Hebu tusaidie hizi kamati ziko ngapi na ofisi za binge Dar zina Kumbi ngapi? Itatua picha kama kuna umuhimu Wa kupata kumbi za Ziada au la!!
Ndugu Kifaurongo,
Kamati za sasa ni 18 katika Bunge la 11 na tofauti yake ni kamati moja tu, kwani katika Bunge la 10 kulikuwa na kamati 17. Naziweka hapa chini uzione (mzione):
Kamati za Bunge la 10 zilikuwa 17, ambazo ni hizi:
1. KAMATI YA KANUNI ZA BUNGE
2. KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE
3. KAMATI YA MASUALA YA UKIMWI
4. KAMATI YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
5. KAMATI YA BAJETI
6. KAMATI YA UCHUMI, VIWANDA NA BIASHARA
7. KAMATI YA ULINZI NA USALAMA
8. KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII
9. MAENDELEO YA JAMII
10. KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI
11. KAMATI YA MIUNDOMBINU
12. KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI
13. KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA
14. KAMATI YA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
15. KAMATI YA NISHATI NA MADINI
16. KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA
17. KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA
Kamati za Bunge la 11 zipo 18 kama ifuatavyo:
1. KAMATI YA UONGOZI
2. KAMATI YA KANUNI ZA BUNGE
3. KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE
4. KAMATI YA MASUALA YA UKIMWI
5. KAMATI YA BAJETI
6. KAMATI YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA
7. KAMATI YA KATIBA NA SHERIA
8. KAMATI YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA
9. KAMATI YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII
10. KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII
11. KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI
12. KAMATI YA MIUNDOMBINU
13. KAMATI YA NISHATI NA MADINI
14. KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA
15. KAMATI YA SHERIA NDOGO
16. KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI ZA MITAA (LAAC)
17. KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)
18. KAMATI YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA
NB: Hatujawahi kusikia katika Bunge la 10 kwamba vikao vya kamati hizo vimehamishwa (pengine mwenye kumbukumbu anisahihishe). Pamoja na hayo, hata kama kuhamishwa kwa vikao hivyo kumetokana na wingi wa kamati na uhaba wa kumbi za mikutano, lakini pale kwenye ofisi za Bunge hakuna hata kamati moja inayoendelea na vikao vyake ili kuhalalisha kwamba kamati nyingine zilizoko Kijitonyama zimeamua kufanya hivyo kukabiliana na uhaba huo.
Kama kuna sababu nyingine, iwe ni uhaba wa kumbi ama kufanya ukarabati (kama upo), nadhani ni uzembe wa uongozi kwa sababu ratiba inajulikana kuhusu shughuli za Bunge na kamati zake.
Ni suala muhimu zaidi kulijadili. Kama Rais alitumia Shs. 20,000 kwa maji na karanga katika kikao cha watendaji, nadhani tuliangalie hili pia, vinginevyo tunaweza kuwa tunamimina maji kwenye pakacha.
Ni mtazamo wangu wadau.