Kati ya Mkapa na Magufuli nani anapaswa kufanyiwa kumbukizi?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,385
38,657
Kwa Bahati wengine mpaka sasa kwa sehemu tumebahatika kuona Marais wote baada ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kung'atuka madarakani. Wengine tumepata bahati kufanya uchaguzi kuanzia enzi Mwinyi akiwa Madarakani.

Kati ya Marais walioingia madarakani baada ya Mwalimu Kung'atuka yaani Ally Hassan Mwinyi, Benjamin William Mkapa, Jakaya Mrisho Kikwete, John Pombe Magufuli, wawili kati yao wameshatangulia mbele ya haki. Benjamin Mkapa na John Pombe Magufuli.

Mkapa na Magufuli kila mmoja waliingia madarakani nchi ikiwa kwenye hitaji la kufanya mabadiliko ya kijamii na kiuchumi. Mkapa alikuwa ni Rais wa Kwanza kuchaguliwa baada ya mfumo wa vyama vingi kurejeshwa mwaka 1995. Na Mkapa aliingia wakati nchi yetu inatoka kwenye mfumo wa njia kuu za uchumi kumilikiwa na dola kwenda kumilikiwa na sekta binafsi.

Magufuli aliingia madarakani wakati Tanzania ikwa na hitaji kubwa la kufanya mabadiliko ya udhibiti wa matumizi ya madarakani ya umma kwa maslahi binafsi. Magufuli aliingia wakati ilikuwa inaonekana kama vile ukiwa na madaraka unakuwa na nguvu isiyohojika na unaweza kutumia madaraka ya umma kujitajirisha.

Kwa mitazamo mbali mbali inaonekana kama kuna shinikizo la kuweka kumbukuzi kwao kwa siku za vifo vyao iwe ni sikuk rasmi ya kitaifa. Jee wote wawili wawekewe kumbukuzi ama ni mmoja tu kati yao ndiye anayefaa kuwekewa kumbukizi?
 
Ukileta mambo ya kumbukizi basi kila raisi bila ubaguzi itatakiwa afanyiwe kumbukizi kwa mambo aliyoyafanya, mfano huwezi kumuacha Raisi Ally Mwinyi kwa kututoa katika lindi la ufukara na umaskini pale alipochukua kijiti kutoka kwa baba wa taifa ambaye aling'atuka (alijiuzulu madaraka) baada ya kuona nchi immemshinda, Mwinyi kipindi anaikomboa nchi katika dhiki na ufukara alipendwa mno na umma wa Watz wakati huo, Kikwete naye huwezi kumuacha kwani anayo yake mazuri aliyoyafanya, kaleta uhuru wa kidemokrasia nk.

Kumbukizi isiwe ya kibaguzi.
 
Hao wameachwa kwa kuwa bado wapo hai kwa ivo huwezi kuzungumzia mambo ya kumbukizi!!
 
Back
Top Bottom