Kingunge, Lowassa, Sumaye itakuwaje endapo watarejea CCM?

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,487
Hawa makada waliondoka CCM kwa mbwembwe nyingi ila kuna dalili wakarejea maana Sumaye ametoa masharti ambayo yakitekelezwa na CCM basi mwana mpotevu atarejea.

Lowasa nae akitoa masharti yake japo najua yanaweza yakawa magumu anaweza akarejea na Kingunge kama kawaida yake atamfuata. Swali ni je, ITAKUWAJE kwa UKAWA?

Hilo linawezekana sana kuliko Zitto na Dr. Slaa kurejea Chadema. Ikitokea hivyo utaamini siasa ni mchezo mchafu ama utaita mabadiliko? Stay tunned.
 

walioko ndani wenyewe wako kimya maana upepo hausomi sasa unauliza walioko nje? ni no vacancy!

kutoa masharti kunategemea na value ya mtoa masharti, unaweza kuwa ulikuwa na value enzi hizo lakini kwa sasa ikawa imepitwa na wakati.

kwa hawa wazee busara kwao ni kustaafu lakini wakijidai kutoa masharti watakuwa kama mwanangumi wa kimarekani tyson.

ukiona mambo yamebadilika wewe staafu mapema kulinda heshima.
 
Makaburi sio kuyafufua ni kuyaombea yalale salama
Itakua miujiza maiti akionekana karudi tena kwao akitembea
 
Aaa wapi! Nani atawapokea hao?
 
Lumumba bwana inaonekana hawa watu wanasumbua Sana vichwa vyenu, ni iman yangu uko ndotoni ukiamka itaelewa kuwa ulikuwa unaota
 
Kwani kuna dhambi gani? Kama mtu ametoa masharti na yakatimizwa anaweza kurudi kwani hizo kasoro ndio zilimuondoa.
Mfano mwepesi kwako mtoa mada ni hivi; Wewe uwe mumeo kakuacha kwa vile ni kahaba, muongo na mshirikina lakini akakupa masharti kuwa ukiacha tabia hizo atakurudia, sasa kama utamuahidi kuwa unaziacha kwa nini asikurudie mahabuba wake?
 
Kwani kabla hawajajiunga cdm kwani chama kilikuwa hakijiendeshi?
 
Kutoka moyoni katika siasa namuamini lowassa kuliko mtu yeyote. Nakuhakikishia lowasa hawezi kurudi ccm hadi mungu atakapomchukua duniani nina uhakika wa 10000000% kama umetumwa jibu ndo nimekupa najua na lowasa mwenyewe anaweza kudhibitisha hili tho sivyo wewe unavyotaka. Maana wapumbavu wa lumumba mpaka wamuelewe lowasa wanahitaji zaidi ya phd za chemistry kwa kiswahili.

Nenda umwambie aliyekutuma ukweli huu. kwa taarifa yenu mtasubiri sana lowasa kurudi kwenye nyumba ya majangiri.
 
miaka miwili iliyopita mliambiwa HUYU LOWASA MNAYEMTUKANA KIASI HIKI KWENYE MITANDAO, SIKU MKIKUTA YUPO CHADEMA ITAKUWAJE? Mkasema haitatokea milele chama kipokee fisadi kama huyo. Leo mpo nae, right?
 
Sasa wewe Sirtula kumbe unayo majibu ya maswali yako yote hapa unajaribu kumbabaisha nani?Mtu unaondokewa wazazi,mke au mtoto na unakuwepo itakuwa wao wakirudi ccm?Kwani kabla ya ujio wa vyama vingi hata hao viongozi wanaoiongoza chadema leo walitokea wapi?Kabla ya hao uliowaorodhesha hapo juu kujiunga chadema haikuwepo?Bado umesema ni haki yao na hujakosea wakitaka kama masharti watakayowapa ccm yakitekelezwa wewe utawazuia? Mwisho kwani wao watakuwa wa kwanza kukihama chama na kurejea?Mwapachu aliporejea tena ccm majuzi tu hapa hakupokelewa? Hizo kebehi na akili zako hizo ziendelezee huko huko Lumumba na uwe mjanja na mapema kabla ya mwezi June kesho kutwa uwe umetafuta ajira kwani Magufuli atakapopokea kofia ya uenyekiti ccm taifa atafutilia mbali kijiwe chenu cha majungu hapo Lumumba.Hazitokuwepo tena buku saba za kulipana kwa threds za kukashifu upinzani.
 
so akirudi ule wimbo wa kumwita fisadi nao utarejea?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…