Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,713
- 13,464
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza Bungeli, leo Aprili 25, 2024 ametoa taarifa ya kuhusu mwendendo wa Matuko ya hali ya hewa, athari zake na hatua zilizochukuliwa na Serikali.
Amesema mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha kuongezeka kwa mvua katika maeno mbalimbali Duniani ikiwemo Tanzania. Taarifa za tahmini kutoka TMA zimeendelea kuonesha mwelekeo wa kuongezeka kwa kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa, ikiwemo matukio ya mvua kubwa na upepo Mkali.
Tathmini ya mvua kwa misimu yote inaonesha maeneo mengi yamepata mvua za juu ya wastani ikiambatana na matukio ya hali mbaya ya hewa hususan mvua kubwa na mafuriko.
Ongezeko la joto duniani limesababisha uwepo wa El Nino ambayo imesababisha mvua kubwa zilizosababisha mafuriko nchini kuanzia Mwezi Oktoba-Desemba 2023. Ongezeko hilo la mvua limeshuhudiwa pia kuanzia mwezi Januari-Aprili 2024 na utabili wa TMA unaonesha mvua za masika zitaendelea hadi Mei 2024.
Mvua kubwa za El nino zinazoendelea zikiambatana na upepo mkali, mafuriko na maporomoko ya udongo maeneo mbalimbali nchini zimesababisha athari kubwa ikiwemo vifo, uharinifu wa makazi na mazao mali za wananchi, miundombinu na kutokana na athari hizo zaidi ya kaya 51,000 za watu 200,000 waliathirika ambapo watu 155 walipoteza maisha, 236 walijeruhiwa na nyumba zaidi ya 10,000 ziliathiriwa kwa kiwango tofauti.