Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,590
- 1,191
KISHINDO CHA KATIBU MKUU UVCCM KENANI KIHONGOSI KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 45 YA KUZALIWA CCM KWA UVCCM KITAIFA WILAYA YA TARIME MKOA WA MARA
Tarehe 3 Februari 2022 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndug: Kenani Labani Kihongosi ameambatana na Mwenyekiti wa Chipukizi UVCCM Taifa Ndug Yusuph Haji Kashmir na Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Ndug Victoria Charles Mwanziva na Wajumbe wa Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wameshiriki katika maadhimisho ya Miaka 45 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi kwa UVCCM ambayo kitaifa yamefanyika Mkoani Mara Wilaya ya Tarime.
Aidha katika maadhimisho hayo Katibu Mkuu wa UVCCM Ndug Kenani Kihongosi kwa kushirikiana na wajumbe wa Baraza kuu wametembelea Miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali ya Awamu ya 6 inayoongozwa na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja kutembelea na kupandisha bendera Mashina mawili katika kata ya Sababa wilayani hapa.
Miradi ya maendeleo iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na Ujenzi wa Madarasa Shule ya Sekobdari Turwa, Mradi wa Ufugaji Samaki na Nyuki was kikundi cha Umoja wa Vijana wilaya ya Tarime, Ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Bemela, Ujenzi wa Zahanati Kijiji cha Kiterere na mradi wa Shamba la Vijana Jimbo la Tarime Vijijini. Kwenye ukaguzi wa miradi ya maendeleo Katibu Mkuu pia aliambatana na Wabunge wa wilaya ya Tarime, Mkuu wa Wilaya na Mkurugezi wa halmashauri ya wilaya hii.
Katika ukaguzi wa madarasa yanayotekelezwa kupitia Mpango wa maendeleo na mapambano ya Uviko 19 kwa Ustawi wa Taifa letu katika shule ya sekondari Turwa,Katibu Mkuu amempongeza na kumshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa Kazi nzuri na kubwa aliyoifanya kuhakikisha kila mtoto wa Mtanzania anapata nafasi ya kupata elimu bila bughuza yoyote.
Kwa upande mwingine katibu Mkuu UVCCM Ngug Kenani Kihongosi amesisitiza umumuhi wa Sensa kwa kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kushirikia katika zoezi hili. "Mwaka huu ni mwaka wa SENSA nawaombeni sana mjitokeze kwa wingi kuhesabiwa, hii itasaidia serikali katika utekelezaji wa miradi muhimu na kuleta huduma kwa wanachi"
Lakini pia Katibu Mkuu amewakumbusha Vijana kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi ndani wa Chama cha Mapinduzi na Jumiya zake hivyo kuwasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama." Mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi ndani ya Chama hivyo wanachama wate wenye sifa nendeni mkachukue fomu kugombea, lakini pia tunaomba sana watendaji wa Chama wasihusike na mchakato waa Ucjaguzi ndani ya chama kwa Kumbeba mgombea flani".
Katibu mkuu hakusita kukumbusha majukumu ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) " Majukumu yetu UVCCM ni kulinda heshima ya CCM na Mwenyekiti wetu pamoja na Viongozi wengine, hivyo hatutamvumilia mtu yeyote atakaye kmtweza na kumvunjia heshima mwenyekiti wetu
Mwisho katibu Mkuu wa umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) amewapongeza Wenyeviti wa Mashina wa CCM kwa kazi nzuri waliyoifanya katika ziara wilayani hapa lakini pia kuwashukuru wananchi waliojitokeza kwa wingi katika ziara hio.
Imetolewa na Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa
UVCCM TAIFA ©️2022