Kaka
JF-Expert Member
- Nov 22, 2006
- 742
- 371
Hapo ni Examination in chief na cross examination. Hiyo huwa ni hatua muhimu sana kwenye kesi yoyote.
Mkuu,
Ukimpata wakili haswa hata "re-examination" inaweza kuokoa jahazi.
Kaka ...
Hapo ni Examination in chief na cross examination. Hiyo huwa ni hatua muhimu sana kwenye kesi yoyote.
Haja zote zinaweza kutoka kwa wakati mmoja, hatari sana huyu bwana.Lissu mjanja sana, yaani kampanikisha huyo shahidi kiasi kwamba naamini huyo shahidi kijasho kilikuwa kinamtoka!
Hata kujibu alikuwa hajui anachojibu na ni jibu la swali gani..
Haki ya nani usiombe huyu jamaa ukutane nae kwenye hilo eneo atakumaliza...
Na kwa taarifa yako kazi ya serikali hii ni kupambana na raia sio kuwaletea maendeleo km unavofikiriNamshauri mh rais aachane n Lissu watu kama akina lisu wana akili sana na wanapatikana dunia nzima, watu kama hawa wakinihusisha na uhalifu huwa ni hatari sana kwani wana upeo mkubwa wa mambo, kwa lissu amejikita kwenye mammbo ya maana na yenye tija ya kutetea haki.
Serikali ispoangalia itaishia kupambana na watu ishindwe kutekeleza mipango yake
Daah Lissu noma....Kesi namba 208 ya 2016 imekwama kuendelea leo katika Mahakama ya Kisutu baada ya Wakili kuhoji shahidi asihojiwe mambo ya Zanzibar.
Shahidi wa kwanza upande wa serikali alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Salumu Hamduni.
Wakili wa serikali Paul Kadushi aliiomba mahakama izuie lakini Lissu akijitetea alisema suala hilo lazima lijadiliwe sababu serikali yenyewe ndio imeliweka kwenye hati ya mashtaka.
MAHOJIANO NA SHIHIDI WA KWANZA WA SERIKALI, KESI YA GAZETI LA MAWIO.
Wakili wa Serikali: Paul Kadushi
Shahidi: Salum Rashid Hamduni
WAKILI: Iambie mahakama ulibaini nini kwenye kazi yako, Januari 14, 2016 asb
SHAHIDI: Nilibaini Mikusanyiko isiyo rasmi sehemu za kuuzia magazeti, wananchi wakijadili habari iliyochapishwa na Mawio.
WAKILI: Baada ya Hapo ulichukua hatua gani
SHAHIDI: Nilimjulisha Mkuu wa Upelelezi, Kanda Maalumu ya Dar (ZCO), na makao makuu ya polisi, ambapo nilitaafiriwa kuwa hali ilikuwa vile vile upande wa Zanzibar
WAKILI; Baada ya hapo ulichukua hatua gani?
SHAHIDI: Niliamua kwenda kununua gazeti la Mawio, nisome kuona kama kuna taarifa zozote zilizochapishwa, nikagundua kuna taarifa za uchochezi na kutia hofu, nikaamua kufungua jalada la uchunguzi.
WAKILI: Kwanini ulifikia Uamuzi huo?
SHAHIDI: Nilifikia uamuzi huo baada ya kusoma headline ya ”machafuko yaja Zanznibar”, nilijiridhisha kuwa baadhi ya maneno katika habari hyo yanaweza kuleta hofu na chuki dhidi ya serikali ya Zanzibar
WAKILI: Taarifa kuhusu tukio hilo uliletewa na nani?
SHAHIDI: Nililetewa na wakuu wa upepelezi wa mikoa ya Ilala, Temeke na Kinondoni, yaani SSP Mchomvu-Temeke, SP Ndalama wa Kinondoni na Jumanne Mliro wa Ilala. Walisema kuna mikusanyiko maeneo yao kwenye vijiwe vya magazeti kulingana na habari iliyochapwa na Mawio.
*** WAKILI WA SERIKALI ALIFUNGA MASWALI*****
Kwa upande wa Wakili Peter Kibatala alimuuliza huyo shahidi anafahamu hilo gazeti la mawio linasambazwa Zanzibar na Tanzania Bara kwa kiwango gani katika shughuli zake za kiuchunguzi?
Shahidi huyo wa upande wa mashtaka alimueleza kuwa hana takwimu sahihi.
KIBATALA; Gazeti la Mawio unajua linachapishwa na nani
Shahidi; sifahamu isipokuwa nakumbuka muandishi alikuwa ni Jabir Idrissa
KIBATALA; Ni sehemu gani ambayo ulisoma na kuona kuna taarifa za uchochezi
Shahidi; Ni heading yenyewe ndio ilikuwa inazungumzia uchochezi kwamba Machafuko yaja Zanzibar
KIBATALA; Je habari hiyo ina uhusiano gani na washtakiwa wa nne
Shahidi; Habari hiyo kwa sehemu kubwa inaonyesha mwandishi alivyomuhoji kwa kina Lissu
KIBATALA: unafahamu aliyekuwa DCI , Diwani Athumani alitenguliwa na mheshimiwa rais baada ya kumuhusisha na Meno ya Tembo.
Shahidi sifahamu
LISSU AJITETEA MWENYEWE
Kisha mshitakiwa namba 4, Tundu Lissu alijitetea Mwenyewe na mahojiano yalikuwa hivi;
LISSU: Shahidi ieleze mahakama elimu yako
SHAHIDI: Nilisoma Uchama Sekondari, nikasoma A Level Kigurunyembe, na IDM Mzumbe
LISSU: Ulijiunga lini na Jeshi la Polisi
SHAHIDI tangu mwaka 1999.
LISSU ulisema wewe ndio ulifungua jalada la uchunguzi, baada ya wakuu wa upepelezi wa mikoa tajwa kukuletea taarifa, je uliwaandika maelezo yao kama mashahidi wa kesi hii?
SHAHIDI; Hapana
LISSU; Mikusanyiko isiyo rasmi, ni halali au sio halali
SHAHIDI: Ni halali
LISSU: Mihemuko na Hofu inazuiliwa kisheria?
SHAHIDI: Hapana
LISSU: Hofu kama ya Mungu, au ya shetani au ya Dikteta, inazuiliwa kisheria?
SHAHIDI: Ndio inazuiliwa,
LISSU: Sheria gani?
SHAHIDI: SIJUI.
LISSU; Mweleze hakimu, sisi tulikaa wapi kula njama ya kuchapisha gazeti hili
SHAHIDI: sijui
LISSU; Mweleze hakimu tuliwasiliana kwa njia gani ili kukaa pamoja kula njama kama tunavyoshtakiwa
SHAHIDI: Sijui
LISSU, unafahamu ni saa ngapi tulikula njama?
SHAHIDI: Sijui
LISSU; kabla ya kushtakiwa hapa je mimi nilifahamiana na washtakiwa hawa wengine?
SHAHIDI; Sijui
LISSU; Kama hujui muda gani, mahali gani, hujui kama tulifahamiana ulijuaje kama tulikula njama?
SHAHIDI; sijui
LISSU; kwa ufahamu wako, mimi ni mwandishi , au mhariri wa Mawio?
SHAHIDI; Hapana, wewe sio Mwandishi au Mhariri
LISSU; Je unafahamu labda najishughulisha na kazi zozote za uchapishaji wa magazeti?
SHAHIDI; SIJUI.
LISSU:Mweleze hakimu, mimi nawezaje kushtakiwa wakati mimi sio mwandishi, sio mhariri, wala sio mchapishaji au mmiliki wa gazeti?
SHAHIDI; siwezi
LISSU; Mamlaka halali ya serikali ya Mapinduzi ya wananchi wa Zanznibar inachaguliwa kwenye uchaguzi kwa mujibu wa katiba na sharia za uchaguzi wa Zanzibar kweli au si kweli?
SHAHIDI; kweli
LISSU;25 Oktoba 2015 kulikuwa na uchaguzi halali wa Zanzibar kweli au si kweli
SHAHIDI ; Kweli
LISSU, Kwa ufahamu wako uchaguzi huo wa Oktoba 25, 2015 ulifanyika kisheria na ulifutwa kinyume cha sharia na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salum Jecha ni kweli au si kweli?
SHAHIDI; Kweli
LISSU; Mweleze hakimu kama unaijua katiba ya Zanzibar na sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar
PAUL KADUSHI WAKILI WA SERIKALI AWEKA PINGAMIZI
Kadushi: Napinga swali , tafsiri ya Katiba na serikali halali ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria, wanataka shahidi atafsiri katiba ya Zanzibar huyu sio mtaalamu wa masuala ya katiba, shahidi sio mwanasheria wala mahakama inayotafsiri sheria.
LISSU; Pingamizi halina mashiko, suala la kwamba serikali ya mapinduzi ya zanzibar ni halali au si halali , na masuala ya Jecha kufuata uchaguzi wameyaleta wenyewe mahakamani ndio maana inabidi yajadiliwe, shitaka lenyewe linasema tulikula njama ya kuleta chuki dhidi ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kifungu cga 157, kinaweka wazi kuwa shahidi anaweza kuulizwa shwali lolote na kwa kuwa wameyaleta wenyewe, wakubali suala la Zanzibar lijadiliwe, naomba mahakama iruhusu.
KIBATALA ANASIMAMA KUONGEZA;
Kwanini wakili wa serikali anamkinga shahidi asijibu Maswali? Imekuja hoja ya wakili huyu kuwa suala la Zanzibar ni suala la Kikatiba, na uchaguzi wake, ikumbukwe kuwa tulipoweka PO, (pingamizi la awali) kuhusu mahakama ya Kisutu kuwa na uwezo wa kusikiliza kesi zinazohusu serikali ya mapinduzi ya Zanzibar iliaamuliwa kuwa inaweza, ndio maana hoja za kesi zimekuja zikitaja masuala ya Zanziba
Hakimu Thomas Simba ameahirisha kesi hiyo hadi kesho saa 3 na nusu.
Kwa nini unarejea bandiko lote namna hii? Bandiko la kwanza hujali hariri na bado umelirudia hivyohivyo. Badilikeni banaHuyo polisi hana kazi kama kila kitu ni sijui na hapana
Nani anajali?hapa cha muhimu ni Lissu kuwashikaKwa nini unarejea bandiko lote namna hii? Bandiko la kwanza hujali hariri na bado umelirudia hivyohivyo. Badilikeni bana
Watoke wapi?Wale wa lumumba siwaoni humu Leo!!!
Sio swala na Lumumba mkuu. Lissu anakufanya ufikiri vizuri unapokutana nae eneo lake la taaluma. Inabidi iwe hivyo ili vizazi vyetu vipate kurithi kilicho bora. Ngoja nirudie mahojiano hayoWale wa lumumba siwaoni humu Leo!!!
Weka mchango tu kama hubadilishi chochote kwenye bandiko la msingi ili kulinda hadhi ya JF.Nani anajali?hapa cha muhimu ni Lissu kuwashika
Hapo kwenye swali linalohusu uchaguzi halali uliofutwa kinyume cha sheria na mtu fulani hapo.......!!!!Huyo polisi hana kazi kama kila kitu ni sijui na hapana
Hakujua anahojiwa na mtu wa aina ganiSasa imeahirishwa mpaka kesho na shahidi anakuja kuendelea kuhojiwa mbona ni balaa kwa polisi wa watu! Sijui yuko hali gani alipo!
Nimecheka sana, swali kuhusu hofu ya Mungu, shetani na dikteta. Jamaa anatwanga humo humo bila hofu
Hata mimi ushauri wangu waaachane na haya mambo ya wapinzani kukimbizana nao mahakamani,miaka mitano itaisha hawajafanya kitu.hawa wapinzani wapo na hata ukiwafunga hawa wataibuka wengine so wao wadili na kutekeleza walichowaahidi wananchiKwakweli lisu wamuache tu wasipoangalia miaka mitano wataimaliza wanahangaika na lisu bila kutekeleza ahadi zao