Kigwangalla: Serikali kupiga Marufuku Matumizi ya Pombe za VIROBA Kufikia Mwezi wa Sita mwaka 2017

Nakumbuka mwaka Jana mwezi flani waziri wa mazingira alisema kufikia January 2017 pombe za viroba hazitakuwepo watatafuta vifungashio vingine ili kutunza mazingira lakini hadi Leo zipo na zinaendelea kuzalishwa ,Sasa huyu naibu waziri wa afya kasema hadi kufikia June 2017 serikali itapiga marufuku utengenezwaji wa viroba ,hizi kiki zingine bhana viroba hata wakizuia ni kazi bure pale tofauti ni vifungashio ila pombe ni Ile Ile watapiga marufuku konyagi ya karatasi wakati ya kwenye chupa ni ile Ile watapiga marufuku Kiroba oriGINal wakati Ile ni K-VANT hizi kiki za wanasiasa bhana zinachosha
Nilifikiri wanapiga marufuku pombe ya Viroba kumbe wanapiga marufuku viroba (vifungashio)!!! Hivi viongozi wa serikali hamuoni kuwa pombe za viroba / power na zinazofanana na hizo zinaua nguvu kazi ya taifa? asilimia kubwa kama si wote wanaotumia viroba wanafanana na mateja wanaotumia madawa ya kulevya. nadhani hata pombe ya viroba ingekuwa classified kama madawa ya kulevya.
 
Back
Top Bottom