Fredwash
JF-Expert Member
- Oct 27, 2009
- 1,291
- 1,802
Pamoja na Jitihada za dhati na ZISIZO za dhati za kubadilisha mpira wetu ila ni ukweli usiopingika kuwa Mpira wa tanzania utabadilika ikiwa mambo mawili yatatokea
1. Timu za Simba na yanga ziparaganyike na kufa na kuzaliwa upya
2. Mfumo wa uendeshaji ubadilike kwa asilimia 100, kutoka umiliki wa umma (wanaitwa wanachama) kwenda umiliki wa mtu mmoja au watu wachache.
Wengi wataweza asinielewe au kukubalina na hili ila ki ukweli Bila timu hizi kubadilika basi tusahau mpira kufikia level za wenzetu walau wa afrika ya kaskazin.
wengi wanaweza kuhoji kuwa kwa nini hao watu wachache wasianzishe timu zao, wakumbuke hata huyo Mo alijaribu na Africa lyon ila siasa za mpira wa bongo zilimkwamisha, na yeye sio wa kwanza KAJUMULO alijaribu na Sigara ila yakawa yale yale.
kwa kifupi mtu mmoja hawezi kuanzisha timu ikapata mafanikio makubwa kwani mafanikio ya timu yanategemea sana mfumo mzima wa uendeshaji, Azam amewewekeza pesa nyingi kwenye club, wengi wakajua sababu Azam inaendeshwa kisasa basi itakuwa chachu kwa simba ya yanga kubadilika, ila wamesahau kuwa mfumo wetu wa mpira hapa una siasa ndani yake na ni kama Baba (TFF) mwenye watoto watukutu mapacha (simba na yanga). sasa anamleta mtoto wa nje ama wa ndugu yake ambaye mtiifu mwenye nidhamu akitegemea awabadili hao watukutu.
Ili watoto hao wabadilike ni lazima mmoja wao abadilikie sio mtu wa nje awabadilishe....
Nndo maana Azam ukiondoa mafanikio yake ya kuwa na kiwanja vya kisasa na mfumo wa kisomi bado huwezi kumtofautisha na Simba ama yanga sababu hata yeye anaathirika na mfumo ndo maana hata Ushindani wa nje hafanyi vizuri.
Azam alitakiwa awe level za TP mazembe ila tofauti ni kuwa Congo hakuna timu kongwe zenye mizizi yake kwenye serikali kama hapa.
hapa simba na yanga zina mizizi kwenye siasa za bongo had serikalini tokea miaka ya Uhuru so ili soka la bongo libadilike ni lazima hizi timu zijiondoe huko na haziwez kujiondoa chini ya mfumo wa sasa hivi wa kumilikiwa na Umma (mnawaita wanachama)
Yanga na club zingine watafaidikia na mabadiliko ya simba kwa sababu watawatumia simba kama case study ama reference... maana yangu ni kuwa simba wakianza kujiendesha kwenye huu mfumo watakutana na changamoto nyingi ambazo zitawalazimu kuwa na mabadiliko ya mara kwa mara kwenye uendeshaji. na hili linaweza kuwachelewesha kufikia wanakokutaka.
lakin ndani ya miaka mitatu ijayo yanga kwa kuona simba wamefanikiwa kubadilika bila kujali mafanikio waliopata watafaidika na haya yafuatayo
1. hawatatumia Nguvu nyingi kuwapa somo hao wanaojiita wamiliki (wanachama) wa timu kukubali mabadiliko
2. watatengeneza proposal ya mfumo wa mabadiliko ambayo itachukua mazuri ya simba na yale yenye changamoto yatayaingizwa kweye proposal yakiwa yamerekebishwa au na majibu ya nini kifanyike
3. hakutakuwa na mizengwe ya kupinga mabadiliko tena hasa kutoka kwa viongozi wenye dhamana, kwa influence kutoka serikalini kwani tayari mtoto mmoja ameruhusiwa huyu wa pili haweza kuzuiwa (kumbuka club hizi zina miziz kwenye serikali ndo maana majibu ya BMTL mwaka jana wakati vilabu hivi vilipoonyesha nia walidai wanaotaka wakaanzishe vilabu vyao,)
4. Walau robo tatu ya club za ligi kuu zikiwa na mfumo huu ni basi ni rahisi kwa TFF kubadilika kwani hakutakuwa na makandakando ya vilabu kwenye uongozi wa TFF hiyo itapelekea club kuwa na nguvu na kuibana TFF kwenye misingi ya soka mwishoe TTF itabadilika , mfani kuruhu kuwe na chombo kitakachoendesha Ligi kuu kisasa na TFF kubaki msimaizi wa mpira ( mfano ligiya uingereza) ama walau hapo jirani kenya
Bila kujali nani atachukua hisa nyingi simba ( Mo ameonyesha nia) basi ikiwa atakayechukua ataweka misingi imara ( kama ilivyo kwa Moïse Katumbi wa mazembe) basi ndani ya muda mfupi timu itafika mbali.
Nawapongeza Simba kwa kufikia hapa, nilitegemea upinzani mkubwa ila nimeshangazwa na upinzani mdogo na uliozimwa bila kelele... Hata ikitokea mwekezaji akashindwa,. chukulia mfano ndani ya miaka 5 ijayo walau nusu ya timu za ligi kuu zibadilike kwenye mfumo huu inamana hata kama akitokea mwekezaji wa simba akashindwa basi anaweza akauza hisa zake kwa mwingine kwani tayari mwamko utakuwa mkubwa
Mungu ibariki safari hii kwani ni ya wapenda soka wote bila kujali Ushabiki au uanachama wa club... tunapenda kuona timu yetu ya taifa ikishiriki kombe la dunia kama vile inashiriki CECAFA (mara kwa mara). na tunapenda kuona kwenye misimu ya usajili dunia wahcezaji wetu wananunuliwa au walau kutajwa tajwa na club za ulaya