Kiama cha bomoabomoa Kibaha maili moja ni tar 23 January

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,807
730,152
Zimebakia siku chache sana kabla matingatinga ya serikali kuingia ndani ya mji mdogo wa Kibaha maili moja kubomoa na kusafisha eneo lote tayari kwa ujenzi na uwekezaji wa kisasa ikiwemo mahoteli na majumba makubwa ya masoko stendi nk.

Watu wameshalipwa fidia na ubomoaji ulikuwa ufanyike tangu tarehe 23 November 2016 lakini ulichelewa kutokana na matatizo ya hapa na pale ambapo sasa yametatuliwa na maandalizi yote yameshakamilika na ubomoaji wa hiari kunusuru vinavyoweza kunusurika piga picha sasa ya maili moja kama kumbukumbu kwakuwa hutakaa uione Kibaha uliyoizoea.
 
ilivyo anza mbezi mwisho ingeunga mpaka kibaha.ingekaa poa
 


Kiama chako?

Maendeleo mnaita kiama, hakika manyumbu hamsadifiki.
 
Kwanini unaita kiama au ubomoaji huo haukuzingatia taratibu?
 
Mshana neno kiama sio zuri kwani hamna hata mtu atayekufa wala kupata jakamoyo kwa kuwa watu wote wameshalipwa fidia. Linalofanyika hapo ni jema sana maana Kibaha ilikuwa mailimoja ilikuwa imechoka sana utadhani stendi za mikoani kumbe ni km 30 toka Ikulu. Mie ni mzawa wa Kibaha naunga mkono huo mpango
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…