Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 16,997
- 20,329
Juzi mwanamama Diane Rwigara alitangaza rasmi kwamba atawania urais wa Rwanda ili kuhakikisha anapambana na kumuondoa rais Paulo Kagame, Siku mbili baadae Zimetoka picha za Utupu za Dada huyu...
Wadasi wa mambo wanasema kwamba mamlaka za Kigali zimehusika na mchezo huu ili kumdhibiti mwanasiasa huyu asiwanie urais wa nchi hiyo. Lakini mimi nalitazama tukio hili kwa jicho la mbali zaidi, naiona Kigalo kwa kutumia idara yake yakijasusi ya NISS inaamua kuidhibiti Afrika Mashariki kupitia Bunge la EALA, Picha za utupu za Diana ni onyo tu na ni kitisho kwa wabunge wa mataifa wanaounda EALA. Kigali inaamini ili kudhibiti Jumuiko la Afrika Mashariki linaloungwa na nchi sita, ni lazima udhitibi Bunge lake.
Nikirejea katika tukio la picha naitazama nadharia ya picha za kupandikizwa ambapo kwa jicho jadidi la nera, (forensic image analysis) utaona "pin hole camera" kwenye kioo cha kujitizama either ni hotel au nyumbani kwa mwanasiasa huyu. Picha nyingine ni kwenye sofa akiwa anaangalia TV au Dirishani ila sio pozi la kupigwa picha.. (Kwasababu za kimaadili sitaziweka picha)
Kigali inapiga ndege wawili kwa jiwe moja, kubwa ni kama nilivyoeleza hapo juu, lakini jamjo lingine muhimu kwa Kigali ni kumjaza hofu Dada huyu ili asigombee,au kupunguza kuaminiwa kuwa hana maadili. i
Ikumbukwe hizi picha hajakutwa akifanyiwa tendo lolote chafu, na pia hajatembea uchi barabarani au kanisani, Ndo maana binadamu tunazo nguo kwa kuwa kila MTU anao utupu,
Hii isiwatishe Dada Zetu wanaotaka kugombea nafasi mbali mbali hasa u Spika na unaibu wa EALA, kama wa Tanzania tuungane kulikemea jambo hilo maana hakuna atakayebaki salama tukiiruhusu hofu hii kwa Jumuiya yetu..
Ukusanyaji wa taarifa za kijasusi njema na mbaya umekuwa mpevu mno ambapo mashirika, idara na jumuiya za ujasusi nimekuwa zikiushiriki kwa mbinu nyingi sana. Ujasusi una zana na mbinu za hali ya juu za namna ya kuzikusanya kiteknolojia au upandikizaji wa watendaji wa mashirika husika kwenye jumuiya za kiserikali, zisizo za kiserikali, makundi, vyama vya siasa mfano Chadema au CCM, taasisi za serikali na binafsi ndani na nje ya nchi ili kupata taarifa muhimu, mipango na mikakati (intelligence gathering devices). Hivi leo, kompyuta yaweza kuunganishwa na nyaya ama kwa upepo (wireless) kisha kuwekwa kifaa kidogo mahali popote, iwe ofisini au kwingineko ambacho huweza kufuatilia nyendo za wote wanaopita jirani na mahali hapo.
Kifaa hicho kilichounganishwa na Kompyuta huweza kuchukua picha na kuzisafirisha hadi kwenye kompyuta ambapo mtumiaji huzitumia atakavyo iwe kiulinzi au kiukachero. Kamera ndogo sana (micro-cameras) ndizo zitumikazo kuchukua picha za matukio, taswira za maeneo au watu wanaolengwa na mashirika ya kijasusi bila ya wenyewe kubaini.
Kutokana na shughuli za ujasusi kupiga hatua kubwa, simu za upepo na kamera ndogo ambazo huko nyuma zilikuwa zikitumiwa na mashirika au jumuiya za kijasusi, hivi sasa ruksa kutumika maeneo ya uraiani kwa ajili ya huduma za kijamii. Kamera hizo huweza kufichwa sehemu mbali mbali ambazo huwa vigumu kubainika. Sehemu hizo ni pamoja na tai za mashati, kosi za fulana, taa za mezani, saa, kalamu, mawani, makoti, soketi za umeme za ukutani, vitabu, kofia, radio ndogo za kushika mikononi, wanasesere, simu za mikononi, ashtrei za sigara, milangoni na vyombo vya kugundua moto pamoja na maua ya mapambo ya nyumbani.
Kamera hizo huweza kupachikwa kwa baadhi ya wanyama hasa wale wafugwao nyumbani ili kuweza kunasa picha na mienendo ya kila siku ya watu wanaotafutwa bila ya wao wenyewe kufahamu. Kamera zenye ukubwa wa kati ya milimita mbili au sentimita chache hivi, zina uwezo wa kupiga picha kubwa na nzuri zinazolingana na zile zipigwazo na kamera kubwa.
Uwezo huo unatokana na betri zake kuwa na nguvu inayowezesha kamera kuchukua picha za aina zote zisizo za rangi (black-and-white) na za rangi (coloured). Baadhi ya kamera hizo huweza hupiga picha mfululizo bila ya kusimama, nyingine huweza kuwekwa maeneo ya matukio kisha kufuatilia kila kitu kwa kasi ndogo sana kisha kujizima pindi tukio au matukio yanapokwisha. Betri za kamera hizo zina uwezo mkubwa wa kuifanya ipige picha kwa muda mrefu. Aidha baadhi ya kamera hizo (infra-red cameras) zaweza kupiga picha eneo lenye ukubwa wa mita 150 sawa na futi 450 hata kama lina kiza kinene.
Zipo ‘bugs’ ambazo ni vifaa nyeti vya kunasia siri ambavyo huwekwa maeneo maalumu hasa kupitia mitambo ya elektroniki na kompyuta ili kuzuia kuingiliwa na mawasiliano mengine au kupitisha taarifa za kijasusi kutoka eneo moja kwenda jingine. Mtu anayenasa taarifa hizo huweza kukaa umbali wa mita 100 na zaidi na bado akaweza kusikia kikamilifu kila kinachozungumzwa kwenye vikao, kumbi au ofisi husika.
Utengenezaji wa vifaa hivi nyeti, ununuzi na upandikizaji wake, hugharimu mamilioni ya dola za kimarekani. Kwa sababu hiyo, mara nyingi ni idara za kijasusi tu zenye uwezo wa kumiliki, kuchunguza na kupeleleza uhalifu au njama kupitia simu (bug telephones) kwa kupachikwa maeneo yanayoshukiwa.
Zipo aina nyingine za utegaji na ufuatiliaji wa simu zikiwemo za unasaji wa sauti na kuzibadilisha kwa namna tofauti zinazoweza kutumiwa na mashirika ya kijasusi, idara za usalama na upelelezi zikiwemo zile za mawimbi ya redio ambayo baadaye hugeuzwa kuwa sauti kamili kuweza kuzisikilizwa vyema na wachambuzi wa taarifa na matukio walioko komandi kuu za usalama na ujasusi.
Hidden pin hole cameras Mara nyingi huwekwa kwenye dressing table Murrow ili kupata picha za utupu
Dada Zetu wanapokuwa hotel rooms wasiache khanga hata kama yuko peke yake,au Taulo
Smoke detector pia huwa na camera,nyingine nyingi haziwekwi na wamiliki wa Hetels ila majasusi,zinakuwa WiFi camera zenye uwezo mkubwa wa kuhifadhi nishati pia megapixel ili ziweze kutoa rangi na hata Zooming (kuvuta taswira)
Na Yericko Nyerere