Kinachokuumiza ni mawazo yako mwenyewe

Hii thread ni nzuri Sana ila nashindwa kuaccept coz nimeumizwa Sana Sana kiasi kwamba nikijitajidi nipotezee baada ya muda yanakuja nisaidie ni Jr Mshana
 
 
JamiiForums782338926.jpg
 
3150e1e2ea0b596d7851e3a0f2f68e71.jpg


Tulikuwa na ile mada ya ongezeko la watu wanoongea pekeyao! Wameumba maumbo Wameumba watu vichwani mwao kisha wamewabeba

Wanatembea nao
wanaongea nao
Wanabishana nao
Wanagombana nao
Wanawalaani
Wanawatusi kuwakejeli na hata kuwaua kihisia tu

Ni usongo wa mawazo na vurugu za kimaono, kwa kushindwa kujimudu! Kwa kushindwa kuzitawala hisia wengi huishia kupata magonjwa ya shinikizo la damu hata kufa

Unakubalije mtu akupotezee furaha yako? Wakati unahangaika kuwaza na kuwazua ukipata majibu mia kwa mpigo! huyu anayekusababishia maumivu yote haya yuko pahala mbali kabisa na wewe akiyafurahia maisha yake

4822d873d17bc7ee75d8808c089b762e.jpg


Tunaishi katika dunia ya changamoto za kila namna
Changamoto za mahusiano
Changamoto za kipato
Changamoto za kazi
Changamoto za majukumu mbalimbali
Changamoto za ki familia hata kiukoo
Changamoto za marafiki ndugu na jamaa nk nk

Jifunze kuwa wewe jifunze kusimama imara, usikubali wala kuruhusu hata siku moja mtu mwingine nje ya nafsi yako akutawale na kuyatawala mawazo na hisia zako kwa namna yoyote ile kwakuwa vyovyote iwavyo yeye atabaki kuwa yeye na wewe utabaki kuwa wewe

Ni pale tu utakapolikubali hili utayaona maisha na changamoto zake katika mtazamo tofauti kabisa

f76e3b00dc812c39025d27937dfae26f.jpg
Uzi bora kabisa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom