Kifo cha Mitandao, uwe mwanzo wa CCM kurudi kwenye misingi

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Mwaka 1987 wakati wa mkutano mkuu wa CCM kule Kizota Dodoma, mwanachama mmoja wa CCM alimuuliza mmoja wa wale waliokuwa wanataka uongozi kama anazijua kanuni za msingi za CCM. Mwalimu Nyerere akaingilia kati na kumkejeli muuliza swali, huku akisema kuwa swali alilouliza halipaswi kuuulizwa katika ukumbi wa mkutano. Wajumbe wote waliokuwa ukumbini wakamcheka muuliza swali.

Lakini nyuma ya lile swali kulikuwa na ujumbe mzito sana. Hoja ya muuliza swali ni kutaka kujua kama wote wenye kutaka uongozi kwenye chama wanaunganishwa na nia moja na wanachama wote waliobakia. Umuhimu wa mwana CCM kuwa tayari kuzifahamu kanuni za msingi za chama chake, umekuwa ukipuuzwa sana ndio maana bila hata ya aibu baadhi ya wanachama hawakuona taabu kuanzisha mitandao ya kirafiki ndani ya CCM.

Wanachama wa CCM waliipuzia misingi inayowaweka pamoja kiasi cha kuwa tayari kuigawa nchi kwa sababu za kibinafsi. Na zipo habari kuwa ni tangu enzi zile za miaka ya 80 mwishoni, ndipo hawa watafuta urais waliopigwa chini mwaka jana, walipoanza kutengeneza makundi ya watu watakaowaunga mkono mbeleni. Rais wa awamu ya tano ambaye inaaminika kuwa hakuwa na wafuasi wa siri, anayo bahati ya kuongoza nchi wakati yale makundi yenye tamaa mbaya yakikosa nguvu na hamu ya kuendelea kujiweka sawa kwa nia za kupata madaraka. Labda yaibuke makundi mengine miaka ijayo.

Na aitumie vizuri bahati hiyo kwa kuendeleza uadilifu ili CCM irudi kwenye zile enzi za mtu kujiunga na chama kwa sababu ya itikadi na sio kwa sababu ya kutaka kuganga njaa. Ni mambo yanayowezekana kutekelezeka, wala sio njozi.
 
Phillipo Bukililo ndugu yangu naomba nikuulize kwa nia njema 1987 mkutano mkuu wa CCM walikuwa wanakaa Kizota?huo mwaka sikuwa nimezaliwa ila wazazi wangu walikuwepo na walishiriki siasa na mimi sasa nashiriki 100% unaujua ukumbi wa CHIMWAGA?nia yangu ni kuelimishwa tu
 
Ni kweli Magu amebahatika lakini cha kusikitisha ni kwamba mpaka sasa inaonyesha hawezi kuitumia hiyo bahati hata kuifanya CCM iendelee kuaminiwa
 
Kizota ni ukumbi, lakini sina hakika kama bado upo au umebomolewa. Nadhani walikuwa wanakaa kwenye mahoteli ya Dodoma. Ukumbi wa CHIMWAGA nausikia, na wenyewe upo Dodoma.
 
hakuna tena Mtanzania anaweza kuikubali CCM wataendelea kuiba kura na kubaka democracy ya watanzania .

swissme
Kwa jinsi ambavyo rais JPM anavyowajali walio wengi, hata mimi naunga mkono wizi wa kura uliofanywa na CCM. Waliiba kura ili JPM aje kumpigania mtu wa chini kabisa, ni wizi mwema kwa taifa letu. Wizi wa CCM naukubali kwani aliyepewa nchi ana afadhali mara 1000 kumlinganisha na yule wa UKAWA, aliyeshindwa hata kuongea na mwandishi wa habari wa BBC, akadai eti anaonewa!!.
 
Ccm wakitaka wapate angalao heshima kidogo, wampe maalim Seif na wazanzibar ushindi wao
 
Basi Kizota ni ghara la mahindi CCM wameanza kutumia baada ya CHIMWAGA kuchukiliwa na serikali yaani chuo kikuu cha UDOM,hiyo miaka ya Nyerere walikuwa wanakaaga vikao vyao UKUMBI UNAOITWA CHIMWAGA kwasasa upo mdani ya eneo la chuo kikuu cha dodoma(mlimani/social)
 
Ni kweli Magu amebahatika lakini cha kusikitisha ni kwamba mpaka sasa inaonyesha hawezi kuitumia hiyo bahati hata kuifanya CCM iendelee kuaminiwa
Wale wa CCM wanaitwa kundi la watu 46, ni wachache sana mitandaoni. Kwa hiyo usidanganyike na hizi siasa za CDM kwenye mitandao ukadhani kuwa zinawakilisha maoni ya wananchi wengi, maoni inayoyasoma kwenye media ni sehemu dogo sana ya uhalisia wa mambo, endeleeni kudanganyika.
 
Kizota ni kata kubwa ambayo kwasasa inaongozwa na diwani na wenyeviti wa chadema,pia inaviwanda na maghara makubwa na ni kata ya pili kwa watu wengi mkoani dodoma
 
Mkuu uhalisia wa mambo huku mtaani CCM inachukiwa haitakiwi, mnalazimisha wapuuzi nyie, vijiji vingi mikoan nimeenda CCM haitakiwi, ila mnalazimisha kupendwa, kinokusaidieni ninyi ni polisi tu
 
Ona unavyojivua Nguo, wizi ni wizi tu, wapi kwenye bible wamesema kuna wizi mbaya Na mzuri, halafu Magu anajipigania yeye Na CCM wala hayupo kwa ajili ya mtanzania
 
Mkuu uhalisia wa mambo huku mtaani CCM inachukiwa haitakiwi, mnalazimisha wapuuzi nyie, vijiji vingi mikoan nimeenda CCM haitakiwi, ila mnalazimisha kupendwa, kinokusaidieni ninyi ni polisi tu
Wenye akili na busara wanawatazama jinsi mnavyohangaika na sarakasi zenu za CDM. CCM kila kiongozi anaheshimu muda wake anaopewa madarakani, nyinyi kwa sababu mmezidiwa akili na Mbowe mmekubali jamaa ajiongeze muda kwa kusigina katiba. Wapuuzi ni nyinyi mnaopokea makapi ya CCM, halafu mnategemea kushinda wakati wa uchaguzi. Jipangeni mje kisayansi, kwani uwezekano wa nyinyi kupotezwa jumla ninauona dhahiri kabisa.
 
Ona unavyojivua Nguo, wizi ni wizi tu, wapi kwenye bible wamesema kuna wizi mbaya Na mzuri, halafu Magu anajipigania yeye Na CCM wala hayupo kwa ajili ya mtanzania
Uwezo wako wa kuelewa umeshindwa kuielewa sarcasm iliyotumika kwenye hayo maandishi, lakini wengine wengi tu wamenielewa.
 
Vijana 46 nawe ukiwa mmoja wao, naona upo kazini Na kaz yako waifanya kwa weledi mkubwa kuepuka kutumbuliwa, mbowe kaingiaje hapa?
 
Vijana 46 nawe ukiwa mmoja wao, naona upo kazini Na kaz yako waifanya kwa weledi mkubwa kuepuka kutumbuliwa, mbowe kaingiaje hapa?
Tafuteni katibu wa chama anayekubalika, atakayetoa mchango wa kukikuza chama, zile biashara za kumnenepesha ng'ombe wiki ya mnada ziliwapa matokeo mabaya, mkaishia kusema mmeibiwa kura. Mlitumia miaka nane kumkashifu mzee wa monduli halafu mkapanda jukwaani na kutaka kumsafisha mpaka asafishike ndani ya miezi mitatu kuelekea uchaguzi!!. Huo kama sio upimbi ni kitu gani?. Jipangeni, kama alivyosema Dr. Slaa CCM inatolewa kwenye uongozi wa nchi kwa kutegemea serious people na serious plans, nyinyi mkakurupuka mkaja kupewa za uso.
 
Uwezo wako wa kuelewa umeshindwa kuielewa sarcasm iliyotumika kwenye hayo maandishi, lakini wengine wengi tu wamenielewa.
Atae kuelewa ni wapuuzi wenzio lkn sio wazalendo, CCM mnaendelea kuwapo kwa sababu ya polisi, bila kusahau Na yule fisi wenu, mnachukiwa
 
Ni bora ukaenda ikulu kumshauri Magu kwamba alikuwa mbunifu mzuri wa lile wazo LA kushtukiza kwani limempatia umaarufu mkubwa sasa atafute njia nyingine, tumeshamshtukia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…