KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 65
- 128
Kupitia jukwaa hili, mimi mwananchi wa Kata ya Kabondo Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu.
Kwa niaba ya Wananchi wa kata hii, naomba kuleta malalamiko yetu kwa viongozi hasa Mheshimiwa Rais na Waziri wa TAMISEMI.
Mwaka 2023 sisi Wananchi na Viongozi wa kata, tulikaa katika mkutano wa hadhara, kujadili changamoto ya elimu kwa watoto wetu hasa wa sekondari.
Changamoto hiyo ni Watoto wetu kutembea kila siku kilometa takribani 20, kwenda Shule Sekondari Mwamishali, iliyopo kata jirani ya Mwamishali.
Mateso ya Watoto, yalitulazimu kama Wananchi wa kata hii kwenye mkutano huo, kuamua kuanza ujenzi wa shule ya sekondari kwenye kata yetu.
Kwenye huo mkutano tulipiga hesabu ya kaya zenye uwezo wa kuchangia kiasi cha Sh. 50,000 kila kaya, ambapo takribani kaya 584 zilitakiwa kuchangia kiasi hicho cha mchango.
Baada ya kupitisha mchango huo, tuliunda kamati ya ujenzi wa shule hiyo ambayo ilikuwa chini ya Mwenyekiti wake Diwani wa Kata yetu na Mtendaji wa Kata.
Kamati hiyo ambayo ndani yake kulikuwepo na Watendaji wa Vijiji na Wenyeviti, ilianza zoezi la kukusanya michango kutoka kwa kaya hizo 548, ambapo zoezi la kuchangisha lilifanikiwa asilimia 100.
Katika mkutano mwingine, kamati ilitutangazia kuwa imekusanya kiasi cha Shilingi Milioni 30 kutoka kwenye hizo kaya na pesa zote kamati ikatueleza imepelekwa benki na ujenzi utaanza mara moja.
Jambo la kushangaza tangu Januari ambapo michango hiyo ilikusanywa, mpaka leo hakuna ujenzi wowote ambao umefanyika katika eneo ambalo liliteuliwa shule hiyo ujengwe.
Shule ya haijajengwa, juzikati kwenye mkutano wa hadhara wananchi tulihoji, viongozi wakaanza kutupiana mpira, tuliambiwa kuwa kwenye akaunti imebaki Shilingi laki 5 tu.
Wajumbe wa Kamati hiyo waliwataka Diwani wa Kata yetu na Mtendaji wa Kata, kuwa wao ndiyo walishika hela zote na kuzipeleka Benki, lakini baadaye zilizokutwa benki ni shilingi laki tano.
Uchunguzi ambao tumefanya imebainika ni kweli Diwani na Mtendaji wa Kata wamekula michango yetu, tumewauliza wajumbe waliokuwa kwenye hiyo kamati wametwambia ukweli wa jambo.
Wajumbe wanasema wakati wanakusanya pesa zote walikuwa wakipeleka kwa viongozi hao, kwa madai kuwa walitaka wapewe hizo hela kisha wao ndiyo watapeleka benki.