Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,180
- 1,756
Salaam wakuu.
"Nendeni mkabuni vyanzo vipya vya mapato"hiyo ndio amri ya bi mkubwa aliyoitoa kwa wasaidizi wake ambayo sasa inaelekea kumgombanisha na wananchi wake.
Binafsi nashindwa kuelewa ubaya wa hii kauli ya Mama ulipo. Mama ni mswahili na ninahakika anakifahamu vyema kiswahili na alichoagiza alimaanisha.
Aliwaagiza wasaidizi wake waje wabuni vyanzo vipya vya mapato lakini badala yake wao wamekuja kubuni kodi mpya kwenye vyanzo vya zamani. Je, hivyo ndivyo mama alivyoagiza!?
Ni dhahiri kwamba mama alijua vyanzo vyote vya mapato vya zamani tayari vinautaratibu wake wa kuchangia maendeleo ya taifa ndio maana ya kuwaagiza waje wabuni vyanzo vingine vya mapato ya Serikali katika maeneo ambayo bado hayachangii pato la taifa moja kwa moja.
Kwa mfano mafundi,madereva na maeneo mengine ambayo hayaja rasimishwa ndio waliotakiwa waje wayapangie utaratibu utakaowezesha kulipa kodi na sio kwenye vyanzo vile vya zamani ambavyo tayari kuna kodi chungu tele mpaka wao wenyewe wanakosa majina ya kuzipa na sasa wanaziita kodi za kujitolea. Kujitolea gani huku kwa lazima!?
Sitoona ajabu hata leo hii Mama akiamrisha kufutwa kwa tozo mpya zilizoanzishwa kwenye miamala ya simu kwasababu sicho alichoamrisha. Ni aibu kuona hadi leo hii kuna viongozi wakubwa serikalini hawakielewi Kiswahili mpaka wafafanuliwe.