Changamoto kubwa amabayo CHADEMA wanayokumbana nayo sasa ni kukosa Agenda. Kukosa agenda kuimeifanya CHADEMA kupoteza imani kubwa kwa wanachama wake. Kwa bahati mbaya kwa muda mrefu Chadema kimekuwa na Agenda moja tu.
Kihistoria Chadema ndiyo mwasisi wa Agenda ya ufisadi. Chadema ilikuwa imara sana kwa kutumia Agenda hii huku wakijivunia vichwa makini kama vile Dr. Slaa na Zitto Kabnwe. Kuondoka kwa watu makini kama vile Zitto na Dr. Slaa kunachangia kwa kiasi kikubwa kuipoteza Chadema.
Kimkakati Chadema ilifanya kosa lingine kubwa kuwapokea watu waliokuwa wanatuhumiwa na kutajwa tajwa sana na wao wenyewe Chadema kama mafisadi wakubwa na kuwafanya viongozi wao.
Ujio wa Rais John Pombe Magufuri umeichangia kwa kiasi kikubwa kuimaliza Chadema. Rais ameonekana siyo tu kuilewa agenda ya ufisadi bali kukerwa kutoka moyoni na ufisadi. Rais Magufuri amejipambanua wazi kabisa kuwa yuko tayari hata kuutoa mwili wake sadaka kutetea nchi yake na amelionyesha hilo kwa vitendo. Rais ameonyesha kuwa na hofu ya Mungu na amebeba matumaini mengi kwa watanzania.
Mwenendo huo wa Rais umemfanya akubalike sana ndani na nje ya mipaka ya nchi. Rais sasa kwa asilimia kubwa anakubalika na watu wa vyama vyote, makabila yote na dini zote. Amnaonekana kuwa tumaini jipya kwa wanyonge.
Kwa msingi huo Chadema wanatakiwa wajipange upya. Pia wanapaswa watambue kwamba kwa sasa wananchi hawawaelewi wanavyoendelea kumpinga Rais anayepambana na ufisadi kivitendo tena kushinda wao walivyofanya kipindi cha nyuma. Chadema wanapaswa wamuunge mkono Rais katika agenda hii ya kupambana na ufisadi. Kama chama cha upinzani kinapaswa kitafute mambo mengine ya kuikosoa serikali kama vile kuwepo kwa uhuru wa habari na mapungufu mengine yanayoonekana.
Nawasilisha