Katuni za Gado: Uchaguzi wa Zanzibar

toka mwaka 1992 kama sikosei akichorea gazeti la daily nation

Okay, sasa kwa mtu aliyezaliwa miaka ya 1986 (ina maana mwenye 30yrs) na kuendelea unadhani atamfahamu jamaa?

Especially kama siyo mfuatiliaji wa magazeti hayo ya Kenya, kwa sababu kwanza magazeti yenyewe hayauzwi kwenye vijiwe vyetu hivi.

Kwa hiyo watu wasiwashangae watu ambao hawamjui GADO, watoe elimu tu kwa staha juu ya GADO ni nani.

Halafu pia kibongo bongo unakuta mtu unaweza kupenda katuni bila hata kujua ni nani mchoraji.
 
Your right ila nadhani alifanya kidogo STANDARD kabla ya kujoin NATION

Kama aliondoka miaka hiyo inabidi uwe mfuatiliaji sana kumfahamu jamaa hasa ukiwa under 30 au umekuja mjini miaka ya karibuni, maana wengine huko kwetu kuna magazeti hata hayafiki kabisa.

Thanks kwa huu utandawazi, hii leo kusoma taarifa au katuni siyo lazima ununue gazeti.

Nakumbuka aliwahi kuwachora kina Juma Nkamia wanamkojolea Madam Spika, jamaa ni very controversial, achana na hawa kina Kipanya wanauma na kupulizia.
 
Kweli huyu ni zaidi ya msanii...Picha hii ukiamua kuijadili, hakika unaweza kuandika kitabu kabisa. Mfano, Tizama nyuso za wale mashabiki nje ya ulingo kwa ukaribu zaidi. Tizama body morphology za mabondia ( wa fisiem na wa cuf ) , n.k.
Fantastic kwa kweli.
A picture or rather Gado's cartoons are worth a thousand words ,more they are entertaining.
 
Huyu Gado ni mtanzania?,kazi zake huziona kwenye magazeti ya kenya ya kiingereza
 
Tanzania ina wachora katuni wengi,tatizo huacha kuchora kutokana na media print nyingi kutokuwa na uwezo wa kuwalipa malipo mazuri
 
Inatia moyo kwa akina nathan (mtu kwao),masoud (kipanya)king kinya nao kazi zao kuvuka mipaka,sanaa hii inarudi kwenye enzi zake.
 
JKCartoon.jpg

Hii ndio iliyosababisha Gazeti la East African kufungiwa
huyo ni JK wa msoga? Kibonzo sijaelewa warembo wanamlisha JK?
 
Inatia moyo kwa akina nathan (mtu kwao),masoud (kipanya)king kinya nao kazi zao kuvuka mipaka,sanaa hii inarudi kwenye enzi zake.
 
Nilizipenda katuni za GADO hasa zile za masuala ya kisiasa,ujumbe unalenga kisawasawa
 
Napenda sana katuni, lakini huyu msanii Gado sijawahi kumsikia
Huyu ni gwiji wa katuni ni Mnyakyusa aliehamia Kenya,alikuwa gazeti la Daily Nation la Kenya kwa miaka mingi wao hudai ndio gazeti kubwa Afrika Mashariki,huyu amechora vikaragosi vinavyowahusu wanasiasa hasa wa Kenya akiwemo Mzee Moi raisi mstaafu wa Kenya ambaye alichorwa hadi akawa mwenyewe anapenda hizo katuni kuliko kuchukia,akaja Kibaki nae kachorwa wee akiwa na gongo la kuchezea gofu ,hata Raila kachorwa sana akiwa na kofia yake,Uhuru na Ruto walipoona wanazidi kuchorwa wakailazimisha kampuni ya Daily Nation kumuondoa kazini,hapa Tanzania anakumbukwa kwa kuchora katuni mbili kwanza ile ya wanasiasa kumlamba viatu mkulu na pia ile kayuni ya kuwafuatilia mafisadi.Kilichomuuzi Uhuru na Ruto ni kuwa Ruto alichorwa anafanyiwa massages na vimwana kwenye ndege ya kukodi,ikiwa ni kuonyesha wakubwa wanavyofuja mali.Hawa nadhani wapo wawili ambao ni wanandugu wachoraji,mmoja wa wazazi wao alikuwa mwalimu shule ya msingi Mlimani Chuo Kikuu
 
Hii imetulia mkuu, safi sana
 
Kilichomuuzi Uhuru na Ruto ni kuwa Ruto alichorwa anafanyiwa massages na vimwana kwenye ndege ya kukodi,ikiwa ni kuonyesha wakubwa wanavyofuja mali.Hawa nadhani wapo wawili ambao ni wanandugu wachoraji,mmoja wa wazazi wao alikuwa mwalimu shule ya msingi Mlimani Chuo Kikuu
GADO-CARTOON.jpg
 
sasa mbona inaonyesha cuf , amefungwa kamba wakati amesusia mwenyewe , nadhani alihitaji kuongeza ubunifu zaidi ya hapo ili kukidhi halihalisi ya hapo
kama vile kumuonyesha akiwa hotelini anaangalia TV au akiwa hospitali anatibiwa!
 
Back
Top Bottom