Jinsi ya kuiweka Business yako Mtandaoni kiusahihi

NgimbaErick

Member
Mar 31, 2020
85
134
Inawezekana umegundua kuwa watu wengi sana miaka ya leo wanashinda mtandaoni kuliko mtaani, lakini hujui namna ya kuiweka biashara yako hukoo mtandaoni katika namna ambayo itakuwa na faida kwa upande wako.

Au, labda umejaribu kuiweka biashara yako mtandaoni, labdaa … umetengeneza website, umefungua social media accounts unatangaza kupitia zoom, jamii forums na sites zingine zigine za classified ads… lakini bado hamna cha maana, unakuta mda wako unaotumia kuyafanya hayo yoote unaonekana sio sawa kabisa na faida unazozipata kutoka mtandaoni.

Basi mi ntakuambia mambo muhimu sana ambayo inabidi uyafanyie kazi…na haya ni mambo ambayo Mimi mwenyewe napenda kuyafanya nnapotengeza Biashara mpya mtandaoni, najribu ku-share tu kile ambacho kwangu kinafanya kazi. So….

  1. Hakikisha Una Website Nzuri.
Nnapoongelea website nzuri namaanisha Website yenye viwango bora baadhi ya vitu vya kuzingatia unapotengeneza website yako ni hivi;
  • Muundo wake uwe wa Kisasa, na siyo kama websites za kizamani. Fanya muundo wa website yako uendane na muda tuliopo na hili unalifanyaje? Kwa kufanya uchunguzi kupitia websites za Kampuni au Biashara kubwa na maarufu, angalia vitu wanavyofanya na ujifunze hapo.
  • Muonekano wa Website yako uwe mzuri kwenye Vifaa vyote vya Intaneti, Simu, Computer na Table. Hili ni janga la wengi sana, watu wengi wanatengeneza Websites lakini hawajui kwenye simu zinaonekanaje, wakati watumiaji wa intaneti zaidi ya 51% watumia simu kuingia matandaoni.
  • Jitahidi ulifanyie kazi sana hili la sivyo unapoteza wateja wengi kwa sababu wakiingia kwenye website yako wanakuta vitu havina mpangilio unaoelekweka.
  • Kitu kingine website yako Iwe Rahisi Kuleweka pale mtu anapotaka kufanya jambo lolote. Hii nayo ni shida ya wengi sanaa. .. Jitahidi website yako iwe na mtirirko utakaomfanya mteja asiwe na maswali mengi na kuumiza kichwa anapohitaji kitu.
  • Kumbuka kuwa mtu anapokuja kwenye website yako anajua anachokihitaji na wewe unajua unachokiuza sasa usiifanye kazi ikawa ngumu weka njia nzuri kwa mtumiaji.
  • Unapoweka Uelekeo mzuri kwa watumiaji wa website yako inakusaidia kuikuza na kuifanya kuonekana kwa watu wengi zaidi kwa sababu ya wepesi wake (yani Good User Experience).
  • Vitu Vingine ni kama Hakiikisha Website yako ina Fungua fasta, social media za biashara yako usizisahau, maneno yote yawe yanaonekana n.k, yapo mengi ila hayo ni muhimu.
  1. Hakikisha unakuwa na Website Management nzuri.
  • Hili ni suala ambalo pia nimeligundua hivi karibuni wafanya biashara na makampuni mengi, hawana website management. Website Management hali ya kuwa na usimamizi website yako ili kuhakikisha inafanya kazi vizuri mda wote.
  • Labda kama hujui, websites zinahitaji wanagement sana kwa sababu ya mabadiliko ambayo yanatokea mara kwa mara mtandaoni ambayo yanaweza kupelekea madhara ya website yako kutokuonekana na kushindwa kufanya kazi vizuri.
  • Vilevile Management itakusaidia kujua Ukuaji wa Biashara yako mtandaoni kupiti namba ya watu wanaotembelea Website yako kila mwezi, itakusaidia kukusanya taarifa ambazo unaweza ukazitumia unapotaka kufanya matangazo mtandaoni.
  1. Hakikisha unatumia Business Email ( mf; info@itv.co.tz) na siyo za Bure kama hizi ; gmail, yahoo hotmail n.k
  • Hii itakufanya uonekane Mtaalamu na Inaifanya Biashara yako kuonekana halali (Good Brand).
  • Unajua unaweza ukawa huna jengo zuri la biashara au kampuni yako lakini Mtandao ukakufanya uonekana Bonge la Biashara au Kampuni, kama kweli ukifanya vitu kwa ustadi. Wapo watu hawana ofisi halisi ila wa Website tu na Biashara zao ni Kubwa sana.
  1. Unapokuwa Mtandaoni Usipende kutangaza Bidhaa au Huduma zako sana.
  • Hapa ndo watu wengi wanafeli inapokuja kwenye swala la kufanya biashara mtandaoni. Wengi wanataka tu kuuza lakini thamani ya kile wanachokiuza haionekani.
  • Unapouza kitu kwenye mtandao inahitaji uuze kwa akil, ili uweze kufanikiwa sana. Fanya hivi… Anza kuonesha Thamani ya kile unachokifanya ili watu waelewe umuhimu wake kisha wakiitaji taarifa zaidi unaweza ukawapa na bei sasa.
  • Mfano; Mimi ni Daktari wa Meno na nina Clinic yangu, angalia sasa utofauti kati ya njia mbaya na Njia nzuri.
  1. NJIA MBAYA: Kila Siku Naandika kwenye website yangu na social media zangu, Mimi ni Daktari bingwa wa meno natibu tatizo lolote lile na leo natoa punguzo la asilimia 40%..... Hii haitakupa wateja bora na wakudumu kwanza unajishusha thamani tu.
  2. NJIA NZURI: Kila siku natoa somo jipya kuhusu afya ya meno na ninatoa nafasi kwa watu wenye maswali na wanaohitaji ushauri…. Kitakachotokea ni kwamba watu watanitafuta ili wapate suluhisho la matatizo yao na hapo sasa unadhani nashindwaje kutaja Bei yangu Iliyoshiba hahaha kwa sababu wamenifata sijawaita…
5. Anza kufanya Email Marketing kama ulikuwa hufanyi (Fursa!)
  • Zaidi ya watanzania Laki 1 mpaka 1M wanafungua email zao kila mwezi kuangalia taarifa mbalimbali.
  • Emails ni bora kuzidi social media kwa sababu,
    • Emails unazimiliki wewe ila Social media Followers huwamiliki, leo hii account yako ikifutwa huna cha kufanya hamna Backup, ila Emails unaweza ukazitunza sehemu zote uzitakazo hata ukizifuta bahati mbaya, unaweza ukazipata popote ulipozihifadhi…..
    • Emails zinamfata mtu kwenye inbox yake na hivyo zimekaa kiusiri, zinamfanya mtu aone jinsi unavyomthamini na zinaonekana kiutalaamu zaidi. Ila social media unapoweka kitu kinakuwa hadharani na thamani yake haiwezi kuonekana sawa na emails hata kidogo.
    • Kwenye Emails wewe ndiyo unaamua cha kufanya, unaweza ukasema leo nawatumia hawa tu, na wasipofungua nawatumia tena, n.k lakini social media huna uwezo huo tena kunakitu kinaitwa “Algorithim” yani waweza ukawa una Followers 10,000 lakini ukipost like 11 tu, mwezi mzima…
    • Kuna faida nyingi sana unaweza ukaGoogle utaziona kabisa..
    • Na uzuri sasa hivi kuna web applications zinazokuwezesha kufanya kazi ya kufanya Email Marketing kwa urahisi zaidi, kwamba kila kitu kinafanyika automatic kabisa, hizi apps zinaitwa Autoresponder, unaweza ukaGoogle kupata taarifa zaidi.
6. Penda Kusoma Tabia za Wateja wako wanapokuwa kwenye website yako, ili ujue namna ya kuendana nao.
  • Hichi ni kitu ambacho ni cha level ya juu kidogo na siyo kitu rahisi kusema ukweli. Inahitaji ujifunze hata kwa miezi kadhaa ili uweze kukifanya vizuri.
  • Lakini ni kitu muhimu sana ambacho watu wenye websites kubwa wanakifanya, na kikubwa wanachokifanya wanaweka codes ambazo zinakuwa zinafuatilia tabia ya kila mtu anapoingia kwenye website yake… na hivyo wanatumia taarifa watakazo zipata ili kunufaika kwa upande wao.
  • Mfano: kwenye website yako una Kitu unauza alafu mtu amekiona kisha akakichagua akaandika taarifa zake zote … lakini alipofika kwenye hatua ya malipo akaacha, mimi sifahamu sababu ni nini, ila kwa kutumia codes ambazo zimewekwa kwenye website yako unaweza ukamtumia email yule mtu ukamwambia kwamba hajamalizia kulipia na unaweza ukampa hata punguzo inawezekana bei ni kubwa kwake.
  • NAdhani umepata picha kidogo sasa sio lazima iwe unauza kitu, unaweza ukatumia njia hii kwa kufanya mambo mengi na ni kitu muhimu sana, kama wewe unauza kitu chochote.
7. Hakikisha unatumia Picha Zenye Ubora mzuri, itakusaidia sana kunasa macho ya watu, wanapokuwa kwenye website au social media zako.
  • Hili suala, usilichukulie kawaida ni heri uingie cost ya kununua camera gharama, ili uweze kulifanya hili.
  • Watu wanavutiwa sana na picha zilizo na ubora wa hali ya juu.
  • na pia itaifanya biashara au kampuni yako kuonekana ya Thamani
  • NB: Usipende Kutumia picha za Google, zinakushushia Hadhi kwa sababu hazioneshi uhalisia na pia watu wengi wanazitumia hizo picha za Kudownload mitandaoni... Picha Halisi na zenye Ubora zitakufanya uonekane Bora Mara zote.
Ntaishia hapo kwa leo mambo yapo mengi sana ambayo unahitaji kufanya ili Business yako iwe yenye faida inapokuwa Mtandaoni.

Erick Ngimba
Uwe na Siku njema.
 
Back
Top Bottom