Kuelekea 2025 Kigwangallah ashiriki maombolezo ya aliyekuwa Kamanda wa Sungusungu, Mzee Chalya. Aahidi kujitolea pikipiki moja kwa kila kata

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Karungikana

JF-Expert Member
Jan 8, 2017
913
844
1722188571672.png

Picha ya Kigwangalla akifanya mambo ya mila​

===

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kigwangalla aeleza ukaribu wake na Sungusungu kutoka kijijini Bujuku ambako alienda kwaajili ya maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mwenyekitu wa Sungusungu eneo hilo. Ambapo mbali na kutoa salamu za rambirambi aliahidi kujitolea kuwajengea uwezo wa kikazi jeshi letu kwa kuwaletea piki piki moja kila kata.

Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Sungusungu ni wadau wakubwa wa usalama wa raia na mali zao nyumbani kwetu. Toka nimeingia kwenye siasa nimekuwa nao karibu sana siyo tu kwenye shughuli za usalama bali pia za kisiasa na maendeleo.

"Hapa walinialika kijijini Bujulu, kata ya Lusu ambapo tulikuwa na maombolezo ya msiba wa Kamanda wa Sungusungu Mzee Chalya, ambaye aliuawa kikatili na mwili wake kutupwa kwenye duara la zamani la wachimbaji wa dhahabu.



"Kwenye Sungusungu kuna kikosi cha ‘ndege ya hasi’ (au ndege ya chini…ni intelligence ya jeshi letu) ambao, kwa umahiri mkubwa sana walifanikiwa kulisaidia jeshi la polisi kuwapata wauaji wa Mzee wetu Kamanda Chalya.

"Pamoja na kutoa salamu zangu za rambi rambi kwa familia na Sungusungu, niliahidi kujitolea kuwajengea uwezo wa kikazi jeshi letu kwa kuwaletea piki piki moja kila kata.

"Kwenye ziara hii niliambatana na mwanangu Hamisi Kigwangalla Jr."
 
Back
Top Bottom