SoC03 Jinsi ya kufanya utatuzi wa ajira nchini

Stories of Change - 2023 Competition

Njile bushokero

New Member
Jul 3, 2023
2
1
Habari zenu watanzania.

Ninajivunia kuwa mtanzania, pia ninayo furaha kupata fursa hii, ili na mimi nitoe mawazo yangu katika ujenzi wa nchi yetu. Asanteni sana mlioandaa shindano hili, siyo tu kwamba kujishindia zawadi, bali, tuna tunatazamia mabadiliko chanya, na uwajibikaji katika sekta mbalimbali nchini.

Katika mada. Ebu tutoe elimu ya kujitegemea kwa jamii, ili tupunguze ukosefu wa ajira nchini. Katika vyuo vikuu na vyuo vya ufundi. Kuwepo na mitaala ambayo inaelezea umuhimu wa mwajiriwa kujiajiri na umuhimu wa yeye kuzalisha ajira katika kazi aliyo jiajiri. Hapa tunazungumzia umuhimu wa mtu binafsi, katika kutatua suala la uhitaji wa kazi, na kuwa muajiri au kutengeneza ajira kwa wengine pia.

Kujenga ufahamu wa kujitegemea kwa jamii ni muhimu sana na ni lazima kama tunataka nchi ya ujamaa, na uchumi wa kujitegemea, lazima tuwaambie waajiriwa kwamba kazi walizo nazo, siyo suluhu la wao kuwa na uchumi imara, bali kama kila mmoja wao katika kazi aliyo ajiriwa, awekeze lengo la kujiajiri mwenyewe, hilo ndilo suluhisho sahihi la uchumi wao, na uchumi wa nchi pia.

Kwa sababu baada miaka fulani atajiuzulu kazi aliyo ajiriwa, na kwa uzoefu alionao kupitia ajira aliyo ipata awali, ataanzisha kazi yake, nafasi aliyo iacha kule msomi mwingine mwenye taaluma kama yake ataichukua nafasi hiyo, na hili ndilo suluhu la ajira litakavyokua limepata mwarubaini wake.

Kazi ya huyu msomi aliyoianzisha, ni lazima nayo izalishe ajira, pia naye atahitaji wasomi wa kuwaajiri. Kama amefungua kiwanda je; hatahitaji wasomi wenye taaluma hiyo? Kama amefungua kituo cha afya je; hatahitaji wasomi wenye taaluma hiyo?

Kama amefungua shule je; hatahitaji wasomi wenye taaluma hiyo, Kama amefungua kituo cha redio je; hatahitaji wasomi wenye taaluma hiyo? Na kama amefungua kampuni ya ujenzi je; hatahitaji wasomi wenye taaluma hiyo, Kama amefungua kampuni ya kilimo je; hatahitaji wasomi wenye taaluma hiyo?, chochote atakacho kifanya kitahitaji ushirikiano na wengine ili kiende.

Katika sekta mbali mbali, nchini, iwapo Tu tutajenga kujitegemea, na jamii kuipatia nafasi hiyo, hakika kila sekta iko na mwendelezo wa ajira. Na katika mpango huu, ushindani mkubwa na ufanisi utaongezeka kila nyanja, ukizingatia kwamba kila mmoja atahitaji kujituma zaidi ili kitu chake kiende.

Hata hivyo nimezungumzia kuhusu sekta binafsi, na namna ambavyo itatatua suala la ajira nchini, kwa hiyo serikali iko wapi katika hili? Serikali iko hapa. Maana yenyewe serikali ndiyo mama wa huu mpango. kwa sababu serikali haitaweza kutatua suala la ajira kwa kumu ajiri kila mhitimu, hivyo hili suala litapelekwa kwa sekta binafsi, ili likapate ufumbuzi. Hivyo kazi ya serikali itakuwa ni kutoa elimu hii kwa jamii na jamii inatekeleza.

Hivyo basi, jukumu la serikali, ni kuleta mazingira mazuri na rafiki, kwa sekta binafsi, ili kuuwezesha mpango huu, kuwa wenye mafanikio. Pamoja na hayo, uwajibikaji na utekelezaji sahihi, uendane na matakwa ya mpango huu. Ili kusiwepo na hitilafu lolote lile, katika ufanikishaji wake.

Hivyo serikali inapaswa iwe na sera mbadala, katika kuwalinda wawekezaji wa ndani, na kuheshimu uwepo wao katika jukumu hili la kutengeneza ajira. Na katika kufahamu kwamba, utakuwa ni mpango wa muda mrefu, na ni mwendelezo usio na kikomo, ni lazima kuwepo na sheria, inayo fahamu mpango husika wenyewe. Ili kusiwepo huu ukakasi wa kwamba, baada ya utawala kubadilika, utawala mwingine uje na maono yake, la, bali iwe ni sheria ya kuifuata kizazi hadi kizazi.

Zingatio katika mpango huu, ni kwamba, nilazima kila kazi iwe na leseni inayo tolewa na serikali, haijalishi iwe kibanda cha nyanya, ni lazima kila shughuli ihesabiwe kama kazi au ajira. Ili kujilinda na kazi hewa au ajira hewa. Hata hivyo pendekezo langu katika kulipia ushuru wa nchi,, mapendekezo yangu ni kuanzia mtaji wa kiasi Tshs laki tano 500,000, na kuendelea juu.

Pamoja na hayo yote, jamii ni lazima ielimishwe kuhusu bima ya kazi husika au mtaji, kwamba baada ya kutokea janga lolote kazi husika bima itashughulikia uharibifu wowote, baada ya kuwaelimisha kuhusu majanga kama ya moto na n.k., ndipo tuta waambia kuhusu kuwa na akaunti za bima ya biashara zao. Kwamba kila asilimia moja 1, ya pato la mwezi, itaenda kwenye bima ya biashara.

Ili kulinda mtaji au kampuni husika na wafanyakazi wake, pale janga lolote litakapo jitokeza ili kulinda maslahi ya kazi husika. hii iwe kama sera muhimu sana katika mpango huu, ili kupunguza biashara au kazi au ajira za kuishia njiani bila kutimiza malengo.

Hata hivyo utoaji wa bima hii utaendana na biashara husika. Kwa sababu kila biashara ina kiwango chake cha mapato kwa mwezi. na bima hiyo tunaweza kuitumia kutatua changamoto za mishahara kwa wafanyakazi kwa asilimia 50 ya bima, na na asilimia 50 nyingine inaweza kutumika kama deni kwa muajiri, (anadaiwa) kama inaweza kutokea uvunjifu wa haki za kazi.

Zaidi sana ninapendekeza pia kuhusu suala la mikataba makazini, hili nalo liwe jambo muhimu sana katika kazi yoyote iliyo sajiliwa na serikali. Ili pale kutakapokuwa shida yoyote kati ya mwajiri na mwajiriwa, mkataba walio saini uweze kuamua. Na hii ni kwa sababu tunataka kujilinda na kazi za kishikaji, hivyo kanuni na taratibu za mikataba ziwe wazi na kueleweka kabla hawajasaini.

Inaweza kuwa kama ndoto. Lakini mimi ninaamini kabisa kwamba kama tutaamua bila shaka tunaweza kufanikisha mpango huu, na kutatua suala la ajira nchini kabisa. Kikubwa ni ushirikiano na umoja wa ari ya kumaliza tatizo lililopo. Kama tutaamua bila shaka Tanzania tutakuwa mfano kwa nchi zingine.

Mungu bariki andiko langu lipate kibali cha utekelezaji, Mungu ibariki Tanzania na watu wake. Amina!
 
Back
Top Bottom