Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo ametuma salamu kwa Wapenzi watazamaji wanaowatazama Vijana wa CCM wakisubiri wakosee ambapo amesema Vijana hao hawatokosea na watashambulia kila kona ya Tanzania kuzisaka na kuzilinda kura za CCM pamoja na kugombea kwenye nafasi mbalimbali kupita Chaguzi zijazo.
“CCM kila saa tuna raha tuna furaha kwasababu tunaishi kama Familia moja, namshukuru sana Rais Samia, Chifu Hangaya, Mlezi wa Wana, Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi , Kamati Kuu na Viongozi wengine kwa kunipa heshima sana ambayo sikuwahi kuota katika maisha yangu kunipa nafasi ya kuwa Katibu Mkuu UVCCM”
“Uteuzi huu umenipa fursa ya kuweka historia ndani ya UVCCM kuwa Mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Utendaji Mkuu wa UVCCM, hivi karibuni nilikuwa kwenye viwanja hivi tulifanya shughuli kubwa kama Katibu Mkuu UWT, kwahiyo CCM imenipa nafasi ya kuweka historia ya kuwa Katibu Mkuu UVCCM na historia nyingine ni kwamba nakuwa Mtendaji pekee aliyetumikia Jumuiya mbili ndani ya CCM (UWT na UVCCM)”
“Imani iliyowekwa kwangu ni kubwa sana, sisimami hapa kama Jokate Urban Mwegelo nasimama hapa kwa niaba ya Vijana wote wa CCM, tunawashukuru sana Viongozi wetu kwa kuendelea kuwa na imani na Vijana, Vijana hawa wako timamu, wanajitambua, na tunatambua nafasi ya Vijana kama Wasaka kura wa CCM na hatuishii kusaka kura tunalinda kura zote za CCM”
“Tunatuma salamu kwa Wapenzi watazamaji wanaotazama Vijana wa CCM wakisubiri wakoseee, Vijana wa CCM hatutokosea na hatutofanya makosa, tutashambulia kila kona ya Tanzania kuzisaka kura za CCM kwasababu tunaamini Serikali thabiti, Viongozi imara wanatoka sehemu moja tu CCM”
“Tutatafuta kura za CCM popote zinapopatikana , tutazilinda kwa wivu mkubwa, wanasema raha ya ngoma uingie ucheze, na raha ya dafu sio kunywa kwenye glass au mrija ni kunywa kwenye dafu lenyewe, tutashiriki kwa wingi kwenye Uchaguzi, Vijana tujitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali tukianza na Uchaguzi wa Mwaka huu wa Serikali za Mitaa, Vijana tunakula kiapo tunalinda kura, tutasaka kura na tutagombea”
Ndugu. Jokate Mwegelo
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa
Ameyasema hayo wakati wa mapokezi ya Sekretarieti ya CCM Taifa yaliyofanyika katika Kiwanja cha Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es salaam, Lumumba.
🗓️ 5 Aprili, 2024
📍 CCM (M) Dar es salaam
#CCMImara
#TunaendeleaNaMama
#KaziIendelee