Kamanda Mpinga: Diamond Platnumz hakufikishwa mahakamani kama dereva wa Singida

Kiujumla amejichanganya sana kwenye kujibu,yani ni pumba juu ya makapi,ukiangalia katika clip zote mbili azitofautiani matukio yake,ingieni Ayo TV muone kituko cha Mpinga,bila kutia shaka huu ndio utendaji wa jeshi la polisi kuna makosa mengi yanafanana ila katika jamii ila maamuzi yake yapo tofauti,kwa mfano aliye na cheo na asiye nacho,mwenye uwezo na asiyenacho na mwenye umaalufu na asiye na umaalufu,Mpinga kwa ili umeteleza.
 
Mzee atajichanganya, tukio ni tukio tu, hakuna kupepesa macho oh eti nini sijui

Nimemsoma tweeter anasema,Dereva wa Singida aliachia usukani na kukaa pembeni ukashikwa na mtu mwingine,wakati Mondi aliachia tu mara moja na baadae kuushika tena

Sasa kwanini alipigwa faini??

Je swala la kupiga nae Picha?

Kamanda mpinga ni jipu liloiva
Kama Kamanda wa Polisi hakupaswa kijichanganya na kijitolea maelezo kihivyo.
Hili jambo halikupaswa kumvuka RTO.
Kufika kwa mkuu wa usalama barabarani na kulitolea maelezo kuna leta "mapicha mapicha".
 
Mkuu naona mtu anatafuta maneno ya kutokea tu, kosadogo kwa ninavyo fahamu mimi nikwamba alietenda hilo kosa dogo anaonywa tu bas na maisha yanaendelea lakini ukipigwa fine ujue nikosa sawa na makosa mengine tu.
Hata Faini nazo zinatofautiana, ipo Notification inayopigwa na Traffic palepale ai anakupeleka Kituoni inalipa kwa kila kosa sh, 30,000/
  • Diamond alikamantwa na Minor offebce ambapo angeweza kulipa kwa M-pesa au Tigo nk kwa wakazi wa Dar kwani alikutwa hajafunga mkanda na aliachilia usukani akisikiliza simu akiwa na familia, alikubali na kulipa 60,000/
  • yule kijana wa Basi la Mamuu Dodoma Manyoni alitoka kabisa kwenye kiti cha dereva na kucheza muziki wakati Basi likitembea zaidi ya mita 200, wakimchukua video
    • walipolalamika walioinasa video, ndipo kukawa hakuna wa kushuhudia ila Mahakama, pale huwezi tena mpiga Notification kwani unatumia video
kwa kawaida Traffic anaruhusiwa kukusamehe kutokana na maelezo yako, kukupiga Fine au kukupandisha zaidi unyang;anywe leseni au kufungwa
 
Hata Faini nazo zinatofautiana, ipo Notification inayopigwa na Traffic palepale ai anakupeleka Kituoni inalipa kwa kila kosa sh, 30,000/
  • Diamond alikamantwa na Minor offebce ambapo angeweza kulipa kwa M-pesa au Tigo nk kwa wakazi wa Dar kwani alikutwa hajafunga mkanda na aliachilia usukani akisikiliza simu akiwa na familia, alikubali na kulipa 60,000/
  • yule kijana wa Basi la Mamuu Dodoma Manyoni alitoka kabisa kwenye kiti cha dereva na kucheza muziki wakati Basi likitembea zaidi ya mita 200, wakimchukua video
    • walipolalamika walioinasa video, ndipo kukawa hakuna wa kushuhudia ila Mahakama, pale huwezi tena mpiga Notification kwani unatumia video
kwa kawaida Traffic anaruhusiwa kukusamehe kutokana na maelezo yako, kukupiga Fine au kukupandisha zaidi unyang;anywe leseni au kufungwa
Kwahiyo ukifanya kosa dogo, unaenda kulipia faini central police na kupiga picha na kamanda wa matrafiki??
 
Ndo silaha ya pekee walobaki nayo CCM ya kuwaombea kura 2020,si unajua Wasanii wote wamewakimbiaaa


Kamanda mpinga kaogopa kutumbuliwa banaaa,aharibu jina la nguvu ya promo 2020

Si unajua WEMA atakaa mita10000 PEMBEN
Hivi kwenye ushindi wa ccm 2015 wema alichangia chochote ninachojua mm ccm tulishindwa ila tuliiba kura na dunia inajua au wema ndo alitumwa kuiba kura chadema walishinda kwa kishindo nyie mnajua na dunia inajua in enl's voice
 
Yeye alijua akipiga picha ataonyesha uma kuwa mondi alifika hahahahahaha upuuzi mtupu mpaka selfie na anahojiwa na mtu mkubwaaaa sisi makapuku ukifika vua mkanda ingia huko
 
Kwahiyo nikiachia usukani mara moja tu napigwa faini ya 60,000Tshs +kupiga picha na Mpinga kisha nasepa
 
Ubaya au uzuri wa tukio unatafsiriwa na mahakama! Kama hakufikishwa mahakamani nani katafsiri uzuri au ubaya wa tukio??
Sheria ya usalama barabarani inawapa polisi mamlaka ya kimahakama ya kupiga faini au kuonya. Lkn sheria hiyo hiyo inampa nafasi dereva au mmiliki aliyeadhibiwa na polisi kukubali adhabu ya faini au kupelekwa mahakamani. Siwakosoi wanaomkosoa Mpinga maana ni haki yao, lkn sheria hii sheria inapotoa uption kama hii ilivyo, maamuzi juu ya uzito wa kosa yanabaki kwa mkamataji ambaye amepewa pia mamlaka nusu ya kihakimu (hata sheria ya wanyamapori nadhani iko hivyo).
 
Sio double standards, mzee yupo sawa kabisa.
Japo fine ya Diamond ni ndogo, 60K kwa kosa kama lile ni uhuni, kuna nchi EU wanakunyang'nya leseni kwa miaka kadhaa kwa kosa kama hilo.

Tukirudi kwa mzee, huwezi sema haya makosa mawili ni sawa, na yupo sawa kusema kua gari modern unaweza achia steering kwa muda, hizi gari zimetengenezwa hivyo, hata ukiachia steering zitaendelea mbele tu bila tatizo lolote, hamjaona gari ka tesla unaachia umbali mrefu mno bila tatizo, zipo nyingi tu za hivyo. Yule dereva its obvious lile gari kubwa na limechoka, alafu alikua mjinga akasimama akatoka kabisa kwenye kiti, mtu na akili zake hawezi fanya ujinga kiasi hiki.

Hakuna double standards, haya makosa mawili sio sawa kabisa.
Jaribu kujificha kwenye kivuli chako. Hapo kajidanganya na wewe unatetea ujinga. Kosa la barabarani halijitofautishi. Huweze sema huyu alikuwa 80 na huyu 85 wakati wanatakiwa 50 sehemu hiyo ukaacha kuwapiga wote faini. Aliyewapeleka wale vijana mahakamani ni polisi wenyewe. Au ukikutwa na bastola na mwenzako smg ambazo siyo halali mtahukumiwa tofauti? Mtu unakamatwa hujafunga mkanda sembuse hiyo
 
Tumeelewa asante. Tumieni walau sekunde moja leo kuwaombea Lema, Lijuakali na walio katika hali kama hizo!
 
Back
Top Bottom