Kisa na mkasa

1974hrs

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
741
536
Habarini wanaJF,

Hivi unapokea simu unaitwa polisi unaelezwa mme/mke amekamatwa na yupo lokapu unawahi kujua msaada gani ili atoke unapofika kuuliza kosa lake unaambiwa kafumani na mme/mke wa mtu na wote wapo ndani
Hapo ni hatua gani muafaka na ya haraka unaweza kuchukua?
 
Kama una uvumilivu wa kipekee utamtoa kwanza kwa dhamana halafu kesi yenu nyinyi wawili mtaimalizia nyumbani na kama huna uvumilivu itabidi mhusika atafute tu mtu mwingine wa karibu amuwekee dhamana.

Mbona kuna jamaa yangu alipatwa na mkasa wa aina hiyo.Kiufupi nyumbani alidanganya kapata kesi ya ajali barabarani halafu akaniita mtu wake wa karibu tukayamaliza polisi kiutu uzima kwa kulipa faini. Ila usiombee yakutokee!
 
unaanza kwanza kushughulikia like ulilopewa taarif yake kwanza, huwezi kushughulikia mambo mawili kwa wakati mmoja.
 
Unamtoa kwanza ili uweze kusikia kutoka kwake....Maelezo ya upanda mmoja si timilivu mara mingi...
 
hii imetokea hapa polisi post mbande aisee sasa huyu jamaa mwenye mke na yule mwenye mume wamekubaliana kuwaacha ndani na wao wakajifidie kwanza mpaka watakapoona wameridhika watakuja kuona la kuamua tehtehteh
 
Rudi nyumbani pika pilau kula...... utarudi mahabusu baada ya siku 3
 
Nitamtoa mwanamke wangu... maisha yataendele... bahati mbaya tu..
 
hii imetokea hapa polisi post mbande aisee sasa huyu jamaa mwenye mke na yule mwenye mume wamekubaliana kuwaacha ndani na wao wakajifidie kwanza mpaka watakapoona wameridhika watakuja kuona la kuamua tehtehteh
Huo uamuzi mtamu sana aiseee
 
Ndugu zangu mnaosema sijui namtoa kwanza mengine baadae msisahau jins mke anavyoumaa!kwanza kabla ya hapo atakuwa ameshakuletea dharau na vurugu ndani ya nyumba sometime siku ya tukio kabla hujaondoka home alikuletea mambo ya kijinga kisha mchana upigiwe simu kafumaniwa guest house na bwana kakamatwa yuko police uende kiroho safi ukamtoe?hahahaha mnatania wakuu me wala sihangaiki nae watamtoa ndugu zake kimbembe atarudije home..in short atakuwa amejifukuzisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…