Natural justice
Member
- Aug 15, 2021
- 30
- 47
Jamaa yangu kati ya mwaka 2011 au 2012 aliwahi kuniambia kuwa kigogo mmoja (kwa sasa ni mstaafu) alisema laiti hoja ya kugawa nchi kimajimbo ingeletwa na mwanaccm yumkini serikali ingelichukua wazo hilo na kufikiri namna ya utekelezaji wake, lakini kwa sababu wazo lilitoka upinzani wala hawana muda nalo. Naandika haya nikijua kwamba hoja ya kugawa nchi kimajimbo itachukua muda sana.
Nije kwenye mada, kiukweli mkoa wa Morogoro ni mkubwa sana kieneo napendekeza mkoa ukigawanywa na hili lisichukue muda mrefu, mkoa mpya uitwe Kilombero na wilaya zake ziwe ni Kilombero yenyewe (yenye halmashauri 2 yaani halmashauri ya mji wa Ifakara na halmashauri ya wilaya ya Mlimba), Malinyi na Ulanga. Pia napendekeza makao makuu ya mkoa huo mpya yawe Ifakara.
Kwanini jina Kilombero, kwanza ni jina la moja ya mito mikubwa hapa Tanzania, pili ni jina la kiwanda kikubwa cha uzalishaji sukari hapa Tanzania, tatu ni jina la soko maarufu pale Arusha jirani na NGARENARO (soko la bidhaa za bei chee kwa wakazi wa Arusha mjini). Namaanisha Kilombero si jina geni kwakweli.
Kiukweli kwa hali ilivyo sasa ya mwanachi kutoka Uchindile (Mlimba)au kata za Ulanga zilizopakana na Ruvuma au Lindi kufuata huduma za kimkoa Morogoro mjini ni umbali mrefu sana na kimiundombinu ya barabara mkoa wa Morogoro upo nyuma saaana ukilinganisha na mikoa mingine ambako lami zimetandikwa kisawasawa. Hebu tuwafikirie wananchi hawa kwa kuwasogezea huduma karibu, ikumbukwe kuwa Morogoro ni moja ya ghala la taifa kwa hbr ya chakula na ina mchango mkubwa kwa taifa hasa kudhibiti njaa nchini kwani mazao ya chakula n.k toka mkoa huu hupelekwa sehemu mbalimbali za nchi. Serikali itenge bajeti kutimiza kiu hii ya wanamorogoro.
Hayo ni maoni yangu, naomba kuwasilisha.