Kumekwepo taarifa na kauli mbalimbali kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii yakishadadiwa na taasisi zinazojiita asasi za kiraia zikikashifu waalimu kuwa ndio wanaongoza kwa kupachika mimba kwa wanafunzi. Kama ni kweli walimu wamekuwa watovu Wa nidhamu kiasi hicho na wamekiuka maadili ya utumishi Wa kwa kiwango hicho ni lazima kama wadau Wa elimu tuhoji uwajibikaji Wa mamlaka zifuatazo; (a). Mamlaka ya nidhamu kwa walimu (b). Vyuo vikuu na vyuo vya ualimu wanakoandaliwa hawa walimu. Pamoja na mamlaka hizo kama wadau Wa elimu bora ni lazima pia tujiulize kuwa ni kweli walimu wrote wakiume ni wahusika au huko ni kudhalilisha taaluma ya ualimu? Kama sio kwa nini maneno ya jumla yanatumiwa sana? Pia ni kweli hakuna walimu Wa kike wanaofanya mapenzi na wanafunzi Wa kiume hasa ktk shule za sekondari? Kama ni kweli mbona wao hawasemwi au wanafunzi wa kiume wa hawana watetezi katka asasi hizo za kiraia?