Kijana wa miaka 25 kuendelea kama bado umekaa kaa tu kwenu jitathmini upya

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,431
12,292
Kijana wa miaka 25 kuendelea kufungua hotpoti asubuhi na jioni huku kazi yako ni kukesha tu sebleni na maseries ya kikorea

Aiseeee jitathmini.....

Wengi hapa hasaa wale wahitimu wa vyuo ndio mda wao wa kusingizia kuwa wanasubiria ajira huku wakiendelea kuwatesa wazazi tu kazi kula kulala

Wazazi wanawaangalia tu lakini wana mengi moyoni mwao yamejificha

Tafuteni hata kibarua jamani mjiongeze

Alafu kinachotuharibu ni tabia ya kuchagua kazi yaani ukiwa na kadegree chako basi ushajiona wewe ndio wewe basi siku nzima upo na tv pembeni una mikeka yako ya kubeti hutaki shida baba na mama wapo

Wengine ukiwatafutia hata kazi za viwandani hawataki hata kusikia kisa wana elimu nzuri... ha ha ha

Mimi mwenyewe nlihitim (.......) 2013 tena nlisomea civil engineering lakini nilisota kwa mwaka mmoja na nusu nikiwa nafanya kazi za viwandani hadi kuja kutoka

********* ******** ******* ****** *****

NILIFANIKIWAJE?

Baada ya ya mimi kumaliza chuo mwaka 2013 kipindi hicho nilikuwa nakaa chumba 1 cha kupanga (getto) na wanafunzi wenzangu wawili, Baada ya kumaliza tu wazazi wangu waliniambia nirudi nyumbani Arusha

Kipindi hicho sikurudi nyumbani ilibidi nidanganye kuwa kuna projects ambazo bado hatujamaliza hivyo nlihitajika bado kuwepo dar

Basi wazazi wakakubali kwa shingo upande kwani hata wao kitabu wamepiga hivyo taratibu zote za vyuoni wanazijua hivyo ni ngumu kuwadanganya lakini hawakuwa na jinsi ikabidi wanikubalie tu

Hivyo tukajipanga na wenzangu nliokuwa nakaa nao getto kuwa wakati tunafight kutafuta ajira tuliyosomea ni lazima tutafute hata kibarua kwanza cha kujishikiza na yote hayo tulifanya kwasababu hatukuwa na ndugu yoyote(refa) katika kampuni yoyote ya ujenzi kutuwezesha kupata kazi kirahisi hivyo ilitubidi tusimame kwa miguu yetu wenyewe

Inaendelea.........
 
Mkuu.vipi wanakuomba chakula.
 
haya malalamiko yako yamenikumbusha mbali sana.

nilipo maliza shule, x-wangu kila siku kulalamika ntakaa na wazee wangu mpaka lini? nitoke nikajitegemee kumbe kulalamika kote alikuwa anataka nikapange ahamie kwangu.

nikaenda kupanga wiki 2 kasha jaza minguo yake na kuhamia kiaina mpaka pale nilipo hama mkoa.

mkuu kukaa home wakati mwingine tunapunguza kero za uzinzi/kuoa bila kukusudia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…