Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita limevamiwa usiku wa kuamkia February, 26 2023

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,261
Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita limevamiwa usiku wa kuamkia leo ambapo watu waliovamia wamevunja mlango na kuingia ndani kisha kuharibu vitu vitakatifu vikiwemo mavazi ya misa na kuvunja misalaba.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP Berthaneema Mlayi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wawili wanashikiliwa na upepelezi wa tukio hilo unaendelea.

1677414935444.jpg
1677414932005.jpg
1677414929066.jpg
1677414925844.jpg
1677414922524.jpg
1677414918507.jpg
1677414914290.jpg

=====
Askofu Flavian Kassala
Wapendwa, nawatangazia kuwa jimbo katoliki Geita tumepatwa mkasa mkubwa ambapo mtu mmoja amevamia kanisa kuu na kuvunja mlango mkuu na kisha kuanza kuharibu vitu vitakatifu, vikiwemo Tabernakulo na Ekaristi. Ni kufuru ya matakatifu.

Kavunja misalaba na mavazi ya misa. Nawaombeni mtumie vyombo vyenu vya habari ktk redio na television muupashe habari umma kuwa kitendo cha kudhalilisha imani yetu kimefanyika na tunakikemea na kukilaumu kwani kukaa kimya ni kama kuonesha hatuthamini imani yetu. Kwa wenye redio au tv, atakayehitaji "Audio" ya baba askofu, nitamtumia ili airushe na tuunganishe nguvu ya vyombo vya habari vya kanisa kukemea udhalimu dhidi ya imani katoliki.

Matukio ya uharibifu wa kanisa kuu la kiaskofu jimbo la Geita usiku wa kuamkia Jumapili trh 26 February 2023. Tukio limeripotiwa saa nane usiku. Uharibifu na kufuru zilizotokea ni kubwa sana. Mhusika amekamatwa. Mungu azidi kutulinda.

======

Polisi watoa tamko kufuatia tukio la kuvunjwa kwa kanisa

Zaidi soma:
Polisi yasema aliyevunja Kanisa Katoliki na kuharibu Vitu Geita ni Muumini aliyekuwa amelewa!
 
Kanisa Kuu la Kiaskofu Jimbo Katoliki la Geita limevamiwa usiku wa kuamkia leo ambapo watu waliovamia wamevunja mlango na kuingia ndani kisha kuharibu vitu vitakatifu vikiwemo mavazi ya misa na kuvunja misalaba.

Screenshot_20230226-160144_Twitter.jpg

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP Berthaneema Mlayi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wawili wanashikiliwa na upepelezi wa tukio hilo unaendelea.

Chanzo: EATV
 
Iwekwe wazi bila kufichwafichwa kwa hofu ya uchochezi.

Hao wahalifu si wakristo, mkristo hawawezi kuingia kanisa lolote na kuharibu vilivyomo humo.

Pia hao si wapani, hao wahalifu itakuwa ni wale masheitwaan maana wao huwa hawana hofu kuingia nyumba za ibada za wengine na kufanya uharibifu
 
Back
Top Bottom