Kama kuwaunganisha wananchi ni shida, itawezekanaje kuwaunganisha wanaCCM?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Mpaka hapa kuna kila dalili ya makundi mbali mbali ndani ya jamii kuanza kuishi kwa utengamano kulingana na malezi ambayo yanataka kuanza kumea, kuna kauli za kuudhi na kufedhehesha ambazo zimekua zikitolewa na viongozi wetu zenye dalili za kuvunja mshikamano wetu kama taifa, viongozi wetu wa sasa wanataka tuwaone wakosaji sio kama wanadamu, wanataka tuwatenge na hata walikwishakosea zamani na wakaungama lakini bado wanataka tuwatenge tu.


Kitendo cha kuwaambia wafuasi wa chama fulani wasisalimiane na chama kiingine ni ubaguzi wa hali ya juu, kitendo cha kuwaita watu waliovuna kwa jasho lao mashetani ni ubaguzi, kuwaambia wananchi kua kiongozi flani anyimwe hata pesa za matibabu ikiwa kama stahiki yake ni ubaguzi uliopitiliza. Hakuna mshikamano kabisa zaidi ya kuwagawa wananchi.

Kuna kiongozi mmoja kwenye uchaguguzi wa wabunge wawakilishi bunge la EALA bila haya wala chembe ya aibu alisikika eti akisema mbona chama flani hakuna waislam?mbona kuna watu wa kanda flani tu? Mbona hakuna wazanzibar chama flan? Huu ni ubaguzi unaofanywa makusudi na ukiachwa kuendelea hakika utaligawa taifa.


Kama CCM na viongozi wao wanaongoza kwa kuwabagua wananchi na hata wanachama wao wenyewe uhai wa chama chao una umri gani uliosalia mbeleni?Kama mpaka kumeanza kujitokeza makundi ya wanachama kuongea lugha tofauti ndani ya chama kimoja bado kuna nini hasa? Wataalam wa siasa watalisema hili vizuri kwa maono yao.Pamoja na CCM kua ni taasisi kubwa na yenye historia ya ukongwe wake lakini kuna kila dalili ya hatima ya ukongwe huu.


Kuwatimua viongozi ambao walishakosea miaka miliwili iliyopita kwa makosa ambayo walishatubu bila kuwasamehe ikiwa hata Mungu mwenyewe husamehe dhambi yeyote ile hata ya kuua hukuwezi kijenga CCM zaidi ya kuia, wale viongozi wana watu nyuma yao.Sasa ndio mwanzo wa makundi ndani ya CCM tofauti na wanavyowaza kina Pole pole.
 
mwambieni kwanza Mbowe aache kutembea mfukoni na majina ya wagombea
 
Viongozi wa sasa so viongozi asili,ni wa kuchonga(hawana vipaji vya uongozi). HIVYO ni vigumu kubaini mapungufu hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…