Kama hatuta mdhibiti sasa basi kuna uwezekano mkubwa wa kuivuruga nchi

Okey unashauri tufanye nini kuupinga unduli?
Unduli ni dhana tu mkuu.
Tawala nyingi za kiafrika bado hazina uvumilivu wa kustahimiliana, ni mapema sana kuhusisha utawala uliopo na dhana ya Unduli.
Ni wazi kuwa siasa zetu za maigizo ndizo tatizo.
Cha kufanya ni kurejesha misingi ya nchi Iliyopotea na kuhakikisha kuwa michakato inayowahusu wanasiasa inafanyika ndani ya bunge.
 
Weka bayana kaka kipi kinajiri Pemba?nijuze mdau!


Imefikia kipindi mtu alifiwa na Baba yake ambaye Ni cuf mtoto ccm kaenda kumzika Baba yake, watu wakamwambia wamwachie maiti azike peke yake au aondoke wazike cuf
 
Kuna thread nyingine zinaanzishwa ili mradi tu kuchokonoa utawala,kibaya zaidi wachangiaji wanazishadidia kisiasa.
Kumdhibiti mtu mwenye mamlaka waziwazi ni kuanzisha uasi na vita baridi vya maneno ambavyo havina tija yoyote.
Tuache vimaneno na kutunga sentensi za uchochezi ili tuonekane/kusomwa/kusikika tu majukwaani ilihali tunapanda mbegu mbaya kwa Taifa.
Bora mbegu ipandwe tu kuliko kunyanyaswa, kuonewa na kudharauliwa kwenye Nchi yetu.Haiwezekani ccm wafanye watakavyo halafu watanzania wengine waambiwe wasifanye mambo yao tu kwasababu wameshika dola! Haya Dodoma kulikuwa na ugonjwa, Moshi nako? Hatukubali kuleta ukandamizaji wa watu kwa kusigina Demokrasia.
 
Ngungenge: demokrasia gani ya kumtukana mtu, acha kiongozi, kweupe kwenye kadamnasi. Unategemea nini! Zitto anatoa kauli za uchochezi ati kama CCM haimdhibiti Rais yeye na wao watafanya hivo. Uhuru gani wa kutokuchagua maneno ya kuongea. BAVICHA nao wanatishia kuchukua hatua dhidi ya Polisi, ubavu huo wameupata wapi! Tusijitumbukize kwenye vitendo vya uhalifu kwa kisingizio cha siasa au demokrasia.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Naona umeangalia tatizo badala ya chanzo, sio malaika huyo akikosea lazima asemwe bila hivyo atakuwa anaongoza kiimla.
 
Mbona mnaishia kulalamika humu JF?,hamuoni mnapoteza muda,ingia mitaani mlete fyoko fyoko wawatengue miguu.Raisi ni Huyu Huyu JPM na wengi waliomchagua wapo vijijini na wanazidi kumpa big up Kwa kukandamiza mafisadi mengine mmeyaona yanaongea Uongo Jana.Nyie poteza muda humu JF na threads za kupeana moto ila jua serikali ndo hii hii miaka 9 na nusu ijayo.
 
Nimeamua kuandika thread thii kwa kutambua kua kuna msuguano wa kisiasa na kijamii unaoendelea katika jamii yetu
Pia ni kutokana na tafakari kubwa juu ya hatimaya nchi yetu hapo baadae
Na je nchi hii isipojengwa ndani ya misingi itadumu au itaharibika
Naona kushamiri vitendo vya polisi kutumia nguvu dhidi ya wapinzani na wakosoaji wakubwa wa serikali
Serikali inataka kujengwa katika mfumo wa kimila kwamba haitaki kupingwa na mtu yyt hilo halikubaliki hasa katika dunia hii ya tatu
Serikali hawataki kusiki demokrasia ikishamiri hawataki kuona watu waki challange kuusu maamuzi au mwelekeo wa nchi yao
Hawataki kusiki watu wakijua wamekose
Hatima yake Tanzania itaingia katika hali mbaya ya kisiasa kiuchumi na kijamii, kutokana na hali hii ya kubagua kikundi au watu wa upande fulani
Serikali ya sasa inapalilia uozo huu mwishoni watavuna mabua
Nchi hauweZi kujengwa na watu wa upande mmoja angalia nchi kama libya wananchi wake walipewa kila kitu kasoro demokrasia mwishowe nchi imebaki magofu
Namaliza kwa kusema kama tusiposimama na kukemea kwa dhati basi tutavuna tulichokipanda pale nchi itakapo kataa kutawalika tena

Mkuu Rwanda ilikuwa hivi hivi. Kiliibuka kikundi cha watu wachache ndani ya serikali ambacho kilikuwa kinamzunguka Rais Habyarmana. Kikundi hiki kilijilimbikizia mali nyingi sana na madaraka wakati huo. Nacho kilijenga ngome ya kukizunguka na hakuna kikundi kingine kilichoweza kupeny ngome hiyo.Ili Rais pamoja na kikundi hiki waendelee kujilimbikizia mali na madaraka, walihakikisha kuwa hakuna biashara, ajira, au nafasi yoyote ya uongozi iliyoweza kupatikana bila kikundi hiki kutoa ruksa. Kikundi hiki kilikuwa cha wahutu ambao ndo walikuwa wakiiongoza Rwanda wakati huo, AKazu kilitumia mali walizokuwa wamajilimbikizia kuanzisha jeshi lake, redio yake na magazeti yake, vyombo vilivyotumika kuchochea wahutu wawachukie watusi. Mwisho wake tuliona nini kilichotokea Rwanda. Hiki ndicho Rais wetu anaanza kukijenga katika jamii yetu. Asipojitafakari mwisho wetu siyo mzuri. Ulimwengu wa leo huu usitake kuongoza watu kwa kuwagawa na kuwabaguwa aitha kwa makabila yao, dini zao, au hitikadi za kisiasa. Huu Mpasuko unaoanza taratibu ukifikiwa kiwango cha juu kilichotokea Rwanda siyo ajabu kutokea Tanzania. Tuombe Mungu atupe uzima tu tuyashuhudie yatakayotokea.
 
Huu sio muda wa kufanya maigizo kwenye majukwaa,fanyeni kazi,kama munataka kuandamana nenda mkaandamane kwenye maeneo ya himaya/familia zenu na si maeneo ya umma,HAPA KAZI TU(in magufuli's voice)
Vilaza kama nyie mnaoshangilia mila kitu ndio hatuwataki
 
Tatizo ni hizi pande mbili kutokuweka maslahi ya taifa mbele,upande mmoja unataka kuhakikisha upande mwingine haufanikiwi wakati upande mwingine unataka kuuonesha upande mwingine kuwa wenyew ndio kila kitu.
 
Wakati ukuta ukishindana nao utaumia mwache tuone mwisho wake
Kumuacha tuone mwisho wake ni kuvumilia maumivu. Tutavumilia kwa nuda gani wakati midomo yetu ikifungwa tusiseme (wawakikishi wetu kuzuiwa kusema); macho na masikio yetu yakikosa kuona na kusikia kile wawakilishi walio wengi wanachofanya mjengoni. Uhuru wa kukutana kushereheka au kujadili mustakabali wa taifa ukikabwa.

Tuvumilie udhalimu huu hata lini?

Mungu atujalie hekima na ujasiri, hasa wanasheria na wana harakati. Waongoze harakati za kuizuia serikali isitumbukie babaya.
 
Huu sio muda wa kufanya maigizo kwenye majukwaa,fanyeni kazi,kama munataka kuandamana nenda mkaandamane kwenye maeneo ya himaya/familia zenu na si maeneo ya umma,HAPA KAZI TU(in magufuli's voice)
lazima utakua mnigeria ww
 
Kuna thread nyingine zinaanzishwa ili mradi tu kuchokonoa utawala,kibaya zaidi wachangiaji wanazishadidia kisiasa.
Kumdhibiti mtu mwenye mamlaka waziwazi ni kuanzisha uasi na vita baridi vya maneno ambavyo havina tija yoyote.
Tuache vimaneno na kutunga sentensi za uchochezi ili tuonekane/kusomwa/kusikika tu majukwaani ilihali tunapanda mbegu mbaya kwa Taifa.
punguza woga lazima tuseme ukweli hatuwezi kua na uongozi wa yes boss,kitu cheupe ni cheupe tuu na cheusi ni cheusi tuu nchi haiwezi endelea kwa maamuzi ya mtu mmoja
 
tuache ushabiki penye mapungufu tuseme na panapostahili sifa na pongezi basi zitolewe,
 
Back
Top Bottom