Kampuni ya DSTV Tanzania imefilisika?

Wadau, amani iwe kwenu.

Nikiwa katika safari zangu Jijini Dar es Salaam nilikofika kwa shughuli za kibiashara, nimepita maeneo ya Leaders Club na kukuta makontena ya kampuni ya DSTV pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa wametapakaa kila kona. Nimebahatika kuongea na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo na kunithibitishia kuwa kampuni hiyo imefukuzwa kwenye jengo walilopanga Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jirani na Kanisa la St Peters baada ya kushindwa kulipa pango.

Nimejiuliza sana. Inakuwaje kampuni kubwa kama DSTV ishindwe kumiliki mjengo wake wenyewe? Au wapo mguu ndani mguu nje? Nashindwa pia kuelewa sababu za wao kushindwa kulipa pango la nyumba ilhali ina wateja kila kona ya nchi hii.


e342ec53482a2e6f0e69c8bc6559c29d.jpg
 
Waliwatumia meseji subscribers wao kuwajulisha kwamba wamehama pale. Mpangaji anaweza ''kufukuzwa'' kwenye jengo la mmiliki kwa sababu nyingi, ikiwemo kushindwa kukubaliana kwenye bei ya pango, especially pale bei inapopandishwa.

But kiukweli wateja wamepungua kiasi. Ninawafahamu jamaa kadhaa ambao suddenly wamegundua kujiunga DSTV ni ''anasa'' na sasa wanacheza na Star Times tu.
Mkuu Star times kuna EPL?
 
hawaja firisika jaman muwe na taarifa rasmi hao wameamia maeneo ya kinondoni
 
Ungekuwa ni mteja wa DStv kama mimi ungeshajua kwa kupewa taarifa. Unadhani kila jambo ni la kuliandikia porojo tu. Hao wamehamisha ofisi tu na kuhamia kwingine. Yaani wewe kila jambo unalitungia porojo na kulileta humu hata bila ya kulijua kwa undani. Unasikitisha sana Mkuu Lizaboni. Halafu eti ndiwe unayetegemewa kujenga hoja!?? Bure kabisa!
 
Back
Top Bottom