MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Kifungu cha 5 (3) cha sheria ya Tawala za Mikoa Namba 19 ya mwaka 1997 kinaelezea wajibu wa Mkuu wa Mkoa kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuwa ni kuziwezesha na kuzijengea mazingira ya kutekeleza majukumu yao kisheria.Zipi hizo sheria ambazo mkuu wa mkoa anaweza kuzikata?
Kama huwezi kuziweka hapa naomba unidirect hata kifungu gani tu nikasome inayomruhusu kufanya hivyo
Dhana hii ya uhuru wa mamlaka za Serikali za Mitaa inaegemea katika sharti kuwa, mamlaka hizo zitakuwa zinajiendesha kisheria. Lakini pale itakapobainika kuwa sheria haifuatwi, basi uhuru huo hautalindwa, bali Serikali Kuu ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Mkoa itaingilia kati kuona kuwa sheria zinatekelezwa.
Msingi huu ndio uliosababisha sheria kumpa Mkuu wa Mkoa uwezo wa kuagiza au kuwaruhusu maafisa wa Serikali Kuu kuchunguza nyaraka pamoja na kumbukumbu nyingine za fedha za mamlaka za Serikali za Mitaa. Lengo ni kutaka kugundua endapo kuna ukiukwaji wa sheria au kanuni za fedha.
Hatua hizi ni kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha sheria ya fedha za Serikali za Mitaa namba 9 ya mwaka 1982. Kifungu cha 78A cha sheria namba 8 ya mwaka 1982, kinampa Mkuu wa Mkoa madaraka ya kusimamia utekelezaji wa sheria za Mamlaka za Serikali (Mamlaka za Miji), ikiwa ni pamoja na kuchunguza uhalali wa vitendo na maamuzi ya mamlaka hizo na kumuarifu Waziri ikiwa kuna ulazima wa kuingilia kati endapo vitendo na maamuzi vinakiuka misingi ya sheria.