Kijana aliyeanzisha vita ya Syria

View attachment 470353
Mouawiya Syasneh alikuwa na umri wa miaka 14, mwaka 2011 akiwa anaishi katika mji wa Deraa, Syria.

Mouawiya Syasneh alianza kwa kuandika ujumbe wa kuiponda na kuikosoa serikali kwenye kuta za shule aliyokuwa akisoma kwa kutumia rangi za ku spray.

Hakujua kuwa kitendo kile kingezua maandamano ambayo yangepelekea vita kubwa ambayo ingeendelea kwa miaka mingi.

Leo ni zaidi ya miaka sita, vita imekuwa kubwa na isiyo kwisha huku yeye Mouawiya Syasneh akiwa mstari wa mbele akipigana upande wa waasi.

Watu zaidi ya nusu milioni wamekufa akiwemo baba yake, ndugu marafiki na jamaa.

Mouawiya Syasneh anasema laiti angejua kuwa matendo yake yangeleta maafa haya, wala asingethubutu kuandika ujumbe ule uliobadili historia ya nchi yake.

Usikose kutazama documentary ya the boy who started the syrian war kupitia aljazeera.
Kilichoanzisha vita sio kilichoandikwa ukutani na hao watoto, ni walichofanywa hao watoto na serikali baada ya kuandika
 
View attachment 470353
Mouawiya Syasneh alikuwa na umri wa miaka 14, mwaka 2011 akiwa anaishi katika mji wa Deraa, Syria.

Mouawiya Syasneh alianza kwa kuandika ujumbe wa kuiponda na kuikosoa serikali kwenye kuta za shule aliyokuwa akisoma kwa kutumia rangi za ku spray.

Hakujua kuwa kitendo kile kingezua maandamano ambayo yangepelekea vita kubwa ambayo ingeendelea kwa miaka mingi.

Leo ni zaidi ya miaka sita, vita imekuwa kubwa na isiyo kwisha huku yeye Mouawiya Syasneh akiwa mstari wa mbele akipigana upande wa waasi.

Watu zaidi ya nusu milioni wamekufa akiwemo baba yake, ndugu marafiki na jamaa.

Mouawiya Syasneh anasema laiti angejua kuwa matendo yake yangeleta maafa haya, wala asingethubutu kuandika ujumbe ule uliobadili historia ya nchi yake.

Usikose kutazama documentary ya the boy who started the syrian war kupitia aljazeera.
Wakati huku mwanangu wa miaka 14 bado anachezea makopo, haelewi chochote kuhusu serikali
 
698bbfe2e52b2499fedf2fc543751594.jpg
7c5edaa2a619b84f4a0499ef6f04746c.jpg

Aisee kumbe haya mambo yanaweza kuleta uchochezi mkubwa.
 
Hakuanzisha vita. Conditions zote za vita zilikuwepo tayari. Yeye alikuwa "the straw that broke the camel's back".

Mos Def katika wimbo wake "Mathematics" ameuliza swali na kujibu mwenyewe.

"Why did one straw break the camel's back? Here's the secret:
The million other straws underneath it - it's all mathematics" Mos Def -Mathematics
 
Aliandika maneno gani
Ya kuisema serikali na viongozi, bahati mbaya mkuu wa usalama pale shuleni kwa alikuwa ana uhusiano na Mke wa rais Bashir Al-Asad, hivyo huyo kijana na wenzake walikamatwa na kuteswa sana kisha walihamishiwa polisi wakaendelea kushikiliwa.
Wazazi hawakuruhusiwa kuwaona hao watoto na waliambiwa wawasahau kabisa.
Raia wakaandamana na kukaa barabarani karibia na kituo cha polisi.
Wakaahidiwa wangewaletea watoto wao, lakini jioni wakashambuliwa kwa risasi na watu kadhaa wakafa.
Hapo ndipo kulipozuka maandamano zaidi na hasira zaidi.
 
Back
Top Bottom