Smart AJ
JF-Expert Member
- Mar 21, 2022
- 5,563
- 5,875
Nawasalimi kwa jina la Muumba..,hiki ni kisa cha Kweli kimetokea miezi kadhaa hapa kwetu mtaani..
Jamaa mmoja tumpe jina k,alitoka kijijini na mke wake na kuamua kuja mjini kwa ajili ya kufanya maisha na mkewe kipenzi. Walipendana sana na alimtolea kabisa mahari yeye anadai ya tsh 800k. Basi walikuja town kwa baraka zote kutoka kwa wazazi wa pande zote mbili. Si kwamba alikuwa na kazi au kipato kizuri,ila ndo hivyo maisha ya kijijini kama mnavyojua.
Baada ya kufika town,alijikita kwenye vibarua vya hapa na pale kwa ajili ya kujikimu yeye na familia yake,alijihusisha na kazi ta ulinzi kwenye moja ya yard za mh joseph mungai(waziri wa elimu mstaafu awamu ya nne nadhani).
Aliamua kumtaftia kazi ya kupika kwenye yard hiyo mke wake ili mradi asiwe anakaa bure na pia kwa nia ya kuongeza kipato chao kama familia. Anasema walipendana sana siku hizo,ila mambo yalikuja kubadilika baada ya mkewe kuanza kufanya kazi ya kupika katika yard hiyo.
Kwa kuwa jamaa alikuwa analinda usiku kumbe mchama mmoja dada alikutana na jamaa mmoja mahali hapo na wakatongozana. Pengine ni udhaifu wa wanawake ila ndo ilkuwa hivyo,basi usiku jamaa akiwa anaenda lindoni dada alikuwa anamleta jamaa kwenye chumba walichopanga na kuenjoy.
Walibahatika kupata watoto wawili,ila kama siku anapanga kumualika mchepuko binti alikuwa anawapeleka watoto wake kwa rafikize ili mradi apate wasaha mwanana wa kufaidi penzi la wizi.
Inasemekana alimdanganya jamaa kuwa hajawahi kuolewa na wala hana mtoto,so jamaa alikuwa anaenda kwa amani zote .
Mapenzi ya wizi yalizaa matunda na hatimaye dada alipata mimba inayosemekana kuwa ni ya jamaa mchepuko ila akamdanganya mumewe kuwa ni yake so wakaendelea kulea tu bila wasiwasi mpaka mtoto alivyofika umribwa miezi kadhaa ,ndipo mambo yalipoanza kuwa bayana
Mama mwenye nyumba yao,ni miongoni mwa watu walioshuhudia usaliti uliokuwa unaendelea ndani humo.
Akaamua kumweleza mwenyekiti wa mtaa huo,ambaye alimwekea mtego jamaa akiwa anatoka chumbani kwa mwanaume mwenzie asubuhi moja na kuamua kumuuliza kila asubuhi huwa anatoka wapi.
Jamaa kwa kujiamini akajibu huwa nakuja kwa mchumba wangu,mwenyekiti ikabidi amwambie wazi kuwa huyo mchumba wako ni mke wa mtu na mama wa watoto wawili.
Jamaa alishangaa sana jinsi alivyoshindwa kulibaini suala lile,bila shaka dada alikuwa makini sana hata kuficha nguo za watoto wao na viatu.
Jamaa(mume)halali alitafutwa na kujulishwa kinachoendelea na alipombana mke wake alielezwa wazi kuwa hata mtoto wao mxhanfa ni wa jamaa.
Ila jamaa aliamua kusamehekabisa na akaahidi kuendelea kuishi naye,alimwambia kuwa kila mtu ana makosa so alikuwa tayari kumsamehe,akikumbuka jinsi walivyotoka mbali.
Jamaa alikuwa anampenda sana mke wake na hakuwa tayari kuachana naye ila tatizo lilikuwa kwa mke wake,mke wake aliweka wazi kuwa yeye hamtaki mumewe kwani jamaa amekuwa mlevi. Kiukweli jamaa alikuwa anatabia ya kunywa pombe,tangu wapo kijijini kama mnavyojua wanaume wengi wa vijijini. Dada anaonekana alilishwa maneno mengi na mchepuko wake kuwa ataolewa na ahadi nyingine nyingi.
Dada alikuwa mkubwa kwa mchepuko wake kwa miaka kadhaa pengine ndo sababu ya kutaka kuishi na jamaa(pengine alikuwa anasimamia shoo )
Basi baada ya kukataliwa kisa alikuwa hana jipya jamaa akaona akubali yaishe,alipojaribu kuwahusisha wazazi pia hilo halikufua dafu kwani,binti alijibu wazi kwa jeuri kuwa msimamo wake ni huo huo HAMTAKI JAMAA.
Basi maisha yakaanza upya kwa jamaa akilea watoto kama single father.. Aliendelea kuhudumia watoto wake huku x wake akaondoka nyumbani na kuhamia sehemu alikopangiwa na mchepuko wake.
Maisha yalienda miezi ikapita,jamaa mchepuko akaanza kumletea dada mawenge,inasemekena akiwa na jamaa zake alikuwa anawaambia anasubiri mtoto akue kue amchukue na kumpeleka kwa mama yake kijijini.
familia yake ilimsihi kuwa asijaribu kuwapelekea mtu huyo kama mkwe kwani kama aliweza kumsaliti mume wake basi hata yeye hatashindwa kumsaliti.
Jamaa akapata kademu saizi yake,na hakuwa anajificha tena ila alkuwa anaongea wazi na mchumba wake mbele ya mtu wake huyo.
Mpaka muda huu jamaa aliyeachwa na mke hana hamu na wanawake na huwa anasimulia watu kisa chake hiko na anaonesha wazi kuwa hataki tena kuoa,ni yeye na pombe tu.
Dada msaliti ameachwa kwenye mataa na jamaa kitu anachoambulia ni hela ya malezi tu kwa mtoto na biashara ilishakufa,anahangaika tu mtaani huku shoga zake waliokuwa wanajua tabia zake wakimsimanga.
Jamaa kashamkataa wazi kuwa hamtaki,na demu anaona noma hata kurudi kwa mume wake kuomba msamaha.
Ni uzi mrefu kidogo poleno wavivu wa kusoma nyuzi ndefu.
NIMEJIFUNZA NDOA ZINAZODUMU SANA HUWA HAZINA AMANI,ILA ZENYE AMANI SANA HUANDAMWA SANA NA MATATIZO.