Kitwanga kama ni jipu kwa nini asitumbuliwe?

sonofobia

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
897
3,427
Mimi ni mmoja wa waungaji mkono wakubwa wa serikali ya Magufuli. Nafurahi utendaji kazi wao na kasi nzuri wanayoenda nayo. Lakini huyu Waziri Kitwanga ni mmoja wa mawaziri ambao sijawahi kufurahishwa nae.

Sijaona utendaji wa kuridhisha kutoka kwake tangu awe Waziri. Nikiangalia idara ya polisi ambayo yeye ndio mwenye dhamana sioni chochote kipya ambacho tunaweza kusema sasa tuna Waziri wa hapa kazi tu, ujambazi upo pale pale na majambazi wanaendelea kupeta ilihali wanajulikna, madawa ya kulevya tunaona watu wanaendelea kuuza unga kama kawaida na wanajulikna na kila mtu ila polisi ni kama awawaoni.... Matrafiki wanaendelea na mradi wao wa kukusanya hela barabarani utadhani hakuna wa kuwakemea.... Waziri yupo wapi?

Haya idara ya uhamiaji ndio utadhani imekufa wahamiaji haramu wapo kila kona na kila mtu anawajua ila tuliona ile sinema ya wiki moja ya kushika wachina na watu wawili watatu then ikawa kimya... Sasa hivi ukitoa taarifa jeshi la uhamiaji ni kama umewapa dili ya pesa wanaenda wanachukua rushwa na wageni wanaendelea kupeta kila mtu ni shahidi umu...

Mimi binafsi nilishawahi kutoa taarifa kwa boss wa uhamiaji Ilala mr John msumule nikaishia kuwapa dili wakatengeneza pesa ndefu.. Tatizo lipo ila Waziri haonyeshi kukerwa ata chembe..

Okay inawezekana anafanya kazi kimya kimya bila kutumia media ila mbona wengine wanafanya kazi kimya kimya na tunaona kazi zao! Jamani kazi haijifichi kina Mbarawa wanafanya kazi bila media ila tunawaona...

Kuna vitu mtu asipofanya kunaweza kuwa na excuse labda ya bajeti ila ata utendaji wa kila siku nao unashindwa kusimamia!? Upo wapi hatukuoni field au upo ofisini bado unadhani uwaziri ni uboss....

Tukiacha hayo hizi tuhuma za kuhusishwa na kampuni iliyofanya ufisadi kwenye wizara unayoongoza inatosha kabisa kujiweka pembeni maana kwa sasa haufanani na wizara na serikali ya Magufuli.

Kitwanga ni jipu Mh rais mshughulikie najua bado serikali inajiridhisha kuona ukweli wote kuhusu scandal yake ila ata bila ya hiyo scandal jamaa tayari ni jipu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…