Kamanda Sirro: Nimeona watu kwenye mitandao wakisema kwamba Polisi wamekuwa kama TRA

Kamanda Sirro issue sio watu kutenda kosa. kwanza kukosa ni hulka ya binadamu yeyote na ndio maana tunaombana msamaha na kwenye dini zote kubwa kuna kipindi cha toba.

Kuna wakati mtu ameamka asubuhi kachelewa kuamka kajisahau kukagua gari yake kama road license ama bima imeisha jana yake. Kwa hiyo anakutana na askari wa barabarani badala ya kumpa onyo na either kumwambia apaki pembeni anunue bima ndio akuruhusu hapo hapo anaandikiwa fine. Pasipokujua ile fine bado haimwondolei huyu mmiliki wa gari hatari atakayoipata ikiwa atapata ajali.

Hivyo badala ya kuwa washauri watoa maelekezo mnakuwa watoza ushuru
 
Police pigeni kz, haijalishi vikosa vidogo vidogo wala makubwa. Piga fine!!
b9def6d6f53d564635c79628c8034403.jpg

Unahaki kabisa kuandika hivyo.
 
Jana amesikika kamanda wa kanda maalum DSM akijibu mapigo baada ya taasisi anayoisimamia kushutumiwa kujigeuza na kuwa tawi la TRA.

Amesikika kwa hoja dhaifu akijibu tuhuma hizo lakini picha ya mapato aliyokusanya kwa kipindi cha kama wiki moja kinaonesha kuwa mapato ya Polisi-TRA yameshuka kwa kasi kubwa kutoka kwenye milioni mia nane na ushee mpaka milioni mia sita na ushee!

Nawashukuru JF ana kuwapongeza wale wote walioshiriki kupinga vikali dhuluma zinazofanywa na polisi wa usalama wa barabarani za kushurutisha madereva walipe faini hata kwa vikosa vidogo vidogo.
TRA Ruangwa na Polisi Wanalazimisha Kukusanya Mapato kwa Kamata Kamata

Dhana ya polisi kuwa wakusanya mapato

======

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro April 5, 2017 ameeleza sababu za Jeshi hilo kufananishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ katika utendaji wao wa kazi hasa katika ukusanyaji wa mapato.

Kamanda Sirro ametoa ufafanuzi huo mbele ya Waandishi wa Habari akisema kumeibuka maneno sehemu mbalimbali hasa mitandaoni wananchi wakidai kuwa Jeshi hilo limeacha kazi yake ya kulinda raia na mali zao na kufanya kazi ya kukusanya mapato ambayo hufanywa na TRA.

“Nimeona watu wengine wanazungumza kwenye mitandao kwamba Polisi wamekuwa kama TRA. Mimi niliweke vizuri, sheria zipo. ukiangalia katika sheria ya Usalama barabarani iko vizuri. Na kama umekamatwa na kosa ambalo tunaamini umekiuka makosa ya Usalama barabarani hatukulazimishi wewe kulipa ile faini. Kuna mawili; kama hauko tayari kulipa ile faini, utaratibu upo tunakupeleka Mahakamani.” – Kamanda Sirro.

Na hii buku ambayo askari wake wa usalama barabarani wanachukua kwenye kila Noah na Hiace huku mikoani isiyo na hata risiti,ni ya nini na inakwenda wapi,mbona hajaigusia?Hivi anataka kutuaminisha kwamba hajui.Ni yale yale tu,ubabaishaji wa WaTz.
 
Police usalama barabarani wanatusumbua Sana kosa si kosa fine hata kosa la kumpa mtu maelekezo wao wanataka fine kwangu mimi police ni kero kubwa sana na siwapendi kabsa
 
Tatizo ww huna hata baiskeli sasa huwez pigwa fine ndo maana unaandika pumba kama hizo
Still inawezekana nyie ndo mnalelewa au hupo kwa shemej yako acha u folo mzee kuna makosa ambayo uwez pigwa fine
Mzee usimlaumu, tatizo ni konyagi ya kupima inawafanya watu wanapinda vibaya sana
 
Fuateni sheria acheni kulialia....saa hizi nimekutana nao kibao na tochi zao, hawajanipata kwasababu najua nini cha kufanya nikifika maeneo hayo.
Mbona unaandika kama "umebebwa" kwenye lift. Ebu angalia hapa alafu uniambie ungekuwa wewe kama ungeandika hayo uliyoandika.

Umetoka nyumbani kwako asubuhi na usafiri wako, ila kabla ya kuondoka ukakagua kila kitu kinachotakiwa kukaguliwa kabla ya kuondoa gari, ukaona kipo sawa. Ukiwa njiani kuna sehemu ulishika breki, taa ya breki ikaungua pasipo wewe kujua. Ukaendelea na safari, njiani ukapigwa mkono na trafiki akakagua gari lako na kuona lipo sawa, isipokuwa tu taa za breki ndio haziwaki, hapo hapo akakuandikia fine ya elfu 30 bila hata maelezo, unahisi utamwelewa, au utafanyaje?
 
duh,power of media,angalia hapo,kuna mic za tbc tu,wenginge wote blogs...eheheh
 
Hizi nazo ni tuhuma za kujibu?

Sasa ndio uone wabongo walivyokuwa ni watu wa ovyo. Tuhuma nyepesi kama hizi ambazo kimsingi ni kejeri wala sio tuhuma, tayari wameshajibu.

Alafu tuhuma nzito za mtumishi wa ngazi ya juu kabisa za kufoji vyeti, wanaita ni tuhuma za kipuuzi na hazistahili kujibiwa kivyovyote.
Nafikiri wakiwa wanafika kwenye tuhuma kama hizo uwenda simu zao zinakata bando au kuishiwa chaji. Maana yote hayo yapo kwenye mitandao na wanayaona kila siku.
 
Hakuna namna, serikali imeanzidha mradi wa kupata 30 30 toka barabarani. Mfano ntu anakusimamisha halafu anasema tairi zimeisha. So lipa faini. Sasa sijui anatumia kipimo gani.
 
Kamanda Sirro issue sio watu kutenda kosa. kwanza kukosa ni hulka ya binadamu yeyote na ndio maana tunaombana msamaha na kwenye dini zote kubwa kuna kipindi cha toba.

Kuna wakati mtu ameamka asubuhi kachelewa kuamka kajisahau kukagua gari yake kama road license ama bima imeisha jana yake. Kwa hiyo anakutana na askari wa barabarani badala ya kumpa onyo na either kumwambia apaki pembeni anunue bima ndio akuruhusu hapo hapo anaandikiwa fine. Pasipokujua ile fine bado haimwondolei huyu mmiliki wa gari hatari atakayoipata ikiwa atapata ajali.

Hivyo badala ya kuwa washauri watoa maelekezo mnakuwa watoza ushuru

Haupaswi kusahau, kosa-faini!
 
Hakuna namna, serikali imeanzidha mradi wa kupata 30 30 toka barabarani. Mfano ntu anakusimamisha halafu anasema tairi zimeisha. So lipa faini. Sasa sijui anatumia kipimo gani.

Askari wanajua kama tairi zimeisha au la kwani ni sehemu ya mafunzo yao!
 
Tatizo ww huna hata baiskeli sasa huwez pigwa fine ndo maana unaandika pumba kama hizo
Still inawezekana nyie ndo mnalelewa au hupo kwa shemej yako acha u folo mzee kuna makosa ambayo uwez pigwa fine
Na hata labda ukoo wao wote hakuna anayemiliki chombo cha usafiri wala mwenye wazo hilo hata kwa miaka 30 ijayo.

Vilevile huenda hana majukumu hivyo akiwa hata ndani ya hiace wakati wakichelewa yeye kwake ni furaha ili akifika akute chakula kimepikwa.
 
Nadhani kupungua kwa mapato huenda kumetokana na watumiaji madereva kuongeza tahadhali na hivyo kukwepa kulipa faini. Pia serikali kuhamia Dodoma kumepunguza idadi ya madereva wanakumbwa na kadhia hiyo.
Hivyo, kwa upande mmoja umakini wa madereva kuongezeka kuna mchango mkubwa . haya ni matokeo chanya.
Polisi wa siku hizi kama utasubiri wakuelimishe, basi kila siku itakula kwako, maana anaanza kuandika kosa hata kabla hajakuuliza.
 
Back
Top Bottom