Kamanda wa Polisi Kinondoni: Sina taarifa ya kukamatwa kwa Gwajima

But also the gvt should be neat and transparent to every touching compared to this. Gvt is people, these people who leads others must be neat. Dola inaogopa ndoto za watu, mikutano.
 
Vipo Bugando bwana labda kama walividondosha pale ILULA njia panda hata hivyo Masanja msalimie Bundala Jirani yake Kashindye
Nashukuru sana mkuu Kiatu kipya,Bundala nilikuwa nae sio mda mrefu na ndiye aliyeniambia kuwa kulikuwa na faili pale ulipopasema wewe! Sitaki nirudi kupasema kwasababu huku kwetu ndio kwanza mvua imeanza Leo na njaaa haipo! Ila naogopa nikipelekwa Butimba wapwa zako watapata shida.

Ombi langu mkipitapita hapo kwa Igwee mwambieni tumemuelewa vizuri,na tumeelewa kuwa yeye ninani! Hata pale alipokataa kutupikia chakula alipokuwa njiani kuelekea kule kwa ndugu yetu Simiyu yetu bado tulimuelewa ila tulidhani anatania ila sasa tumeelewa kuwa amedhamilia.

Mwambieni Igwee pale Buzuruga ambapo wake zetu walikuwa wakipatia Riziki kwa kuchemsha michembe na matoborwa sasahivi pamekuwa pasafi ile mbaya,askari wa jiji hawana urafiki na watu.
Mkumbusheni kuwa alituahidi hata pale alipokuwa akitoka mapumzikoni kuwa wasitusumbue wapiga kura wake ila kwasasa wametuacha tukijipaka machozi yashukayo kwenye mashavu ya nyuso zetu Mara baada ya kuambulia virungu vya maafande city.

Mwambieni tunahuzunika kwa hofu ya kutokumwona tena akishuka na Bombardier yetu hapa kwasababu Chato international airport itakuwa tayari,ila mkumbusheni kuwa asitusahau,sisi ndio tuliopiga zile kura za maruhani hakika mwambieni bila sisi Mzee wa miaka mingi mwenye nywele nyeupe alikuwa ameshapita.

Naomba mkimkosa mwambieni hata Daudi afikishe Ujumbe huu.Aende hata kwa miguu Bashite tunamuamini anakimbia sana yule.

Hakika msalimieni sana Huyu Daudi Bashite,mwambieni tunampenda sana.

Niwatakie siku njema na yenye Furaha na amani.

Ni Mimi yule yule Masanja Nguku
Kijiji cha Koromije /Misungwi/Mwanza.
 
Hawa Wasukuma Makonda na Magufuli kwa kweli WANA AIBISHA KABILA LA WASUKUMA kwa 100% Ajabu ni kwamba wanapambana na Msukuma mwenzao GWAJIMA sijui wanamtaka nini hasa!!
Mimi nawapa angalizo tu kwamba Mungu hadhihakiwi na Mungu hamfichi Mnafiki. Magufuli na Makonda ni wana siasa na Viongozi wa Serikali lakini mwenzao ni MTUMISHI WA MUNGU. Hili lazima walijue.
Kwa Makonda na Magufuli kushindana na GWAJIMA ni kutaka kushindana na MUNGU. Sasa ngoja tuone mwishoo wake utakuwaje.Sijawahi kusikia au kusoma kwenye Biblia Takatifu mahali ambapo Mwanadamu alitaka kushindana na Mtumishi wa Mungu au Mungu mwenyewe na akashinda.
Kwa mtaji huu Magufuli na Makonda wanaupiga teke mchokoo na wao ndo watakao umia.
 
Serkali inatumia muda mwingi kupambana na vitu visvyokuwa na msingi wakt yapo mamb kibao
 
Kiongozi sampuli ya Gwajima atawatesa mno. Ukicheza na koki mbovu lazima ulowe tu. Gwajima anajua kuwa ni msafi na uovu wao anaujua wote mwisho wakichoka wataenda kupata kitubio kwake. Huwezi kusimamia haki ukiwa na mikono michafu. Kwa Gwajima ujue akitoka atamlipua mwingine tena.
Kweli hakosi matukio
 
hii serikali wanacomplicate maisha kwanini gwajima na daudi bashite wawasifanye proof mbele ya wanahabari atakae kuwa muongo wamuweke ndani
 
tatizo la polis wetu ni kutumiwa na wanasiasa badala ya kufuata sheria, taratibu za ukamataji wa raia...
 
Nashukuru sana mkuu Kiatu kipya,Bundala nilikuwa nae sio mda mrefu na ndiye aliyeniambia kuwa kulikuwa na faili pale ulipopasema wewe! Sitaki nirudi kupasema kwasababu huku kwetu ndio kwanza mvua imeanza Leo na njaaa haipo! Ila naogopa nikipelekwa Butimba wapwa zako watapata shida.

Ombi langu mkipitapita hapo kwa Igwee mwambieni tumemuelewa vizuri,na tumeelewa kuwa yeye ninani! Hata pale alipokataa kutupikia chakula alipokuwa njiani kuelekea kule kwa ndugu yetu Simiyu yetu bado tulimuelewa ila tulidhani anatania ila sasa tumeelewa kuwa amedhamilia.

Mwambieni Igwee pale Buzuruga ambapo wake zetu walikuwa wakipatia Riziki kwa kuchemsha michembe na matoborwa sasahivi pamekuwa pasafi ile mbaya,askari wa jiji hawana urafiki na watu.
Mkumbusheni kuwa alituahidi hata pale alipokuwa akitoka mapumzikoni kuwa wasitusumbue wapiga kura wake ila kwasasa wametuacha tukijipaka machozi yashukayo kwenye mashavu ya nyuso zetu Mara baada ya kuambulia virungu vya maafande city.

Mwambieni tunahuzunika kwa hofu ya kutokumwona tena akishuka na Bombardier yetu hapa kwasababu Chato international airport itakuwa tayari,ila mkumbusheni kuwa asitusahau,sisi ndio tuliopiga zile kura za maruhani hakika mwambieni bila sisi Mzee wa miaka mingi mwenye nywele nyeupe alikuwa ameshapita.

Naomba mkimkosa mwambieni hata Daudi afikishe Ujumbe huu.Aende hata kwa miguu Bashite tunamuamini anakimbia sana yule.

Hakika msalimieni sana Huyu Daudi Bashite,mwambieni tunampenda sana.

Niwatakie siku njema na yenye Furaha na amani.

Ni Mimi yule yule Masanja Nguku
Kijiji cha Koromije /Misungwi/Mwanza.
Kalimbwane mkuu nimechemka mno ama hakika kila jambo kina chanzo nitapita hata Nyanza shule ya msingi kupata uhakiki wa Bashite,ndio mjini umeng'aa afande wa city na lori lao rangi ya blue wanatisha mjini ni bora bwana samaki ila sio wao,najua amedhamilia kwa hakika juu ya shamba LA serikali tupambane kura zile sasa hazimsumbui kichwa nitapita pia national kwa wazazi wa mpango wa kando niwape salamu watafurahi sana kupata taarifa sahihi za Ingwe
 
Dar es Salaam. Wakili Peter Kibatala amesema polisi wamepiga picha nyumbani kwa Askofu wa Kanisa la Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima.

Kibatala ambaye ni wakili wa Askofu Gwajima amesema jana kuwa mbali na kupekuwa na kupiga picha kila kona walikwenda katika kanisa lake lililopo Ubungo.

“Waache wafanye yao na sisi tutafanya yetu kisheria. Kwani hatuwezi kuwazuia Polisi kufanya shughuli yao na baada ya kumaliza na sisi tutajua nini cha kufanya,” amesema Kibatala.

Msemaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, David Mngongolwa amesema Gwajima alikwenda jana kuripoti kama alivyoamriwa kufanya hivyo.

Mngongolwa amesema baada ya kuripoti askari walimchukua na kwenda naye nyumbani kwake wakakaa kwa dakika zisizozidi sita na kuondoka naye.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda amesema hana taarifa za kukamatwa kwa Gwajima kwa maelezo kuwa alikuwa katika kikao.

“Naomba uumtafute Sirro (Simoni-Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Gwajima awali alishikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam hivyo ni vema ukamtafuta kamishna,” amesema Kamanda Kaganda.

Source : mwananchi
Tanzania ya viwandaaaa hiyooooo
 
*TAARIFA*

Karibu kwenye Ibada ya Jumapili 05/03/2017 katika Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo, Dar es Salaam. Askofu Dr Josephat Gwajima atakuwepo akifundisha na kuwaombea wenye shida na matatizo mbalimbali. Kama ilivyo kawaida miujiza na mambo mengine makubwa yatafanyika.

Kanisa liko ubungo karibia na jengo la TANESCO. Ibada itaanza asubuhi saa mbili kamili na Pia itarushwa live kwenye vituo vifuatavyo:

Rudisha Radio: www.mixlr.com/rudisha-radio

Na YouTube Channel: www.youtube.com/user/ufufuonauzima

Mtaarifu na mwenzako.
 
Back
Top Bottom