Kipi bora kati ya kuishi na mpenzi (bila ndoa) au kufunga ndoa?

mkushite

JF-Expert Member
Sep 2, 2021
664
1,607
Kuna scenarios nyingi ambazo kwa mtu mwenye uelewa anaweza jiuliza bila ya kupata majibu. Mfano;

1. Unakuta mwanamke amezaa na mwanaume watoto 3 na wanaishi pamoja ila mwanamke analalamika kwamba bado hajaolewa na anatafuta mwanaume wa kumuoa.

2. Mwanamke anaishi na mwanaume kwa zaidi ya miaka 5 ila bado ananungunika kwamba bado hajaolewa na anadiriki kusema kwamba anatafuta mwanamme wa kumuoa.

3. Binti ana boy friend na tayari ashapitia mahusiano tofauti tofauti ila bado anaenda kanisani kuomba kupata mume wa kumuoa wakati ana mwanaume ana date naye, anashindwa nini kumbadilisha huyo mwanaume aliye naye kuwa mume?

4. Unakuta wapenzi wanaishi pamoja kwa muda mrefu wakiwa na adabu, heshima na furaha kabla ya kufunga ndoa, ila wakifunga ndoa mambo yanaanza kuvurugika mpaka ndoa inavunjika.

5. Wanandoa wengi wanaishi kwa kuigiza, hawana upendo na wanatamani kuachana na hicho kitanzi. Wengi wana michepuko na mahitaji yao ya kingono wanayapata nje ya ndoa.

Kipi cha msingi, kuwa na uwezo wa kuishi na mwanamke, kuoa au kufunga ndoa?
 
Najibu kwa kila namba..

1. Mwanaume kumzalisha haina maana kampenda. Mwanamke wa aina hiyo huwa hapendwi lkn hana masharti magumu kutoa k yake. Hivyo mwanaume humtumka kukata kiu yake na kujikuta kambebesha mimba.

2. Ukiona hivyo ujue mtu anaishi na mpenzi mwenye mpenzi wake.

3. Huyo ni fuska lkn hajijui kuwa ni fuska.

4. Hao ujue walioana kwa mihemko ya ngono lkn hawapendani. Na hiki ndiyo chanzo kikuu cha ndoa za miaka hii kuvunjika. Watu wengi wanaona wakati hawapendani .....mmoja anapenda mwingine anafeki..
 
Back
Top Bottom