realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 1,539
- 3,214
Niwakumbushe tu vijana wa kudai haki zenu hakikisha unatimiza wajibu wako.
Mfano kama ulisomeshwa vizuri na wazazi wako na wewe ukatimiza ushauri wa wazazi wako na ukakosa ajira ni haki yako kudai haki.
Kama unafuata sheria za nchi kama katiba inavyoeleza una haki ya kudai haki. Sio ujiingize kwenye maandamano na mibangi bangi yako ukadhani utaachwa hapana huwezi achwa.
Mzalendo wa nchi yake hawezi kudai haki yake kwa kuharibu vitu vilivyotumia pesa nyingi na muda kuviandaa ukaviharibu kwa siku moja.
Haki haidaiwi hivyo.
Nakukumbusha tu kuwa baada ya maandamano yenye uharibifu yanaweza kusababisha maisha kuwa magumu zaidi kwa sababu pesa nyingi itatumika kurekebisha miundombinu.
Jingine hakikisha una pesa ya kutosha kwa ndugu zako watakaokuja kukuhudumia hospitali waweze kukupikia chakula. Usije ukasumbua watu.
Jiulize ulitimiza wajibu wa kuhudhuria kwenye mikutano ya mitaa na vijiji kutoa maoni?
Ulishiriki kutoa maoni ya miswada mbalimbali Bungeni.
Dai haki kwa kutimiza wajibu Kijana.