Kiburi hutangulia maangamivu, Magufuli jitafakari!

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Ndugu zangu nimeona nianze kwa kuweka mstari huu wa Biblia kwa kuwa Magufuli anamweshimu Mungu na kwa kinywa chake amekuwa akikiri kuwa msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Mimi pia nimependa niendelee kuwa mpenzi wa Mungu kwa kumwambia Magufuli ukweli unaotoana na neno la Mungu.

Mara zote Magufuli amekuwa akitaka sana maombi ya Watanzani bila kujali itikadi na imani zao, huku akijua wazi ndio waliomuweka hapo alipo kwa ajili ya kuwatumikia. Kwa bahati mbaya au kukusudia Magufuli ameanza taratibu kujivika moyo wa kiburi kiasi cha kusahau kuwa aliwekwa na watanzania ili awatumikie wala hajajiweka wenyewe. Ndio maana nikaanza na neo hili la
Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko."

Mithali 16:18

Ni jambo la kusikitisha sana kuona mtu aliyechaguliwa na wananchi kwa lengo la kuwatumikia akiongea lugha la kiburi kama zile alizoongea siku ya kuweka jiwe la msingi pale Ubungo.

Mimi sikushauriwa na mtu kuchukua fomu kugombea Urais kwa hiyo siwezi kushauri cha kufanya, kwahiyo mimi ndie ninayejua nimuweke wapi mtu yeyote siwezi kupangiwa na yeyote. Hii ni lugha ya mtu mwenye kiburi ambaye amefika kiwango cha mfalme Nebukadneza wa Babylon aliyesema kuwa mimi ndie mfalme na mji huu niliujenga mimi, lakini Mungu alimpeleka porini akawa kama mnyama hadi pale aliponyenyekea tena baada ya miaka saba.

Lugha aliongea Magufuli ni ya kiburi maana kuna watu ambao wanalipwa kodi ya wananchi kwa ajili ya kumshauri, pia kuna viongozi wa kiroho wachungaji na mashehe ambao wanamshauri, wapo Marais wastaafu ambao pia wanatakiwa wamshauri, kwa maneno yake hayo amedhihirisha hawezi kukubali ushauri wa makundi yote haya kwa kuwa yeye ni zaidi ya raia wote wa Tanzania na ana akili kuliko watu wote. Hakika hiki ni kiburi ambacho Mungu hapendi kiongozi yeyote kuwa nacho.

Magufuli hahakisi tena moyo wa unyenyekevu aliowaonyesha watanzania wakati wa kampeni, amekuwa na lugha zenye viashirio vya kiburi kama hizi. Serikali ya Magufuli, Tanzania ya Magufuli, nataka niinyooshe nchi maana imevurugwa sana kila kitu kilikuwa hewa tu.

Jambo lingine la kushangaza amekuwa mtu ambaye hataki kuheshimu katiba ya nchi ambayo aliapa kuilinda, mfano kuzuia mikutano ya kisiasa wakati katiba imeiruhusu ni kiburi kibaya sana kwenda kinyume na katiba.

Pia amekuwa mtu wa double standards kuna watu wamefukuzwa kazi ambao walibakiza mwaka mmoja kustaafu kwa kosa la kufoji vyeti, leo watu wanapiga kelele kwa kijana wake kukosa vyeti vya form four amesema achape kazi tu wala asiwasikilize. Juzijuzi Mwakyembe kafanya kosa la kuwataka watanzania wasiokuwa na vyeti vya kuzaliwa wasifunge ndoa kesho yake alikuja na tamko la kufuta kauli hiyo, ila la Makonda kuvamia ofisi za clouds na askari wenye bunduki ameona ni umbea wa mitandaoni.

Amekuwa mtu wa kutumia kauli kali za kutaka vyombo vya dola kutumia nguvu kwa raia, kiasi cha kutamani yeye angekuwa IGP

Magufuli jitafakari bado rehema za Mungu zipo ila kama hutaki Mungu hadhihakiwi.
 
kweli kabisa mkuu.

tupitie mafundisho ya maandiko matakatifu yanayotoa maonyo kuhusu kiburi.


katika Isaya 14:12-15, maandiko yanatukumbusha kuwa shetani alitupwa kutoka mbinguni kwa sababu ya kiburi......

12 “Lo! Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni,+ ewe mwenye kung’aa, mwana wa mapambazuko! Jinsi ulivyokatwa ukaangushwa kwenye dunia,+ wewe uliyekuwa ukiyaondolea mataifa uwezo!+ 13 Kwa habari yako, wewe umesema moyoni mwako, ‘Nitaenda juu mbinguni.+ Nitakiinua kiti changu cha ufalme+ juu ya nyota+ za Mungu, nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano,+ katika sehemu za mbali zaidi za kaskazini.+ 14 Nitaenda juu ya mahali palipo juu pa mawingu;+ mimi nitajifananisha na Aliye Juu Zaidi.’+ 15 Hata hivyo, utashushwa chini mpaka katika Kaburi,*+ katika sehemu za mbali zaidi za shimo.

maandiko yanaendelea kutufundisha kuhusu upendeleo na kiburi pale 1 Kor 4:6-7.....

6 Basi, akina ndugu, mambo haya nimeyahamisha ili kuyatumia juu yangu mwenyewe na Apolo+ kwa faida yenu, ili katika hali yetu mjifunze kanuni: “Msipite mambo yaliyoandikwa,”+ ili msijivune+ mtu mmoja-mmoja kwa kumpendelea mtu mmoja juu ya mwingine.+ 7 Kwa maana ni nani anayekufanya wewe kuwa tofauti+ na mwingine? Kwa kweli, una nini ambacho hukupokea?+ Basi, ikiwa kwa kweli ulikipokea,+ kwa nini unajisifu+ kana kwamba hukukipokea?
 
Katika hili sijafilikili kuna kitu kama hicho Hii vita wengi tunaangalia kwa juu juu kwa ndugu huyu asingeacha kuchukua hatua ila anajua kuna nguvu ipi nyuma ya haya ndio maana kasema nafikili wamenielewa wewe chapa kazi, kundi hilo linataka kutumia udhaifu huo kumpoteza ila la Cheti limegoma, la uvamizi limezaliwa, kuna jingine lanakuja ndipo ukweli utawekwa hadharani
 
Nimekuelewa mleta mada ila kumbuka kwamba,
ili unabii utimie basi ni lazima viashiria (unabii huambatana na viashiria
ambavyo aliyepewa unabii huoneshwa kuwa vitatimia kabla ya unabii kamili kutimia) vitimie kwanza.
 
Hilo lingine ni lipi mkuu?
 
Hilo lingine ni lipi mkuu?
Jipe mda katika siasa kila kipindi kuna janga Lake watu wamesahau tulikuwa tunapigwa sana na wazee wa dili na siasa ya wakati huo ilipewa jina ufisadi, na watu wakakuza chama kwa neno pambana na ufisadi Leo napo limezaliwa jipya dikiteta lakini bado Kiki yake watu hawajaielewa vizuri, ila linawezekana ndio litakalo beba siasa ya sasa kwenda 2020
 


Asante sana kwa kuongeza hayo maandiko Mungu akubariki
 


Interesting..you sound genuinely knowledgeable.
 


Kwa kweli sina comments zozote kuhusu hiyo vita yao ila kiburi anachokionyesha kwa Watanzania, hata hivyo huwezi kufanya makosa au kuvunja sheria kwa sababu ya wewe kutendewa kosa.
 
Umenena vyema mkuu. Hekima imejaa tele kwenye maneno yako.
 
Nimekuelewa mleta mada ila kumbuka kwamba,
ili unabii utimie basi ni lazima viashiria (unabii huambatana na viashiria
ambavyo aliyepewa unabii huoneshwa kuwa vitatimia kabla ya unabii kamili kutimia) vitimie kwanza.


Sijatoa unabii ila nimefuata kanunia za Biblia au maandiko yasemavyo kwamba kiburi hutangulia maangamivu Mithali 16:18
Hivi kama ni viashiria wewe hujaona lugha za kiburi kama alivyofanya Nebukadneza?
 
Aaahahaaja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…