Kila Rais wa Tanzania anafanya vibaya, ndiyo maana hujuta mwishoni

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
18,687
47,123
Watanzania wamezungumzia ubaya wa katiba yetu tangu siku nyingi.

1. Mwalimu Nyerere alikiri kuwa katiba yetu ni mbaya.

2. Bunge la mwaka 1993 lililopitisha maamuzi ya kuundwa kwa Setikali ya Tanganyika, lilidhihirisha pia jinsi katiba yetu ilivyokuwa mbovu. Fikiria, Bunge lilifanya maamuzi, Serikali ya JMT ikaridhiaa maamuzi ya Bunge, mtu mmoja tu, Mwalimu Nyerere, akiwa Mwenyekiti wa CCM aliweza kufuta maamizi ya Bunge na ridhio la Serikali.

3) Tume ya Jaji Warioba iliyoundwa kwa sheria maalum ya Bunge. Ikazunguka nchi nzima ikachukua maoni ya wananchi wa kada mbalimbali, ikafanya majumuisho kwa weledi mkubwa, mtu mmoja tu, Rais Samia kafuta maoni ya wananchi wote, kisha akaanzisha katume bandia kasikotungiwa hata sheria yoyote, halafu baadaye mtu mmoja tu, tena mwenye weledi mdogo sana, Waziri, anasema eti Watanzania wanatakiwa wafundishwe kwanza kwa miaka mitatu kuhusiana na katiba kabla ya kupata katiba mpya!! Huu ni uhuni wa hali ya juu unaodhihirisha namna katiba yetu ilivyo mbovu. Inawezekanaje mtu mmoja tu, Samia afute matakwa na maamuzi ya wananchi mamilioni, kwa maslahi yake binafsi?

4) Tume huru ya uchaguzi haiwi huru kwa sababu tu umeamua kuiita huru. Uhuru wa Tume unategemea zaidi muundo wake, na sheria inayoielekeza namna inavyotakiwa kufanya kazi. Kwa sheria ya sasa hii ni Tume ya Rais ya kusimamia uchaguzi. Huwezi kuiita ni Tume huru wakati inamilikiwa na Rais. Wajumbe wanaopendekeza viongozi na watendaji wa Tume wote ni wateule wa Rais. Yaani mteule wa Rais anampendekeza mtu mwingine kwa Rais ili naye awe mteule wa Rais!! Huu ni upuuzi!! Kama Rais atawateua watendaji wa Tume ya Uchaguzi, ni lazima wapendekezaji wa majina hayo ya watendaji wawe ni watu ambao ni huru, siyo wateule wa Rais directly au indirectly. Kisha Tume iwe huru kutengeneza kanuni zake zitakazoongoza namna ya kusimamia uchaguzi, ikiwemo kutengeneza sifa za wasimamizi wa uchaguzi na namna ya kuwapata.

NB: Kinana amepotoka sana ama kwa sababu ya uzee au kwa sababu ya unafiki. Anasema eti wanaotaka katiba ni CHADEMA. Mara eti hata nchi nyingine, Rais huwa mteuzi wa wajumbe wa Tume ya uchaguzi. Tumwombe Kinana alete mfano japo wa nchi moja ambayo muundo wa Tume na uteuzi wa Watendaji upo kama huu wa hapa kwetu, halafu Tume hiyo inaitwa Tume huru ya Uchaguzi. Najua hana mfano hata mmoja. Kwanza katika nchi zote za kidemokradia, hakuna nchi hata moja ambayo Jaji mkuu anateuliwa na Rais pekee bila kuhusisha taasisi nyingine.

Mara eti CHADEMA ilitaka suala la katiba mpya liwe la CHADEMA na CCM tu!! Huu ni uwongo mkubwa. Hivi tume ya Warioba ilikuwa inakusanya maoni ya wanachama na viongozi wa CHADEMA pekee? Yaani wananchi wote waliosema wanataka katiba mpya wakati ule, siyo baadaye, walikuwa ni CHADEMA? Kwa nini viongozi wetu wanapenda uwongo na kutetea vitu visivyo na tija kwa Taifa?

Ushauri Kwa Kinana:
Ukishafikia umri ulio nao, jitahidi kuchangia mambo yenye tija kwa Taifa ili kwayo Taifa likukumbuke. Usiumalizie uzee kwa kuacha kumbukumbu mbaya. Angalia wafuata:

1) Nyerere, wakati wa uzee wake alisema katiba yetu ni mbaya na inamfanya Rais kuwa dikteta.

2) Mkapa akasema anajutia kuruhusu CCM kuiba pesa ya Serikali, mauaji ya Zanzibar. Na akasema, angetamani Tanzania ingekuwa na Tume huru ya uchaguzi (akimaanissha kuwa Tanzania haina Tume huru ya uchaguzi).

3) Mwinyi akasema anajutia kutengeneza cheo cha Naibu Waziri Mkuu, na kumpa Mrema, cheo ambacho hakikuwepo kikatiba.

Tuwasaidia akina Kinana na Samia kuhakikisha yaliyo sahihi yanafanyika, wapende wasipende, ili tusiwafanye wajutie wanapoondoka kwenye nyadhifa zao.
 
Cdf alisema Kuna wageni wengi wapo kwenye vyombo vya maamuzi nchini,katika kundi hili mzee kinana yumo.

Tuhumu zake za biashara ya meno ya Ndovu,ni ishara ya kukosa maadili,Binafsi siwezi msikiliza Kinana.
 
Duh

Chadema mnaamini Mbunge anawakilisha Watu bungeni au anawakilisha Hoja?

Mnyalukolo, ebu jibu swali lifuatalo:

Mbunge anachaguliwa na hoja ili akawakilishe hoja Bungeni,
au Anachaguliwa na wananchi ili akawawakilishe wananchi Bungeni?
 
Inasikitisha sana

Wanafanya makosa wakosa wakiwa madarakani, wanajutia wakati wakiondoka madarakani!! Na sisi tunaona ni sawa!!

Samia anapora na kuzigawa rasilimali za nchi kwa wageni, halafu akitoka madarakani aje aseme najutia kuzigawa bandari, misitu na mbuga za wanyama kwa wageni! Halafu na sisi tumshangilie kuwa eti muungwana, angalao anekiri makosa yake!!!
 
Mnyalukolo, ebu jibu swali lifuatalo:

Mbunge anachaguliwa na hoja ili akawakilishe hoja Bungeni,
au Anachaguliwa na wananchi ili akawawakilishe wananchi Bungeni?
Wananchi huchagua chama kikawawakilishe bungeni

Lakini " Mbunge" huchaguliwa na Hoja kwa Hoja

Ndio sababu Wabunge wa CCM na ACT Wazalendo wako baridi sana kwa sababu uwepo wao bungeni hutokana na Vyama vyao lakini siyo binafsi yao

Wabunge wa Chadema huchaguliwa kwa Hoja zao binafsi na ukichunguza utakuta huwa wanatokea kule kinapoishi Kizazi Cha Kuhoji

2015 Lowassa aliiharibu Chadema na watu wengi walichagua Chama na Ndio sababu Magufuli akapita mule mule kuwachukua Wabunge wote wa Lowassa kwa sababu hawakuwa na nguvu binafsi

Uwe na Jumatano yenye Baraka 😄
 
Unafikiri hawajui wafanyalo ?

Wanafanya makusudi wakijua hawawezi shitakiwa hiyo kuonesha kujuta baada ya kumaliza muda wao ni ulaghai tu.
 
Back
Top Bottom