JUVICUF kuhusu safari ya kwenda Buguruni Jumapili

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

JUVICUF NDIO ITAKAYOONGOZA ZOEZI LA USAFI WA OFISI YETU YA CHAMA ILIYOPO BUGURUNI SIKU YA JUMA PILI TAREHE 30 APRIL 2017.

KUHUSU SAFARI YA KWENDA BUGURUNI JUMA PILI.

Ndugu waandishi wa habari, awali ya yote mimi binafsi kama Bobali na mbunge wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, nianze kwa kuwapa pole kwa vurugu na kipigo ambacho mmefanyiwa na watu wahuni wasio na utu wala aibu wakati nyinyi mkia katika majukum yenu ya kazi ya kila siku. Binafsi nimesikitishwa sana na sifikirii kama polisi itashindwa kuwakamata wahusika na kuwafikisha mahakamani mara moja. Lililo jema kwetu , wapenda amani na utulivu ni kwamba wahusika wameirahisishia kazi jeshi la polisi kwa wao wenyewe kuamua kutoka hadharani mbele ya camera zenu na kukiri kutenda kosa hilo.

Jumuiya ya vijana JUVICUF ninayoiongoza imesikitishwa sana na kiukweli butwaa tuliyonayo hivi sasa ni kuona wahusika bado wapo mtaani wakiendelea kunywa kahawa na kutanua huku wakijiona kuwa wao ndio dola na dola ndio wao. Jambo hili likiachwa hivi, litaendelea kulivunjia heshima jeshi letu la polisi na waziri husika wa mambo ya NDANI YA NCHI Mh. Mwigulu Nchemba. Baada ya kutokea kwa tukio hili mimi mwenyekiti wa JUVICUF nilifanya juhudi za makusudi kuwasiliana na waziri Mwenye dhamana kumtahadharisha kuwa jeshi la polisi lisiache jambo hili lipite hivi hivi bila wahusika kuchukuliwa hatua kwani linaweza kupandikiza mbegu na vimelea vya chuki na visasi kwenye jamii jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa taifa letu pendwa la Tanzania. Hivyo bila hata kupepesa macho, JUVICUF inalitaka jeshi la polisi kuwakamata na kuwafikisha mahakamani madereva wote wawili walioendesha magari yaliyohusika katika kufanikisha tukio lile ili wao wawataje watu waliokuwa wakiwaendesha siku hiyo. JUVICUF inalitaka jeshi la polisi kumkamata na kumfikisha mahakamani mtu yule aliekamatwa siku ile ya tukio pale vinna hotel.

Kuhusu safari ya kwenda Buguruni juma pili.

Jumuiya ya vijana cuf imeandaa utaratibu nzuri ambao utawawezesha kila kijana Mwenye nia popote alipo hapa Dar-es-salaam na maeneo Jirani kuweza kufika buguruni. Utaratibu huo mtafahamishwa na mratibu wa vijana juu ya safari hiyo ambayo tumekuwa tukiisubiri kwa muda mrefu. Lengo na nia ya kwenda buguruni katika ofisi kuu yetu ya chama ni kufanya usafi tu na Si vinginevyo. Mnaombwa vijana wote mnaokipenda chama chenu ambao mnamatumaini ya kuiondosha ccm madarakani mwaka 2020 na serikali itakayo wajari na kuheshimu wananchi kupatikana , basi ni vizuri kwenda kufanya usafi katika ofisi yetu ya hapa dar es salaam. Imekuwa Bahati kuwa juma pili itakuwa ni mwisho wa mwezi, hivyo pamoja na nia ya usafi lkn pia tutakuwa tunatekeleza kwa vitendo agizo la Rais (presidential order) ya kufanya usafi kila mwisho wa mwezi.
Na kwanini imekuwa juma pili nadhani inafahamika kuwa tunatarajia sisi wabunge kusafiri siku ya juma mosi kutoka dodoma kuja dar ili juma pili tushiriki zoezi hilo la kihistoria ambalo nadhani kila mwana cuf wa kweli asie na punje ya ukibaraka kwa ccm atapenda kushiriki ili kuwa sehemu ya historia hiyo muhimu katika chama chetu.

Mwisho, tunatoa wito kwa baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakirubuniwa na kutumika na vibaraka wa ccm, kuacha mara moja kutaka kuivuruga cuf. Mafanikio tuliyoyapata mwaka 2015 yanahitaji kulindwa na kuongezeka mara mbili zaidi 2020 . Wenye jukumu la kufanikisha hilo Si wengine ni sisi vijana. Tuache tabia ya kutumika kirahisi rahisi ili kufanikisha maslahi ya watu wachache. Maslahi ya taifa letu linatutegemea zaidi vijana kuliko kundi lolote lile. Tusipoamua kutumia vizuri vichwa vyetu katika kufikiri, vibaraka watatumia nguvu zetu katika kuhofisha juhudi za ukombozi wa taifa letu.
Nape akiwa anaongea na wanahabari hivi karibuni aliwahi kunukuu usemi wa mwanazuoni mmoja usemao " there is nothing , nothing to fear than fear itself ".

Maneno hayo ni mazito na yanapaswa kuwa ni sehemu ya misingi yetu vijana mara zote tunapokusudia kufanya maamuzi mazito na magumu kama hili la kwenda ofisini kufanya usafi baada ya kuiacha ofisi kwa takribani miezi zaidi ya sita hivi sasa.

Ninatanguliza shukrani za dhati. Ahsanteni wanahabari na niwaombe msikose juma pili kuja kushuhudia zoezi hilo la kihistoria.

Hamidu Hassan Bobali (Mb)
Mwenyekiti wa JUVICUF Taifa
Tarehe 27.04. 2017.
 
Ni vema Maalim Seif akaenda Buguruni na kuingia ofisini kwake bila kushirikiana na Lipumbavu. Aende tu tuone polisi watafanya nini.
 
ijumaa kuna kikao na msajili wa vyama ....hivi ulipataje ubunge wewe ?
 
MAONI YANGU: MAADAMU KESI IKO MAHAKAMANI, SUBIRI MAAMUZI YA MAHAKAMA.
HOFU YANGU: MTALETA MAAFA YA VIFO , VILEMA ETC
KWA NINI: POLISI WATATUMIA NGUVU KUPITA KIASI KAMA ILIVYO ADA YAO.
Taarifa zinadokeza kwamba polisi imechoshwa kuchafuliwa na lipumba , sasa hivi imeamua kusimamia haki tu .
 
MAONI YANGU: MAADAMU KESI IKO MAHAKAMANI, SUBIRI MAAMUZI YA MAHAKAMA.
HOFU YANGU: MTALETA MAAFA YA VIFO , VILEMA ETC
KWA NINI: POLISI WATATUMIA NGUVU KUPITA KIASI KAMA ILIVYO ADA YAO.
Hakuna kitu kibaya kama kuwa muoga halafu unawaogofya na wenzako
 
Yangu macho kuona jinsi watu mnavyochakazwa kwa virungu vya polisi, taarifa yako inaonekana kuna kitu kimejificha nyuma ya kufanya usafi huko ila nawatakia Usafi mwema
 
Hakuna kitu kibaya kama kuwa muoga halafu unawaogofya na wenzako
Let us be realistic, polisi wetu mnawafahamu, kwa nini watu wafe wakati kuna kesi mahakamani. Inaweza ikatamka kuwa Lipumba siyo mwenyekiti wala mwanachama. Basi mmeepusha vifo tayari. May be wakitamka vinginevyo, labda hilo mnaweza mkalifikiria in violation of court judgement! Subiri kwanza!
angalia hii please
https://www.jamiiforums.com/threads/police-brutality-in-tanzania-the-world-has-a-right-to-know.19331
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…