuwabembeleza muwe na ushirika nao?Ni mhalifu yupi anayeweza ua binadamu kisha ukachunguza akakubali kwenda kuonyesha silaha.Mm ni raia mwenye ndg zangu askari nina uchungu sana na raia wenzangu tunaoshabikia vitendo hivi vya kipuuzi.Walazimishwe hao kuwataja wauaji na si vinginevyo.
Mhalifu wa kosa la jinai ajionyeshe?

Haiingii akilini ,lazima wafanye mambo kwa siri kubwa ,

Hao wahalifu ni anoynomous ,wana plan kiakili ,

Ulaya ulaya tu ,..

Toka lini uhalifu ukitokea USA FBI wanasambaza dozi kwa RAIA ,lakini ndani ya 24hrs wanawapata wahalifu

Bara la Giza hili hakika ,
Nguvu bila akili ni tatizo
Mzigo kwa kichwa

Police uchwara
 
Wanafanya makosa sana wakati ilitakiwa wakae chini watafiti kwa kina tatizo ni nini na wanawezaje kuzuia na si kufanya hivyo wanavyofanya..
 
Hiki ndicho kilichonifanya nianze uzi bila salaam kutokana na vitendo visivyo vya kizalendo vya askari polisi kupiga na kuumiza raia ambao sisi tunasema kuwa hawana hatia.

Baada ya kutokea shambulizi la kijambazi lililoua askari kadha mkoani pwani sasa imekuwa ni chuki na kulipiza kisasi kwa jeshi la polisi dhidi ya raia yeyote yule atakaeonekana anakatiza katiza barabarani kwa hari yeyote ile, ikiwemo kupigwa virungu na mashuti na ngumi mfano wa mtu anayecheza boxer, hawaishii hapo tu! bali hadi kupora mali za watu katika vioksi.

Kibaya zaidi ni pale mtaji uliozuka kwa wana usalama barabarani kuzidisha kasi ya kukamata magari na kupora pikipiki za watu na kuzifungia.

Sasa hii si njia nzuri ya kuzuia matukio kama haya kuendelea sababu yanaongeza chuki baina ya serikali na raia kwa kupitia polisi.

Angalizo

Njia ya pwani kwa sasa si salama tena kuanzia Mkuranga hadi kibiti hivyo mnaetembea ambao ni wafanyakazi wa ummah basi mnatakiwa muwe na set of ID.
Jambazi ni yupi na raia ni yupi?
Au wana sale maalum
 
Kama polisi wanapiga RAIA unategemea watawapata majambazi wengine?. RAIA ndiyo wanawapa taarifa maana wanaishi na hao majambazim polisi mujirekebishe
 
Ni heri ikawa hivyo.Uhalifu unatendwa na raia na wanaodhurika sana ni raia.Kama unaona uendelee kuhifadhi taarifa za wahalifu utakuwa unajiandalia moto ww mwenyewe na raia wenzako.Nalo hilo kuna uhitaji wa polisi kukubembeleleza umpatie taarifa wakati nyoka unamfuga ili akudhuru wewe mwenyewe?Basi ushenzi huo wa kuficha wahalifu uishie huko kwenu wapenda wahalifu na uhalifu.Mnapofuga uhalifu kiasi cha kuleta madhara kwa wanaolinda usalama wenu kuna haja gani ya kuwabembeleza muwe na ushirika nao?Ni mhalifu yupi anayeweza ua binadamu kisha ukachunguza akakubali kwenda kuonyesha silaha.Mm ni raia mwenye ndg zangu askari nina uchungu sana na raia wenzangu tunaoshabikia vitendo hivi vya kipuuzi.Walazimishwe hao kuwataja wauaji na si vinginevyo.
Utakuwa mburura la kutupa,, yaani unaona ni sahihi polisi kupiga kila raia wanayekutana naye ili wapate taarifa? Kama taarifa huko kwenu mnatafutaga hivyo usitegemee kama mtafanikiwa kwa kupiga raia. Jeshi la polisi linatakiwa likae vizuri na raia, pale tutakapokuwa na civilians friendly police ndo itakuwa rahisi kupewa taarifa. Tumieni weredi siyo makalio katika kufikiri!
 
Hiki ndicho kilichonifanya nianze uzi bila salaam kutokana na vitendo visivyo vya kizalendo vya askari polisi kupiga na kuumiza raia ambao sisi tunasema kuwa hawana hatia.

Baada ya kutokea shambulizi la kijambazi lililoua askari kadha mkoani pwani sasa imekuwa ni chuki na kulipiza kisasi kwa jeshi la polisi dhidi ya raia yeyote yule atakaeonekana anakatiza katiza barabarani kwa hari yeyote ile, ikiwemo kupigwa virungu na mashuti na ngumi mfano wa mtu anayecheza boxer, hawaishii hapo tu! bali hadi kupora mali za watu katika vioksi.

Kibaya zaidi ni pale mtaji uliozuka kwa wana usalama barabarani kuzidisha kasi ya kukamata magari na kupora pikipiki za watu na kuzifungia.

Sasa hii si njia nzuri ya kuzuia matukio kama haya kuendelea sababu yanaongeza chuki baina ya serikali na raia kwa kupitia polisi.

Angalizo

Njia ya pwani kwa sasa si salama tena kuanzia Mkuranga hadi kibiti hivyo mnaetembea ambao ni wafanyakazi wa ummah basi mnatakiwa muwe na set of ID.
Watu walipotoa kauli za hatari bila kushirikisha akili tulitahadharisha kwamba busara itumike lakini kuna watu walitawaliwa na mihemko zaidi.
Watu wote ni sawa na dhambi ya kujeruhi na kuuwa polisi ni sawa na dhambi ya kujeruhi na kuuwa raia asiye na hatia.
Watafutwe wahalifu na waliotenda kosa bila kuwatesa watu wasio na hatia.
 
Utakuwa mburura la kutupa,, yaani unaona ni sahihi polisi kupiga kila raia wanayekutana naye ili wapate taarifa? Kama taarifa huko kwenu mnatafutaga hivyo usitegemee kama mtafanikiwa kwa kupiga raia. Jeshi la polisi linatakiwa likae vizuri na raia, pale tutakapokuwa na civilians friendly police ndo itakuwa rahisi kupewa taarifa. Tumieni weredi siyo makalio katika kufikiri!
Mbona una hasira sana.Unafikiri wao ni vichaa kupiga kila wanayekutana naye.Mkuu wana kaulimbiu yao ukiiheshimu mambo kwako poa.wao wanauawa na raia hao hao au unataka watuache tumalizane wenyewe kwa wenyewe.Nina hakika ningetokea usoni kwako ungening'oa meno.
 
Back
Top Bottom