Kimenuka jumuiya za kimataifa, Rais Magufuli hasomeki

Kuna wingu zito kati ya ushirika wa NATO na mshenga wao Marekani na ule mlengo wa kushoto wenye wakumunisti wa zamani China na Russia.

Issue iko hivi.

Mabepali wa Ulaya na Marekani hawamsomi JPM kabisa, kama unavyojua kila Rais mpya anapoingia hawa ndugu zetu hufanya juu chini ili kupata nafasi ya kumteka katika upande wao, ili maslahi yao na ya makampuni kutoka kwao yalindwe. Sasa kasheshe likaanzia hapa

Mabepari walimualika Mh JPM katika mkutano wa Jumuiya ya Madola in personal, kwanza ili ajitambulishe kwa wenzie lakini pia wapate nafasi ya kuteta nae kuhusu interest zao, na kumvutia kwao. Jamaa hakwenda akatuma wawakilishi.

Wakamualika tena kikao cha mazingira na hali ya hewa, Ufaransa, ikiwa ni mara ya pili, ili kupata nafasi tena ya kutimiza ile adhma yao, jamaa tena kakomaa, hakwenda instead akatuma wawakilishi. Hii haikumfurahisha Uingereza kabisa na za chinichini zinasema akamtonya mshenga wake Marekani watunyime zile za MCC ili Mkuu wa kaya afunge safari kwenda kuwabembeleza na wapate nafasi ya kutoa masharti.

Mshenga akafanya hivyo kwa visingizio vya kitoto. lakini mpaka leo JPM hajaenda wala kubembelezea hiyo kitu. Jamaa wakapanic na wakaanza kufikiri labda JPM anahamia ukomunistini

Wakuminist kuona hivi, wakatupa karata yao, kwanza wakamualika kwenya kikao muhimu cha SINO Africa, wakijua jamaa hachomoi hapo, na kwa za ndanindani ujumbe wa Russia pia ulikuwepo huko SA, to their surprise JPM hakutokea instead akaenda VP. China na mshirika wake Russia wamesikitika sana hasa ukizingatia Russia anaitolea macho Gas yetu kwa muda sasa.

Ikumbukwe Tanzania ina reserve kubwa sana ya Uranium, Gas, na Coal , hivi ni vitu muhimu sana kwa hii miamba ya milengo miwili na mpaka sasa wanashindwa kumuelewa JPM. Hawamsomi wala hasomeki kwao

Nasikia soon Tutapata ugeni mzito, wameamua kuja wenyewe

JPM hasomeki, Hongera JPM
hii analysis imejaa alinacha.Hao jamaa unawasema wakimtaka magufuli wana njia nyingi tu za kumpata na wala magufuli kutokwenda kwake nje kwa sasa hakutokani na kwamba anawakwepa wakubwa bali bado hajamaliza kuunda serikali yake na kuinyesha njia hiyo serikali mwelekeo wake,subirini tu atasafiri sana tu na sitashangaa iwapo naye hantamsema kuqa anasafiri sana
 
Tatizo lugha kule hawaongei kiswahili,jk alipewa miaka kumi kuwa waziri wa mambo ya nje ili ajifunze lugha akaambulia kile anachoungaunga
Tuwe serious katika kujadili issues. Hii ni thread muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu. Kama unafahamu masuala ya international relations lugha haiwezi kuwa issue. Je, PUTIN huwa anazungumza lugha gani anapokutana na Cameron au Obama. Je, yule Rais wa China huwa anazungumza lugha gani kwenye mikutano ya kimataifa au anapokutana na Obama na wengineo. Hujui kuwa kuna wakalimani wanaoweka mambo sawa kwenye mikutano hiyo? Halafu, hii hoja mufilisi ya kwamba JPM hajui kiingereza imeanzia wapi? Tusilete hoja zisizo na maana. Sisi watanzania tuna inferiority complex za ajabu mno. Eti wengi wetu tunadhani kufahamu kuzungumza kiingereza ndio usomi... Kiingereza ni lugha kama zilivyo lugha nyingine. Mbona kuwa wamalawi huko Mwananyamala wengine ni ma-housegirl na wengine wakata michongoma na wazungumza kiingereza lakini maisha yao ni hohehahe? Kuna wakati watanzania walikuwa wanapeleka watoto wao Kenya na Uganda kusoma katika shule za huko na wakirudi na umahiri wa kuzungumza kiingereza wazazi hao, baadhi, walikuwa wanafurahia wakidhani kuwa hiyo ndiyo elimu... Sijui sisi watanzania tukoje..Wapo waztu wanakomalia eti JPM hajui lugha!!! Wapi na wapi??!!
 
Tatizo lugha kule hawaongei kiswahili,jk alipewa miaka kumi kuwa waziri wa mambo ya nje ili ajifunze lugha akaambulia kile anachoungaunga

Lugha gani?......, kichina, kifaransa, kiingereza, kiarabu ....au

Too low, unaheshimika sana humu, usitake tuamini kwamba uwezo wako wa kufikiri ni mdogo wakati siyo
 
Jidanganyeni magu hana uwezo wa kuwatikisa mabepari ila atatikkswa ww mnajifanya kama hamumjui us akitaka lake
 
Tatizo lugha kule hawaongei kiswahili,jk alipewa miaka kumi kuwa waziri wa mambo ya nje ili ajifunze lugha akaambulia kile anachoungaunga
Mleta uzi unabore, Issue ya MCC ilishaanza long na matokeo ya uchaguzi wa zenji kuharibiwa na Jecha+ccm.
Yaani nyie michongo ya foreign policy za marekani na uingereza zimewapita mbali sana.

Hata ile sentensi inayorudiwarudiwa ya marekani haina adui au rafiki wa kudumu bali maslahi yake nayo imewapita kushoto.
 
Tuwe serious katika kujadili issues. Hii ni thread muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu. Kama unafahamu masuala ya international relations lugha haiwezi kuwa issue. Je, PUTIN huwa anazungumza lugha gani anapokutana na Cameron au Obama. Je, yule Rais wa China huwa anazungumza lugha gani kwenye mikutano ya kimataifa au anapokutana na Obama na wengineo. Hujui kuwa kuna wakalimani wanaoweka mambo sawa kwenye mikutano hiyo? Halafu, hii hoja mufilisi ya kwamba JPM hajui kiingereza imeanzia wapi? Tusilete hoja zisizo na maana. Sisi watanzania tuna inferiority complex za ajabu mno. Eti wengi wetu tunadhani kufahamu kuzungumza kiingereza ndio usomi... Kiingereza ni lugha kama zilivyo lugha nyingine. Mbona kuwa wamalawi huko Mwananyamala wengine ni ma-housegirl na wengine wakata michongoma na wazungumza kiingereza lakini maisha yao ni hohehahe? Kuna wakati watanzania walikuwa wanapeleka watoto wao Kenya na Uganda kusoma katika shule za huko na wakirudi na umahiri wa kuzungumza kiingereza wazazi hao, baadhi, walikuwa wanafurahia wakidhani kuwa hiyo ndiyo elimu... Sijui sisi watanzania tukoje..Wapo waztu wanakomalia eti JPM hajui lugha!!! Wapi na wapi??!!
Well said mkuu. Kuna majitu ya ajabu sana siku hizi humu JF.
Hayana hoja wala sera yanakuja na single mpya ya Mh. Rais na kingereza.
 
Waongee na mabalozi huko au kama watakuja sawa. JPM toka awe rais hatujaona rais yeyote akimtembelea, hivyo ni sawa tu nae asipowatembelea,
 
Ulimbukeni ni tatizo kwa wabongo, kuongea kiingereza sio kupata maendeleo
 
Nafikiri kwa Rais kukaa kimya ni silaha nzuri zaidi kuliko kuanza kujikombakomba kwa wanaojiona ni wakubwa. Sisi ndiyo wanaotuhitaji kuliko tunavyowahitaji wao kimalighafi. So mh. Rais komaa wasikuelewe. Wakija wenyewe unawapa masharti kama hataki aondoke
 
Huwezi kumchenga mchina au mzungu eti ukajitegemea mwenyewe,haiwezekani,nchi zote zinategemeana isipokuwa inatakiwa mikataba ambayo iko fair.uwekezaji wote unategemea wageni,imports and exports zinategemea wageni,mtauza wati madini na mazao yenu kama mnajifungia ndani.economic diplomacy ni muhimu kwa sasa
 
Ni raisi gani wa Tanzania aliwahi kutumia wakalimani?Hujui adha ya aibu wewe tena kwa magazeti ya Tanzania na watu wake wanavyoongeaga.

JPM ni mtumishi wa watanzania, anawajibika kujua kiswahili, hizo lugha nyingine sio lazima wakalimani wapo na ataeleweka tuu .
 
Tatizo lugha kule hawaongei kiswahili,jk alipewa miaka kumi kuwa waziri wa mambo ya nje ili ajifunze lugha akaambulia kile anachoungaunga

HIVI WACHINA WAKIWA KWENYE MIKUTANO YA KIMATAIFA HUWA WANAONGEA LUGHA GANI? TUAMZIE HAPO KWANZA!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
HIVI WACHINA WAKIWA KWENYE MIKUTANO YA KIMATAIFA HUWA WANAONGEA LUGHA GANI? TUAMZIE HAPO KWANZA!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Usijifananishe na mchina.mchina yuko level ya USA kiuchumi na kitechnolojia so ana jeuri ya kukomalia lugha yake.si unajua jeuri ya pesa
 
Back
Top Bottom