Jinsi ya kuandaa mkataba kati ya mpangaji na mpangishaji wa nyumba za familia

Aliko Musa

JF-Expert Member
Aug 25, 2018
209
304
Kumbuka kuwa thamani ya nyumba ya biashara inaweza kuathiriwa na muda wa mkataba wa upangishaji wa nyumba husika.

Nyumba ya biashara yenye mkataba wa upangishaji wa miaka mingi inakuwa na thamani kubwa ukilinganisha na nyumba ya biashara yenye mkataba wa miezi michache tu.

Vilevile jambo hili linaweza kuwa sawa kwenye nyumba za makazi ya familia. Hivyo unahitaji kuzingatia muda wa kuingia mkataba wa upangishaji wa nyumba za familia ili kutoathiri kipato endelevu.

Hutakiwi kuingia mkataba wa upangishaji wa zaidi ya miaka mitano kwa sababu huwezi kupata makadirio ya ongezeko la thamani ya nyumba yako zaidi ya miaka mitano ijayo.

Unapopata mpangaji wa muda mrefu. Unatakiwa kuingia mkataba wa upangishaji wa miaka mitatu hadi miaka mitano.

Mikataba ya upangishaji ya zaidi ya miaka miwili (miezi 24) inatakiwa kuwa na kiasi tofauti tofauti cha kodi kwa kuzingatia ongezeko la thamani ya nyumba husika.

Mfano; kama nyumba ya familia inapangishwa kwa Tshs.200,000 kwa kila mwezi. Basi kodi hii inatakiwa kubadilika angalau kila baada ya miezi 24.

Kila baada ya miezi 24 unashauriwa kuongeza 03% hadi 10% kutegemeana na hali halisi ya ongezeko la thamani ya nyumba yako.

Kwenye ukurasa huu nimekushirikisha mifano tofauti tofauti ya mikataba halisi unayoweza kuitumia kwenye upangishaji wa nyumba za familia (Family rental houses).

MFANO; Mkataba Wa Kupangisha Chumba/Nyumba Za Familia.

MKATABA WA UPANGISHAJI WA NYUMBA YA KUISHI YA FAMILIA

Mkataba huu umefanyika siku ya tarehe 24 ya mwezi wa NOVEMBA mwaka 2021.

KATI YA ENITHA P NDYUMBA wa sanduku la posta ..., Tukuyu-Mbeya ambaye ndani ya mkataba huu anajulikana kama MWENYE NYUMBA (MPANGISHAJI).

NA

Ezekiel J Joseph wa sanduku la posta ...., Songea ambaye ndani ya mkataba huu anajulikana kama MPANGAJI.

Na kwamba MPANGISHAJI amekubali kwa hiari yake kumpangisha MPANGAJI aliyetajwa hapo juu.

Na kwamba MPANGAJI amekubali kwa hiari yake mwenyewe kupanga kwenye nyumba iliyotajwa kwa kipindi cha miezi ishirini na nne (24) kwenye mkataba huu kuanzia siku ya tarehe 02 ya mwezi DISEMBA mwaka 2021 hadi siku ya tarehe 02 DISEMBA mwaka 2021.

Mkataba Huu Unashuhudia Kama Ifuatavyo;-

(01) Kiasi cha kodi ya pango la nyumba.

Kiasi cha kodi ya pango kwa ajili ya upangishaji wa nyumba ni shilingi za kitanzania ELFU HAMSINI (Tshs.50,000/=) kwa kila mwezi ambapo jumla yake ni shilingi za kitanzania milioni moja na laki mbili tu (Tshs.1,200,000/=). Kiasi hiki kitalipwa kwa mkupuo mmoja tu kupitia namba ya simu 0752 413 ... (Majina ya M-pesa ni ENITHA P NDYUMBA).

(02) Mkataba unapoisha.

Mkataba huu umekubaliwa kwa kipindi cha miezi ishirini na nne (24) na mkataba unapofikia tarehe ya mwisho, mkataba huu unaweza kuhuishwa kwa masharti na makubaliano yaliyopo kwenye kipengele namba sita ndani ya mkataba huu.

(03) Uthibitisho wa MPANGISHAJI.

MPANGISHAJI anathibitisha na anamhakikishia MPANGAJI kuwa yeye ni mwenye nyumba halali ya nyumba aliyopanga.

Pia, MPANGISHAJI anamthibitishia MPANGAJI kuwa katika muda wa mkataba huu MPANGAJI atatumia nyumba bila kuingiliwa na mtu yeyote endapo masharti na makubaliano yaliyomo kwenye mkataba huu.

(04) Majukumu ya mpangaji.

MPANGAJI anakubaliana na anamhakikishia MPANGISHAJI kama ifuatavyo;-

(a) Kwamba MPANGAJI atalipa jumla ya kiasi cha kodi ya pango la nyumba kwa mkupuo kwa kupitia utaratibu unaokubalika ndani ya mkataba huu.

(b) Kwamba MPANGAJI atatumia nyumba hiyo kwa ajili ya malazi tu na sio matumizi mengine.

(c) Kwamba anakubali kutotoboa ukuta wa nyumba au kubadilisha rangi ya ukuta (au paa ) wa nyumba bila kupata ruhusa kutoka kwa MPANGISHAJI au msimamizi wa nyumba.

(d) Na kwamba MPANGAJI atalipia gharama za matumizi ya umeme ya nyumba aliyopanga kupitia mamlaka ya umeme iitwayo TANESCO.

(e) Kwamba MPANGAJI atalipia gharama zote za bili ya maji kwenye mamlaka husika.

(f) Kwamba MPANGAJI atahakikisha nyumba aliyopangishwa kuwekwa katika hali nzuri ya nje na ndani ya nyumba katika kipindi chote cha upangaji.

(g) Pia, MPANGAJI atahakikisha kuwa mazingira yanayozunguka nyumba yanakuwa katika hali nzuri na hali ya usafi katika kipindi chote cha mkataba huu.

(h) Kwamba hatampangisha mtu yeyote chumba au sehemu yoyote ya nyumba aliyopanga bila kupata ruhusa kutoka kwa MPANGISHAJI.

(05) Majukumu Ya MPANGISHAJI.

MPANGISHAJI anakubaliana na anamhakikishia MPANGAJI kuhusu mambo yafuatayo;-

(a) Kwamba MPANGISHAJI atalipa kodi ya pango la ardhi na kodi ya pango la nyumba na kodi nyingine inayohusiana nyumba.

(b) Kwamba MPANGISHAJI anamthibitishia kuwa MPANGAJI kuwa atatumia nyumba kwa uhuru bila kuingiliwa na mwakilishi au mwenye nyumba kipindi chote cha mkataba huu, masharti na makubaliano ya mkataba yanapozingatiwa.

(c) Na kwamba MPANGISHAJI atakuwa anafanya ukarabati na marekebisho ya nyumba kila inapohitajika. Pia, taarifa ni lazima itolewe kwa MPANGAJI kabla ya kuingia kwenye nyumba kuanza kufanya ukarabati na marekebisho.

(d) MPANGISHAJI ana haki ya kuingia kufanya ukaguzi wa nyumba kabla ya kuanza ukarabati au marekebisho ya aina yoyote na MPANGAJI hutotakiwa kutotoa ruhusa bila kuwa na sababu za msingi.

(06) Makubaliano Ya Pande Zote Mbili.

Imekubaliwa na pande zote mbili (MPANGAJI na MPANGISHAJI) kwenye mkataba huu kama ifuatavyo;-

(a) MPANGAJI atatakiwa kutoa notisi ya muda wa siku tisini (90) kabla ya kufikia tarehe ya mwisho ya mkataba huu endapo yupo tayari kuingia mkataba mpya au hataendelea kuishi kwenye nyumba yako.

(b) MPANGISHAJI anaweza kumruhusu MPANGAJI kusaini upya mkataba huu endapo masharti na makubaliano ya mkataba unaoisha yamezingatiwa vizuri kipindi chote cha upangaji.

(c) Vitu vifuatavyo vimekabidhiwa kwa MPANGAJI tangu siku ya kuanza kutumika kwa mkataba huu;-

✓ Meza moja ya kupikia jikoni.

✓ Viti vinne (04) vya plastiki vyote vina rangi ya kijani.

✓ Kapeti moja zito lenye UREFU mita 20 na upana MITA 15 na lina rangi nyekundu. Na lina kilogramu 10 likipimwa bila kuwa na unyevunyevu au maji.

✓ Seti tatu za kochi, ya kwanza ya kukalia watu wanne, ya pili ya kukalia watu watatu na ya tatu ya kukalia watu wawili.

✓ Kabati moja la nguo lenye UREFU wa sentimita 50, UPANA wa sentimita 20 na KIMO cha 150.

Maelezo Mengineyo.

Nakala moja ya mkataba huu atabaki nayo MPANGISHAJI na nakala ya pili atabaki nayo MPANGAJI.

Mkataba huu umeshuhudiwa na kusainiwa mbele ya MPANGAJI, MPANGISHAJI na mashahidi wawili.

MPANGISHAJI.

Majina kamili: ENITHA P NDYUMBA.

Tarehe: 24 NOVEMBA 2021.

Sahihi ..............................
MWENYE NYUMBA.

MPANGAJI.

Majina kamili: Ezekiel J Joseph.

Tarehe: 24 NOVEMBA 2021.

Sahihi .......................
MPANGAJI.

SHAHIDI NAMBA MOJA.

Majina kamili: Juma K Asubuhi.

Tarehe: 24 NOVEMBA 2021

Sahihi .....................

SHAHIDI NAMBA MBILI.

Majina kamili: Daudi O Simfukwe

Tarehe: 24 NOVEMBA 2021

Sahihi .....................

Mwandishi,

Aliko Musa
 
safi sana
asanteee.

wanaohitaji nyumba kitunda machimbo, DSM
mje tuyajenge ina vyumba viwili luku inajitegemea
0653171045
kodi laki2
haina udalali
 
Ngoja ni kopi hii contract.Ni nzuri sana.Shukrani nyingi kwako bwana Ali Musa
 
Nakutafuta boss unakitu wewe nakihitaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…