Kamanda Sirro: Watu 7 akiwemo Abduli Kambaya wakamatwa kwa Vurugu za CUF Mabibo

View attachment 502199
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Profesa Lipumba, Abdul Kambaya

Dar es Salaam.
Watu saba wamekamatwa kwa kusababisha vurugu katika mkutano wa CUF uliofanyika Mabibo hivi karibuni, akiwamo mfuasi wa Profesa Ibrahim Lipumba, Abdul Kambaya.

Kambaya ni Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Lipumba.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema upelelezi wao umekamilika na jalada la mashtaka hayo lipo kwa wakili wa serikali.

Sirro ameyasema hayo leo Ijumaa katika mkutano na waandishi wa habari.

Chanzo: Mwananchi
Mwananchi imenifurahisha kwa kumtambua Kambaya kama mkurugenzi wa mawasiliano wa Prof Lipumba..
 
ok
View attachment 502199
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Profesa Lipumba, Abdul Kambaya

Dar es Salaam.
Watu saba wamekamatwa kwa kusababisha vurugu katika mkutano wa CUF uliofanyika Mabibo hivi karibuni, akiwamo mfuasi wa Profesa Ibrahim Lipumba, Abdul Kambaya.

Kambaya ni Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Lipumba.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema upelelezi wao umekamilika na jalada la mashtaka hayo lipo kwa wakili wa serikali.

Sirro ameyasema hayo leo Ijumaa katika mkutano na waandishi wa habari.

Chanzo: Mwananchi
 
Bila Ibrahim Haruna Lipumba kukamatwa na kufunguliwa mashtaka, nakiri kwa herufi kubwa "UPANDE WA UPELELEZI UMEAMUA KUFICHA UKWELI, NA KUJIWEKA UPANDE WA IBRAHIM".
 
Siyo suala la kukamatwa bali na tuone sheria ikichukua mkondo wake sambamba
 
Hii ni muvi kama ya jambazi kuvua viatu na kuana kuiba, hipo mahususi kudhibiti wanachama wa cuf halali kwenda buruni jumapili,
Huyu kamanda yeye anatekeleza maagizo kutoka kwa muvi directors.
 
Kwa mambo yanavyoenda, hiyo inaweza kuwa danganya toto. Na bila shaka intelijensia itakuwa imenusa jinsi wananchi walivyokasirishwa na ule uvamizi.

Nimesikiliza RFA leo alfajiri ndio nikagundua hii kitu imekera sana watu, na wakubwa lazima wamelijua hilo. Sarakasi muhimu.

Wanataka kuepusha watu wanapovamiwa wasijitetee .
 
Back
Top Bottom