JKT yatangaza majina ya vijana waliohitimu Kidato cha Sita 2022 wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria

xz0r_africa

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
316
313
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2022, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.

Vijana waliochaguliwa wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma - Mara, JKT Msange - Tabora, JKT Ruvu - Pwani, JKT Mpwapwa Dodoma, JKT Mafinga - Iringa, JKT Mlale - Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga, JKT Makuyuni - Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila - Kigoma, JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa - Rukwa, JKT Nachingwea - Lindi na JKT Kibiti- Pwani na Oljoro JKT- Arusha.

Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) waripoti katika kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

jkt 1.png

jkt selection 2.png

majina nimeshare folder kwenye google drive kwa sababu web ya jkt inload sana bofya hapa ku view kwa sasa


PDF ZA MAJINA YA KAMBI ZOTE BOFYA HAPA KU DOWNLOAD

au angali kwa kambi


 
Mimi nilitegemea kijana akienda JKT atarudi na mabadiliko ya kinidhamu, ukakamavu, na uzalendo lakini alivyorudi ni kama hajaenda jeshi nilipomwuliza kwa nini hivyo? Akiniambia kuwa yeye alikuwa kwenye kitengo cha kufayatua tofali lakina zamani enzi zetu haikuwa hivyo.
 
Naomba mwenye kujua atujulishe kuna madhara gani kwa kijana aliyeitwa asipoenda ? What would be the consequences of not attending ?

Nimeuliza hivyo kwa sababu kuna wazazi wanahaha hawana uwezo wa kuwapatia voijana wao hayo mahitaji na hizo nauli. Kwa haraka haraka hayo mahitaji pamoja na nauli ya kwenda na kurudi si chini ya 200K.

Huu wito wao wanaona umekuwa wa ghafla hawakuandaliwa mapema. Ilitakiwa kijana aandaliwe tangu akiwa masomoni kuwa atatakiwa kwenda JKT soon baada ya kumaliza mitihani ya F6.
 
Back
Top Bottom